Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  20 Rabi' I 1444 Na: HTS 1444 / 09
M.  Jumapili, 16 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hotuba ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari Kwa Jumuiya ya Ikhwan ul-Muslimin na Mashirika Yanayofanya Kazi katika Masuala ya Palestina
(Imetafsiriwa)

Suala la kuiregesha Palestina mikononi mwa Umma wa Kiislamu, na kuitakasa na najisi ya Mayahudi, ni suala la Waislamu wote. Sio suala la watu wa Palestina peke yao, kwani ufuska wa Mayahudi unataka iwe hivyo, na mbele yake wapo watawala wa Magharibi koloni ya Kikafiri, na nyuma yao wako watawala wa dola zenye madhara katika nchi za Waislamu. Msikiti wa Al-Aqsa ndio kibla cha kwanza ambacho Waislamu walikuwa wakiswali kuelekea, na ni safari ya Mtume kipenzi, rehma na amani zimshukie, na kabla ya hapo na baada ya hapo ni ardhi ambayo Mwenyezi Mungu ameibariki. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

(سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ)

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Israa: 1].

Bait Al-Maqdis ilikuwa ni ya kwanza kufunguliwa na Waislamu, ambapo aliyepokea ufunguo wa Mji Mtakatifu, ni Khalifah ar-Rashid (Khalifah Muongofu) wa pili Al-Faruq Omar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, na kuandika mkataba unaojulikana kama Mkataba wa Omar, ambao miongoni mwa vifungu vyake: "Kwamba Mayahudi wasiishi katika Nchi Takatifu."

Katika kipindi chote cha utawala wao, Waislamu walibakia kuwa ni wahifadhi wa Al-Aqsa na msikiti wake hadi dola ya Bani Abbas ilipodhoofika, hivyo Makruseda wakaikalia kwa mabavu Jerusalem kwa zaidi ya miaka thamanini, ambapo Waislamu hawakuiacha Palestina na Al-Aqsa mpaka Mwenyezi Mungu alipopitisha Salah al-Din al-Ayyubi, na akaikomboa Jerusalem kutoka kwa Makruseda, na akawaunganisha Waislamu na jeshi lao, na akapata ushindi siku ya Ijumaa, tarehe ishirini na saba Rajab al-Khair mwaka 583 H.

Kisha Khilafah ya Kiuthmani ikaihifadhi Palestina hata katika hali yake dhaifu zaidi, huku Mayahudi wakijaribu kumrubuni Sultan Abdul Hamid II kwa pesa kwa badali ya kuwaruhusu Mayahudi kuhamia humo. Yeye Mwenyezi Mungu amrehemu, alikataa matakwa ya Mayahudi yaliyofanywa na Myahudi Mzayuni Herzl, akisema: “Mpe ushauri Dk. Herzl asichukue hatua zozote zaidi katika mradi wake. Siwezi kutoa hata shubiri moja ya ardhi hii hata kidogo kwa kuwa sio yangu, ni ya Umma mzima wa Kiislamu uliopigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao. Mayahudi wanaweza kubakia na mamilioni yao. Iwapo Khilafah ya Kiislamu itavunjwa siku moja basi wataweza kuichukua Palestina bila ya thamani yoyote. Lakini nikiwa hai, ni afadhali kuzamisha upanga ndani ya mwili wangu kuliko kuiona ardhi ya Palestina ikikatwa na kupeanwa kutoka kwa Dola ya Kiislamu. Hii haitakuwa. Sitaanza kuikata miili yetu tukiwa bado hai”

Na alikuwa sahihi, rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwani Palestina ilichukuliwa bila ya thamani yoyote baada ya Dola ya Khilafah kuvunjwa na ardhi za Waislamu kuchanwa vipande vipande na kukaliwa kimabavu na Makafiri wakoloni. Kisha wakavipa vipande hivi kile kinachoitwa uhuru, na kwa hivyo wakaunda vijidola vidogo vya utendakazi vinavyo tumikia maslahi yao, na kutekeleza njama zao dhidi ya Waislamu kupitia walinzi, ambao waliwaunda kwa jicho la utambuzi. Wakawakabidhi utawala, na wakauongoza Ummah katika njia ya upotevu, hivyo wakaligeuza suala la Palestina kutoka kuwa ni suala la Kiislamu hadi kuwa ni suala la Waarabu, wakidai mapambano ya kirongo dhidi ya umbile la Kiyahudi, na hali kiasili wao walikuwa ni walinzi wa Mayahudi kutokana na bunduki za waumini kuwafikia. Na watawala hawa wangali wanalidogosha suala hilo mpaka wakalifanya kuwa ni suala la Palestina ambalo kwalo Waislamu na Waarabu haliwahusu. Kisha wakatembea kuelekea kuhalalisha hadharani mahusiano na umbile hili la kikatili, baada ya kuhalalisha mahusiano hayo kwa siri.

Na wakati mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina yanazidi siku hizi, mauaji, unyanyaji na uzingiraji, na wakati makundi ya walowezi yanafanya uharibifu na mashambulizi kwa watu, na uvamizi wao ndani ya Al-Aqsa kuongezeka kwa nguvu, ufidhuli, na kasumba ya uyahudi, na wakati watu wa Palestina na watoto wao wanakabiliana na umbile la Kiyahudi kwa uthabiti wote, ushujaa, kusubutu na ujasiri. Makundi yanakusanyika nchini Algeria chini ya mwamvuli wa serikali ya Algeria kutia saini makubaliano mapya ya maridhiano chini ya jina la Tangazo la Algiers, ambalo si lolote bali ni muendelezo wa usimamizi wa kipuuzi na mtazamo mbovu ambao umepelekea suala la Palestina kupata hasara na kuzorota. Ni usaliti kuweka kadhia zetu mikononi mwa maadui zetu katika kile kinachoitwa jumuiya ya kimataifa, ambayo hapo awali ndiyo iliyoanzisha unyama huu, na bado inalipatia njia ya maisha.

Enyi Waislamu: Jinai za umbile la Kiyahudi hazikomi na watawala wa Waislamu wanashiriki katika jinai zake, na ushabiki wao wa vyombo vya habari hautailinda damu ya ndugu zetu wa Palestina wanaouawa kinyama asubuhi na jioni na jeshi la Kiyahudi la ukandamizaji.

Njia ya Palestina imeegemezwa juu ya msingi wa Uislamu, na ukombozi wake ni jukumu la Umma wa Kiislamu na majeshi yake. Ndiyo maana tunaelekeza ombi letu kwa Umma bora katika sehemu zote za dunia, na kwa majeshi yake, kwa watoto wetu katika majeshi miongoni mwa maafisa na wanajeshi. Kwani katika historia yote, Bait Al-Maqdis imekuwa ni suala linaloleta pamoja Ummah wa Kiislamu uliotawanyika, hivyo inakusanya nguvu zake. Inaushinda udhaifu wake na kumshinda adui yake. Kwenye ardhi yake, Makruseda walishindwa, na Mamongoli wakashindwa.

Umma wa Kiislamu ​​unao uwezo leo wa kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, na udhaifu uliousibu leo si chochote ila ni udhaifu wa muda unaosababishwa na usaliti wa watawala wa dola zenye madhara ambao wako makini kuuonyesha kwa namna ya udhaifu.

Hivyo enyi majeshi ya Kiislamu, kwa jina la Ummah wa Kiislamu, tunatafuta nusra yenu na kukuhutubieni kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah:38]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

(وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيّاً وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيراً)

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa: 75].

Na kwamba munao uwezo wa kulifanya umbile la Kiyahudi kuwa ni taathira baada ya kivutio, na kuwatawanya walio nyuma yake miongoni mwa dola za kikoloni, na hili linawahitaji muvunje viti vya utawala vya madhalimu kutoka kwa watawala wazembe, na muwape msaada wafanyikazi wa kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo kwayo nchi za Waislamu na majeshi ya Waislamu yataunganishwa. Ili kucheza dori yake katika kuitakasa Ardhi Tukufu kutokana na najisi ya Mayahudi na wengineo, Mtume wetu Rehema na Amani zimshukie ametoa bishara njema kwamba tutawashinda Mayahudi, lakini hatutawashinda kama Waarabu au Wapalestina, bali tutawashinda kama Waislamu, na hilo litatokea tu ikiwa tutaungana ndani ya chombo kimoja; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, Mtume (saw) amesema katika Hadith iliyopokewa na Imam Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ، فَيَقْتُلُهُمْ الْمُسْلِمُونَ، حَتَّى يَخْتَبِئَ الْيَهُودِيُّ مِنْ وَرَاءِ الْحَجَرِ وَالشَّجَرِ، فَيَقُولُ الْحَجَرُ أَوْ الشَّجَرُ: يَا مُسْلِمُ يَا عَبْدَ اللَّهِ، هَذَا يَهُودِيٌّ خَلْفِي فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ، إِلَّا الْغَرْقَدَ فَإِنَّهُ مِنْ شَجَرِ الْيَهُودِ»

Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawauwa Mayahudi hadi Yahudi atajificha nyuma ya jiwe na mti, kisha jiwe au mti huo utasema: ‘Ewe Muislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, Yahudi huyu hapa nyuma yangu basi njoo umuue; isipokuwa mti wa Gharqad, kwani huo ni katika miti ya Mayahudi.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu