Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 29 Shawwal 1441 | Na: 1441 / 71 |
M. Jumamosi, 20 Juni 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kufuata Maagizo ya IMF, Serikali ya Bajwa-Imran Imebwaga Mlima wa Deni la Mzunguko Vichwani mwa Watu
Serikali ya Bajwa-Imran imewasilisha mswada katika Bunge la Kitaifa kurekebisha Sheria ya NEPRA ya 1997, kwamba NEPRA (Mamlaka ya Kitaifa ya Udhibiti wa Umeme) inaweza kutoza ada ya ziada kwa watumiaji umeme ipendapo. Serikali ya Bajwa-Imran imefanya hivyo kufuata maagizo ya IMF. IMF imeweka masharti kwamba deni la mzunguko la sekta ya kawi lazima lipunguzwe hadi Rupia bilioni 50 hadi 75 kwa mwaka ifikapo 2023, ambapo kwa sasa ni Rupia bilioni 456 kwa mwaka. Zaidi ya hayo, deni jumla la mzunguko lililokusanywa ni takriban Rupia bilioni 1800. Sehemu kubwa ya mlima wa deni hilo la mzunguko ni kutokana na hasara za laini za usambazaji, bili zisizolipwa na riba kubwa, ambayo sasa itawekwa kama mzigo juu ya watu. Tangu kuingia madarakani, serikali ya “mabadiliko” tayari imeongeza gharama ya umeme kwa angalau asilimia 12.5 na hadi asilimia 30 kulingana na matumizi.
Kwa kuongezea, kwa kipindi cha miaka mitatu, sekta hii hairuhusiwi kuzalisha umeme wa bei ya nafuu, kuupa mzigo mkubwa uzalishaji na kudhoofisha ushindani. Kwa hivyo, serikali ya "mabadiliko" inauangusha uchumi unao ng'ang'ana na watu hadi chini, ili kuwatii mafia wakoloni wa kimataifa. Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan inalaani vikali serikali hiyo kwa ukandamizaji ambao unanufaisha tu wawekezaji wa kimataifa na wa ndani katika sekta ya kawi.
Asili ya deni la mzunguko katika sekta ya kawi ya Pakistan ni rundo la makubaliano yaliyo fanywa na wazalishaji kawi wa kibinafsi. Kupitia makubaliano haya, mabilioni ya Rupia ya faida za uzalishaji umeme huingia mifuko mwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, badala ya hazina ya serikali. Fauka ya hayo, kiwango cha chini cha gharama ya umeme kimekisiwa kwa makadirio ya juu, huku mabilioni ya rupee yakitozwa kila mwaka kama "malipo ya uwezo." Malipo ya uwezo hulipwa kwa vitengo vya uzalishaji wakati vikiwa havizalishi, au vina zalisha chini ya uwezo, nyakati za upungufu hitajio kutokana na sababu za kimsimu au nyenginezo. Malipo ya uwezo hupigiwa hesabu ili kulipia malipo ya mkopo wa benki, gharama za kudumu za uendeshaji na faida kwa wazalishaji huru wa kawi. Kwa mujibu wa ripoti ya Julai 2019, malipo ya uwezo yamepanda hadi rupia bilioni 900 kwa mwaka. Sasa, mzigo mzito wote sasa utaporomoshwa vichwani mwa watu.
Chini ya nidhamu ya kidemokrasia wa kirasilimali, Waislamu wa Pakistan kamwe hawatapata umeme kwa bei ambayo inapunguza gharama za mapato ya tasnia, kilimo na biashara, ili uchumi ufufuke. Ni Khilafah pekee juu ya Njia ya Utume ndiyo itakayo ondoa janga la deni la sekta ya kawi. Kwa kukataa maagizo ya IMF, Khilafah itajisalimisha kwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo yanaiweka sekta ya kawi chini ya umiliki wa umma, na kuzuia umiliki wa kibinafsi kabisa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu, maji, malisho na moto (nishati).” (Ahmed). Kwa hivyo, Uislamu unaweka usimamizi wa sekta ya nishati kwa serikali, ambayo itahakikisha utoaji wa umeme kwa bei ambayo haitakuwa mzigo, ikiruhusu mwamko wa haraka wa uchumi.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |