Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  3 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: HTS 1442 / 70
M.  Jumatatu, 14 Juni 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kaimu wa Kazi za Ubalozi wa Pakistan Jijini Khartoum Akataa Kukutana na Ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan chini ya uongozi wa Msemaji Rasmi Ibrahim Othman Abu Khalil, akiandamana na Ustadh Nasser Ridha Muhammad Othman - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Ustadh Suleiman Al-Dasis - Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Ustadh Abdul Qader Abdul Rahman - Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na Mhandisi Ahmed Jaafar, mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, ulitembelea Ubalozi wa Pakistan jijini Khartoum leo Jumatatu 14/06/2021 M, kwa madhumuni ya kumkabidhi balozi, au mwakilishi wake, taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa anwani: "Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan", isipokuwa kwamba kaimu huyo wa kazi za ubalozi wa Pakistan jijini Khartoum alikataa kukutana na ujumbe huo, na akakataa kupokea taarifa hiyo!

Tabia hii ya Kaimu wa kazi za Ubalozi wa Pakistan ni tabia ya kawaida kwa mtu anayewakilisha serikali yenye kuwateka nyara wenye ikhlasi miongoni mwa watoto wa Umma huu, na kuwaweka katika vyumba vya chini vya huduma za ujasusi kwa zaidi ya miaka tisa bila mashtaka, kwani ilivyo fanya kwa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, Mhandisi Naveed Butt tangu 11 Mei 2012 M, sio kwa sababu yoyote isipokuwa alikuwa mkweli, mwenye ikhlasi, na mwanafikra nadra wa kisiasa. Aliyeipenda nchi yake na aliyetaka iwe bwana na sio mtumishi mtiifu wa Amerika, yenye kuwaua watu wake katika eneo la makabila la Pakistan ili kupunguza shinikizo kwa jeshi vamizi la Amerika, na Naveed alilaumiwa waziwazi na majenerali mafisadi, na maafisa vibaraka ambao waliruhusu kuenea hatari ya ushawishi wa Amerika ndani ya vituo nyeti zaidi vya taasisi za kijeshi na serikali.

Taarifa hiyo ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir ilihutubia maafisa waaminifu na wanaojitolea wa safu zote za jeshi la Pakistan, ikisema: "Someni ayah zinazoambatana na miito yenye kuyapamba mabega yenu. Kumbukeni mafundisho ya itikadi asili ya kivita ya jeshi lenu. Angalieni usaliti unaofanywa kwa kaka na dada zenu katika maeneo ya FATA, Jammu na Kashmir. Angalia kutokuchukua hatua kwa wanaodhulumiwa nchini Myanmar, Msikiti wa Al-Aqsa na Ukanda wa Gaza.", na taarifa hiyo ilisema: "Hakika Ndugu Naveed ni mmoja wa mashababu wanaojulikana kwa kujitolea kwao kwa hukmu za Uislamu na tabia njema, mwanafikra mwaminifu, na mwanasiasa mashuhuri ... Aliwasilisha ramani ya ukweli ya utendakazi ambayo ingeleta kheri na wokovu kwa Pakistan na nchi zote za Waislamu ulimwenguni ... Ramani ya Utendakazi ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume Muhammad, (saw)... Lakini badala ya kumheshimu na kumthamini, watu mafisadi kati yenu walimteka nyara mahali kusikojulikana, La Hawla wala Quwatta illa Billah... Kwa hivyo, tunamtaka kila mmoja wenu mwenye ikhlasi kushinikiza mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru haraka kwa Ndugu Naveed kurudi kwa familia yake, ili apande minbar na kusema ukweli pamoja na ndugu zake wengine katika Hizb ut Tahrir."

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir pia ilihutubia wanachama wa ujumbe wa kidiplomasia wa Pakistan, ikisema: "Nyinyi mnawakilisha sura, sifa, historia na hivi sasa watu wa Pakistan ulimwenguni. Kupotezwa kwa nguvu kwa Naveed kunachafua sifa ya haki katika nchi yenu. Kwa hivyo tunakulinganieni mufanye sehemu yenu katika kumaliza aibu hii ambayo serikali imejiletea." Vilevile ilihutubia kila Muislamu, na kila mwandishi habari kujiunga na kampeni ya shinikizo kwa serikali ya Pakistani ikiwalingania: "Njooni mjiunge na kampeni hii kuishinikiza serikali ya Pakistan na majenerali wa jeshi lake kumwachilia huru Naveed Butt na kumunganisha tena na familia yake." Mwenyezi Mungu (swt) asema: 

وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ﴿

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu