Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Muharram 1443 Na: HTS 1443 / 01
M.  Alhamisi, 26 Agosti 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

(وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 155-156]

 (Imetafsiriwa)

Kwa nyoyo zilizojaa imani na kuridhika na qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), na kwa macho yaliyojaa machozi, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan inamuomboleza yule aliyesamehewa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu:

Mubarak Al-Makki Al-Baqir

ambaye alikuwa kutoka kizazi cha kwanza, ambapo alitumia zaidi ya ujana wake kufanya kazi ya kurudisha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu; kupitia kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, akijitolea nafsi yake, wakati wake na mali yake kwa ulinganizi. Alikamatwa wakati wa enzi ya dhalimu Jaafar Al-Numeiri, na pia alikamatwa wakati wa enzi ya serikali uliopita. Kukamatwa huku hakukumzuia kubeba dawah hii na kutangaza haki hadi alipofariki mnamo Alhamisi, 18 Muharram 1443 Hijri sawia na tarehe 26/08/2021 M.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ambariki kwa rehema Yake, na amsamehe, akirimu makaazi yake, apanue kaburi lake, na aibariki familia yake na kizazi chake, na atutie moyo sisi na ndugu zake miongoni mwa wabebaji wa Da'wah, familia yake, na wapendwa wake kwa subira, na faraja bora.

Moyo unahuzunika, na macho yanabubujika machozi, na tunasikitishwa na kufarikiana nawe, na hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mola wetu:

 (إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 155-156].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu