Jumamosi, 15 Muharram 1444 | 2022/08/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  7 Jumada II 1443 Na: HTS 1443 / 16
M.  Jumatatu, 10 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe Kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan
Watoa Rambirambi kwa Kiongozi Abdul Rasoul Al-Nur
(Imetafsiriwa)

Jumamosi, tarehe 8/1/2022, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ukiongozwa na Sheikh Nassir Ridha Muhammad Othman, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, akifuatana na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, na Ust. Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, ujumbe huo ulitoa rambirambi kwa marehemu Abd al-Rasoul al-Nur, gavana wa zamani wa Kordofan, na kiongozi wa Chama cha Kitaifa cha Umma, nyumbani kwa familia huko Omdurman. Ujumbe huo ulikutana na viongozi wa Chama cha Umma, watoto wa marehemu na familia yake.

Mwenda zake alikuwa na maingiliano mazuri na Hizb ut Tahrir, na aliitikia mialiko ya hizb, hafla na vikao, na kushiriki katika hafla mbalimbali za Mashababu.

Marehemu aliendelea kuwasiliana na viongozi wa hizb, akiamiliana nao kwa kuheshimiana, kuwasikiliza na kukubali ushauri. Siku moja katika mwaka wa 2019, baada ya kujibu mwaliko wa Iftar ya Ramadhan ilioandaliwa na hizb, aliandika maneno mazuri kuhusu hizb na wafanyakazi wake, yaliyoandikwa kwa herufi za dhahabu.

Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe na umrehemu, na umuweke katika bustani zako pana, na yakirimu makaazi yake, na upanue maingio yake, na umuoshe kwa maji, theluji na mvua ya mawe, na umtakase na madhambi kama nguo nyeupe inavyotakaswa na uchafu na umkubali pamoja nawe, Ewe Mola Mlezi wa walimwengu wote. Tunarudia kutoa rambirambi zetu kwa familia yake, ndugu na wapendwa wake.

 [إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea [Surah Al-Baqarah: 156]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu