Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  16 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 07 / 1443
M.  Ijumaa, 15 Julai 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwanahabari Aunga Bogi la Khiyana na Usawazishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Mwanahabari wa umbile la Kiyahudi, Roi Kais alimkaribisha mwandishi wa habari Suhair Abdel Rahim, mhariri mkuu wa tovuti ya Sawt As-Sudan, katika kipindi kilichopeperushwa kwenye idhaa moja ya Kiebrania. Mwandishi huyo wa habari, Kais, alizungumzia suala la "msichana (wa kituo cha basi) ambaye alikwenda kwenye barabara ya umma na kutaka kuolewa. Roi alimuuliza mwandishi wa habari Suhair Abdel Rahim kuhusu maoni yake juu ya suala hilo, hadhi ya wanawake wa Sudan katika jamii ya Sudan, na kiwango ambacho walipata haki zao. (tovuti ya Zarqa, 15/7/2022 imehaririwa)

Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunataka kueleza yafuatayo:

Kwanza: Mwandishi huyu wa habari ameunga bogi la usawazishaji mahusiano wa vyombo vya habari na umbile la Kiyahudi, mnyakuzi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Masra (mahali pa Isra) ya Mtume (saw), na mkiukaji wa matukufu ya watu wa Palestina, wanaume na wanawake wao. Alipanda treni ya usaliti pamoja na vibaraka wa makafiri: wanasiasa, wanahabari na wengineo walioitukuza batili ya usawazishaji mahusiano, ambayo si chochote ila ni usawazishaji mahusiano wa watawala wanyenyekevu, ambao Umma wa Kiislamu ulijitenga nao, na unaomba kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ataujaalia ushindi na tamkini, ili wale waliodhulumu wajue hatima yao.

Pili: Usawazishaji mahusiano wa vyombo vya habari vilivyolipwa kwa bei duni usingetokea lau isingelikuwa usawazishaji rasmi wa mahusiano katika wakati ambapo watawala Ruwaybidha (wajinga) walikataa kufuata njia ya Mtume (saw) katika kukabiliana na dola ya Kiyahudi, inayochafua Masra Tukufu (mahali pa Isra), kuuwa wanawake, kufunga jela, kupora, na kuvunja heshima ya watu wetu huko Palestina mchana na usiku. Yote ni kutokana na kutokuwepo kwa mamlaka (sultan) ya Uislamu, Khilafah.

Tatu: Dola ya Kiyahudi inatafuta mikono miovu ili kuisaidia kufichua ukiukaji unaofanyika katika jamii yetu unaotokana na utekeleza wa mifumo ya kikafiri kwa watu. Haya yote ni sehemu ya kazi iliyopangwa ya kumchafua mwanamke wa Kiislamu, ambaye ndiye msingi wa muundo wa jamii.

Enyi Wanawake wa Sudan, viumbe viovu zaidi, Mayahudi, wamechagua kutuelekezea mishale yao yenye sumu kwa sababu wanatambua umuhimu na hatari ya dori yetu katika uhai na usafi wa Uislamu. Kwa hiyo, muonyesheni Mwenyezi Mungu (swt) kheri ilioko ndani yenu, kabilianeni na mashambulizi makali ya Magharibi kafiri na wafuasi wake, kwa kushikamana na Shariah ya Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo njia ya kuokoka kutokana na janga hili. Na pazeni sauti zenu juu kutangaza kwamba hamkubali kwamba tarumbeta hizi zinazovuma zipotoshe rai jumla kwamba zinawakilisha wanawake watukufu wa Kiislamu.

Enyi Waislamu: Wale wanaotekeleza usawazishaji mahusiano rasmi na wa vyombo vya habari wanajaribu kukamilisha njama za Mayahudi katika kufanya mikataba na umbile hili la Kiyahudi kuwa ni jambo la kimaumbile, ambao ni udanganyifu wa wahalifu watakaowajibishwa na Dola ya Kiislamu; Khilafah kwa yale wanayostahiki. Tuna imani na ahadi njema ya Mwenyezi Mungu (swt) na kauli yake:

 [وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ * فَلاَ تَحْسَبَنَّ اللهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ إِنَّ اللهَ عَزِيزٌ ذُو انتِقَام]

“Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima * Basi usimdhanie Mwenyezi Mungu kuwa ni mwenye kuwavunjia ahadi yake Mitume wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, na ni Mwenye kulipiza.” [Ibrahim: 46-47].

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake
cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu