Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: HTS 1442 / 14
M.  Alhamisi, 08 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwanamke ni Heshima Ambayo ni Lazima Ilindwe, Sio Bidhaa Hairuhusiwi kwa Mwanamke Kuchuma Pato Isipokuwa la Kazi ya Mikono Yake
(Imetafsiriwa)

Mji mkuu wa Sudan, Khartoum, alishuhudia onyesho la mitindo kwa wanawake kwa mara ya pili na mwanamitindo Nermin Qarqafi, lililohudhuriwa na kundi la vyombo vya habari, sanaa na watu maarufu wa jamii. Kwenye onyesho hilo, walimbwende wa kiume na wa kike waliwasilisha mikusanyo anuwai ya mitindo na miundo ya kushangaza, kwa ushiriki wa wanamitindo wa kiume na wa kike, na walimbwende wa kike. Mitandao ya kijamii iliripoti picha hizo kwa mapana. (Tovuti ya Niles, 6/7/2021).

Enyi Watu wa Sudan: Urasilimali na hadhara ya Kimagharibi, ambayo Serikali ya Mpito hufuata katika kila shimo la mjusi, zimejengwa juu ya thamani ya kimada, faida na hasara, na sasa serikali inaruhusu ufanyaji biashara na heshima yenu, kwa sababu wanafikra na waanzilishi wa urasilimali walikadiria kuwa bidhaa ya kiuchumi ni kila kitu kinachotakwa, licha ya hatari yake, au makadirio mengine yoyote ya vima, akhlaqi na maadili. Bidhaa kwao inakuwa sehemu ya maisha ya kiuchumi ikiwa kuna wale wanaoitaka. Mrasilimali huchukua kazi yoyote kwa ajili ya faida, iwe ni biashara ya mihadarati, ngono, watumwa, silaha, au tabia zengine ambazo zimekuwa kawaida katika jamii za kirasilimali, na isingefanikiwa bila huduma zinazotolewa na serikali. Je! Mnasubiri uhalisia huu uwepo majumbani mwenu?!

Kufuatia sheria za Magharibi kwa kutunga sheria zilizoanguka za uhuru na ukombozi, Serikali ya Mpito iliwashajiisha wanawake kufanya kazi katika taaluma ambazo uke wao unatumiwa; kukuza na kuizingatia kuwa sanaa na utamaduni, kama onyesho hili la mitindo, kucheza, kuimba, huduma katika ndege, mikahawa na maduka. Kwa haya yote na vidokezo vyengine ambavyo ni vingi sana kuvitajwa, onyesho la mitindo ni uzazi asili wa serikali hii iliyo cheshewa, na sio tabia isiyo ya kawaida kwa serikali ya kisekula inayoupiga vita Uislamu katika sheria zake. Uislamu hufanya kazi ya kuimarisha maadili, thamani ya kibinadamu na ya kiroho katika jamii na kuzufanya ziipiku thamani ya kimada ambayo ndicho kipimo cha serikali hii, ambayo haijali kulinda maisha ya kijamii na jamii ya Kiislamu kutokana na aina zote za ufuska, muozo na utumiaji mbaya.

Uislamu umewalinda wanawake, umewaheshimu, umekataza utumiaji wao mbaya, umehifadhi utakaso wao na usafi wao, na hata umewazunguka na ukuta wa vifungu ambavyo vinawahakikishia maisha ya utakaso na usafi. Uislamu kwanza kabisa umewafanya wanawake kuwa ni heshima ambayo lazima ilindwe. Uislamu pia umeharamisha kazi yoyote kwa mwanamke ambayo uke wake utatumiwa, kama vile ulimbwende. Islam Rafi 'bin Rifa'ah alisema:

«وَنَهَانَا ﷺ عَنْ كَسْبِ الْأَمَةِ إِلَّا مَا عَمِلَتْ بِيَدِهَا، وَقَالَ هَكَذَا بِأَصَابِعِهِ نَحْوَ الْخَبْزِ وَالْغَزْلِ وَالنَّفْشِ»

“... Na amekataza (saw) chumo la mwanamke isipokuwa la kazi iliyofanywa na mkono wake, na akaashiria (baadhi ya vitu) kwa vidole vyake kama kuoka mikate, kufuma na kusuka.” [Imepokewa na Ahmad].

Enyi Walezi: kwa kuzingatia hali hizi, Uislamu haukuacha hatma ya mwanamke dhaifu kugonga mawimbi ili kumchukua mahali anapotaka, akipatiliza fursa ya uhitaji wake na udhaifu. Uislamu ulisema kwamba mwanamke ana mlezi (wali) kumlinda na kumsaidia kufanya uamuzi wa busara mbali na hamu na mihemko; kumlinda na kulinda jamii kutokana na uovu na muozo. Uislamu umelazimisha kufinika za sehemu za uchi (awrah), kuharamisha mchanganyiko isipokuwa kwa hitaji lililoidhinishwa na Shariah, uharamu wa Khalwa (mwanamume na mwanamke wasio mahrim kuwa faraghani), ulazima wa kushusha macho, uharamu wa kuonyesha urembo kwa wanaume (tabarruj) na mambo mengineo, kwa hivyo je, mumesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuachana na sheria hizi?! Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itamaliza njama hizi kwa kuondoa maovu yote haya.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu