Jumatatu, 10 Rabi' al-awwal 1445 | 2023/09/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  25 Shawwal 1443 Na: BN/S 1443 / 16
M.  Jumatano, 25 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Uturuki na Serikali za Wasaliti wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake (saw), na Waislamu katika Usawazishaji Wao wa Mahusiano na Umbile la Kiyahudi Zinathibitisha Njama Zao na Khiyana Zao kwa Msikiti wa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa

(Imetafsiriwa)

Kwa Kusawazisha Kwao Mahusiano na Umbile la Kiyahudi, Zathibitisha Njama na Usaliti Wao wa Msikiti wa Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amefanya ziara katika umbile Kiyahudi leo siku ya Jumatano ambapo alikutana na waziri wa mambo ya nje wa umbile hilo. Pia amefanya mkutano wa pande mbili katika ngazi ya wajumbe kujadili uhusiano wa nchi hizo mbili na masuala ya kikanda na kimataifa. Na miongoni mwa aliyoyasema huko, "...tutaendelea kuratibu pamboja na upande wa Palestina hasa kuhusu usawazisha mahusiano na (Israel), na tunaunga mkono kadhia ya Palestina kwa muundo ulio tofauti na uhusiano wetu na (Tel Aviv)...".

Katika ziara yake ya kusikitisha, Davutoglu alitembelea Msikiti wa Al-Aqsa ulio mateka chini ya viziwio vya uvamizi huo, badala ya kuingia humo na jeshi la Uturuki, wajukuu wa Mauthmani na walinzi wa Al-Aqsa, wakiwa ni wakombozi na wenye kupiga takbira!

Ziara hii inajiri huku kukiwa na athari za dhulma za kila siku na kuongezeka kwa uhalifu wa umbile la Kiyahudi, na umwagaji wake wa damu ya watu wa Palestina, ile damu ambayo ingali haijakauka na ambayo Mayahudi hawatofautishi kati ya wanaume na wanawake, wala baina ya wazee na watoto. Davutoglu anakuja katika kilele cha unyanyasaji, ubomoaji wa nyumba, kukamatwa, ukiukaji wa matukufu na kuvamiwa na mwenendo wa bendera, na huo ndio mwenendo wa serikali ya Uturuki inayokwenda upande wa usawazishaji mahusiano wenye hali ya kudhalilisha, hali kama ya tawala zengine za wasaliti wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waislamu. Ziara hii ya kusikitisha inadhihirisha uhakika wa serikali ya Uturuki inayokula njama na haitofautiani katika dori yake chafu nchini Syria, ambapo kutokana nayo adui wa Mwenyezi Mungu Bashar na utawala wake wa kihalifu alimakinika... Je, Uturuki ya Erdogan imekuwa ni chombo mikononi mwa maadui wa Uislamu ambao kupitia kwayo wanatekeleza kile wasichoweza kukitekeleza kwa mikono yao wenyewe?!

Hakika sisi kutokana na ziara hii ovu tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Kuharakisha kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi kwa njia hii ya aibu kwa watawala wa Uturuki na tawala khiana chini ya kivuli cha vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na umbile la Kiyahudi, hakika ni aina miongoni mwa aina za uadui, njama na uchochezi dhidi ya Palestina, watu wake na matukufu yake, na kusubutu kwa umbile la Kiyahudi kufanya zaidi, na ni ujumbe unaoipa idhini kuendelea na uhalifu wake.

Kwa hivyo tawala hizi dhalilifu zilikimbilia katika kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi huku likiwaua kwa makusudi na kuwahamisha watu wa ardhi iliyobarikiwa, likibomoa nyumba na kuunajisi Msikiti wa Al-Aqsa kila uchao, jambo ambalo ni khiyana juu ya khiyana.

Pili: Usawazishaji huu wa kufedhehesha wa mahusiano, ikiwa unaashiria chochote, basi unaonyesha kwamba tawala hizi zimetenganishwa kikamilifu na Umma, na sio jinsi yake hata kidogo. Umma unapoona nia yake ya kuangamizwa na umbile hili, tawala hizo huona maslahi yake, usalama, biashara na uhai wake katika kuwepo kwake na uhusiano wake nalo, na hii ni kinyume kabisa na maslahi ya Umma na kile unachohitaji.

Tatu: Kujenga uhusiano kati ya Uturuki na umbile la Kiyahudi kwa msingi wa madai ya maslahi ya pamoja ina maana ya kuhifadhi maslahi hayo, yaani kulihifadhi umbile la Kiyahudi na kudumu kwake, na kulipatia njia ya uhai na kubakia. Hivyo basi, tunaziona tawala hizi za khiyana kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake zikifunganisha maslahi yao pamoja nalo na kuwepo kwao kwa kuwepo kwake, na wao hawatambui kwamba wakati huo huo wanafungamanisha kifo chao na kuangamia kwake, na kwamba kwa khiyana yao hiyo hawatapata ila ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na hasara iliyo wazi!

Nne: hakika wenye kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa wamesikia sauti yao na kupinga ziara yake ya kudhalilisha, wamemsikilizisha kwamba Msikiti wa Al-Aqsa hauwapokei vikaragosi na wadanganyifu, bali Mujahidina na wafunguzi. walimsikilizisha wito wao kwa Mujahidina katika jeshi la Uturuki kutekeleza wajibu wao kwa Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, (saw). Je, vyombo vya habari vya Uturuki vitafikisha ujumbe huu kwa Waislamu nchini Uturuki?!

Tano: Katika hatua ya kufedhehesha, Waziri Mevlutoglu aliweka shada la maua kwenye mnara wa mwenge kama heshima kwa Mayahudi waliouawa! Lakini vipi kuhusu msimamo wake juu ya mashahidi wa Kiislamu waliouawa na umbile la Kiyahudi?! Je! mashahidi hawa hawawahamashi majeshi ya Waislamu kutekeleza jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka katika mizizi yake?!

Hatimaye:

Tunachokiona katika usawazishaji mahusiano wa kufedhehesha kutoka kwa tawala zilizopo katika nchi za Waislamu, na kuusaliti Umma na kadhia zake, na kudhalilishwa mbele ya maadui zake na kuwafanya vipenzi, ni matokeo ya kimaumbile ya kuwepo kwa tawala hizo za kisekula baada ya kuvunjwa Khilafah iliyoihifadhi Palestina mithili ya kuhifadhi kiungo cha mwili. Na huku Davutoglu anayewakilisha utawala wa kisekula wa Uturuki akija Palestina akiwa dhalili chini ya mikuki ya uvamizi huo na kuusaliti na kujipendekeza kwa Umma, Waislamu nchini Uturuki na jeshi la Uturuki wanatamani izza na vyeo vya utukufu, wakitamani jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, kama vile Koplo Hasan Al-Agderli, askari wa mwisho wa kambi ya kijeshi ya Uthmani aliyefariki akiwa amesimama, akidumisha wajibu wake katika Msikiti wa Al-Aqsa, na hili linawakilisha tofauti kati ya dola bandia za kisekula na dola ya Khilafah itakayosimama hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ili kuziondoa tawala za usawazishaji mahusiano, na kuliondoa umbile dhaifu la Kiyahudi na ulimwengu kupumzika kutokana na shari zake.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ * فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ﴿           

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu* Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Maida: 51-52]

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu