Mtoto Aliyeuawa Shahidi, Kuhesabiwa kwa Waathiriwa Kutaisha Lini? Watu wa Damu hiyo Watainuka Lini Kuwalipiza Kisasi?
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wizara ya Afya ya Palestina ilisema kwamba vikosi vya uvamizi vilifyatua risasi kwenye gari moja lililokuwa limebeba raia wa Palestina katika mji wa Hebron katika Ukingo wa Magharibi wa kusini unaokaliwa kimabavu, na kusababisha kifo cha kishahidi cha mtoto mchanga wa miezi saba Sam Abu Hikal huku akiwa mikononi mwa mamake. Mamake na babake pia walijeruhiwa.



