Jumatano, 29 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  24 Dhu al-Hijjah 1446 Na: BN/S 1446 / 38
M.  Ijumaa, 20 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Baada ya Kuibuka kwa (Israel) Tulikabiliana na Ulimwengu wa Kiarabu Ulioungana, na Polepole Tukaugawanya”
(Imetafsiriwa)

Kwa maneno haya, Netanyahu anahutubia watu wake na ulimwengu, akijigamba kana kwamba amefanya hivyo. Kama ilivyo desturi ya watu wake, ni wachongezi, waongo na kudai wasichokuwa nacho! Kabla ya kuwepo kwa umbile la wale ambao Mwenyezi Mungu amewalaani na kabla ya kuvunjwa kwa Khilafah, “Ulimwengu wa Kiarabu” haukuunganishwa tu. Badala yake, ulikuwa ni umma mmoja chini ya dola moja. Umma huu haukugawanywa na nyinyi, bali mabwana zenu waliokubuni kwa uovu na hila. Mabwana wenu waliopigana na umma huu kwa karne nyingi, wakionja nguvu zake na kushuhudia kuanguka kwa miji yao mikuu mmoja baada ya mwingine. Konstantinopoli ilitekwa na dada yake (Roma) karibu kuanguka, lakini Mwenyezi Mungu akataka ibaki kuwa hifadhi kwa ushindi mpya ujao, Inshallah.

Mabwana zenu wa Magharibi walikuwa wakikabiliana na ulimwengu wa Kiislamu ulioungana na walijua chanzo cha nguvu zake. Kisha, wakati umma wa Kiislamu ulikuwa haujitambui na ni dhaifu, walijipenyeza katika fikra na nyoyo za watoto wake, na kuzusha fitna na kuamsha utaifa na uzalendo: huyu ni Mwarabu na yule Mturuki, huyu ni Mkurdi na yule ni Amazigh. Walinyanyua miito ya mgawanyiko juu ya dini na udugu wa Uislamu, kwa hivyo waliugawanya umma wetu na wakawa kama kisu kwenye mwili mmoja, wakizigawanya nchi kwa Mkataba wa Sykes-Picot, ambao ulizaa Azimio la Balfour.

Umma wa Kiislamu uligawanyika siku walipotutengenezea mipaka ya kundoto na bendera za mgawanyiko. Walituambia tutukuze nchi zetu na tutengeneze mipaka ya kindoto baina yetu. Kisha wakaweka manii yenu maovu ndani ya tumbo la ulaghai na uovu. Wamagharibi walikukusanyeni kutoka katika tawanyiko la ardhi, na mlikuwa duni kuliko mbwa. Kisha siku mlipozaliwa, nchi za Magharibi zilikuwa zimechukua udhibiti wa ardhi zetu na kuweka walinzi juu ya maslahi yake, watawala ambao walikuwa na mazoea ya uhaini na utiifu. Kisha ikakufanyeni kuwa kambi yake ya hali ya juu katika ardhi zetu na kisu cha mgawanyiko katika pande zetu. Kwa hivyo, mlizaliwa katika kiota cha serikali vibaraka zilizoundwa na Magharibi ambazo zilistahili umbile lenu haramu. Kwa hiyo, mgawanyiko na uwepo wenu katika ardhi zetu vilikuwa kitu kimoja.

Kisha Magharibi, kwa ushirikiano wa watawala vibaraka na PLO wasaliti (Shirika la Ukombozi wa Palestina), wakafanikiwa kuasisi umbile lenu kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na wanajaribu kulipa uhalali kupitia mikataba ya amani ya khiyana.

Hata hivyo, ijapokuwa hamkuichukua Palestina isipokuwa baada ya kugawanyika Ummah, na ijapokuwa sasa munaipiga mabomu Gaza na Lebanon, Syria na Yemen, kisha Iran, na mgawanyiko unakutumikieni, na kukosekana kwa ari na usaidizi kunaongeza nguvu na vita vyenu, na ingawa hamjishughulishi katika yote hayo isipokuwa kwa msaada, ulinzi, na silaha za wale waliokuwekeni katika ardhi hii, tunasikia pumzi za umoja katika umma, na maana za jihad sasa zinaibuka kutoka kwenye vumbi la mateso, na Umma wa Kiislamu leo ​​unatamani umoja wake, na umejua siri ya udhaifu wake na adui yake, na kinachokosekana ni juhudi zake za kuunganisha ili kuziangusha tawala vibaraka zilizougawanya, na kama vile mulivyoichukua nchi hii kwa udhaifu na mgawanyiko wake, Ummah huu utakufurusheni nyinyi na mabwana zenu kutoka humo kwa nguvu zake na umoja wake, na nyinyi si chochote ila ni vumbi linalopita lenye kupeperushwa na upepo wa umma unaokuja.

[قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَنْ يُصِيبَكُمُ اللهُ بِعَذَابٍ مِنْ عِنْدِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُمْ مُتَرَبِّصُونَ]

“Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” [At-Tawba: 52]

﴿إِنَّ اللهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً

“Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq: 3]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu