Jumatatu, 12 Jumada al-awwal 1444 | 2022/12/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  27 Safar 1444 Na: HTS 1444 / 07
M.  Ijumaa, 23 Septemba 2022

 Habari kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Sheikh Al-Sajjadah Al-Qadiriyah Al-Arkia huko Taiba
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan kwa uongozi wa Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, akifuatana na Ust. Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Abdul Qadir Abdul Rahman, mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Al-Nazir Mukhtar, Shariq Yusef Al-Barbari, Ahmed Bahr, Rahmah Al-Mawla Hajj, na Adam Omar, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelee Sheikh Al-Reeh Ibn Sheikh Abdullah katika ngome yake huko Taybeh Sheikh Abdul Baqi kisiwani, mnamo Jumatano, 21/9/2022. Mkutano huo ulizungumzia hali ya kisiasa nchini, hali ya kuzorota na mizozo, na mgongano wa mipango iliyowasilishwa na vyama na kukataliwa na wengine, chini ya ushawishi wa balozi za kigeni, inafichua hali ya mizozo kati ya vyama vya siasa, raia na jeshi, ambayo inachochewa na balozi za Amerika, Uingereza, Saudi Arabia na Imarati, na kwamba kila kitu kinachofanyika hakiwakilishi masuala ya wananchi.

Suluhu ni kwa watu wa nchi hii kukusanyika kwa msingi wa itikadi yao ya Kiislamu, na kwamba Uislamu pekee ndio unaowaunganisha watu wa Sudan na wenye utatuzi madhubuti wa masuala na matatizo yote. Mfumo wa Kiislamu unawakilishwa ndani ya Khilafah, na changamoto inayoukabili mradi wa kikoloni unaoongozwa na balozi hizo nchini ni kuanzishwa kwa Khilafah. Mwishoni mwa mkutano huo, Sheikh Al-Reeh aliushukuru ujumbe wa Hizb ut Tahrir kwa ziara hii, mazungumzo haya adhimu yaliyobeba hamu ya watu wa Sudan. Akasema: Tumesikia maneno mazuri, na akasisitiza kuwa wao ni kama zulia lenye masuala ya wananchi na kwamba utatuzi wao uwe kwa mujibu wa Kitabu na Sunnah. Alhamdulilah Rabil Alamin, ulikuwa ni mkutano mzuri, na watu wa Sujada walikutana na ujumbe wa Hizb ut Tahrir kwa dhati, shukrani na heshima, Mwenyezi Mungu awalipe kheri.

Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano alimkabidhi Sheikh Al-Reeh rasimu ya katiba ya Dola ya Kiislamu, kitabu, Ukanushaji Fikra ya Kirasilimali ya Kimagharibi, na masuala kadhaa kutoka Gazeti la Ar-Raya.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu