Jumatatu, 11 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  10 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 12
M.  Jumamosi, 18 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Walinzi wa Kike wa Demokrasia Hawawakilishi Wanawake wa Sudan ambao Wanaikufuru Demokrasia
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, 15/5/2024, mjumbe wa Marekani nchini Sudan, Perriello, alitembelea makao makuu ya Alharisat (Shirika la Walinzi wa Kike wa Mapinduzi) jijini Kampala, ambako alifanya mashauriano ili kujifunza kuhusu maoni ya kuweka amani nchini Sudan. Alikutana na wanaharakati wanawake wa Sudan nchini Uganda na kujadiliana nao kuhusu juhudi za kumaliza vita na ukiukaji unaoathiri wanawake. Alikiri uzembe wa jumuiya ya kimataifa kuhusu ukiukaji wa kibinadamu uliowaathiri, na kuwapa wanawake walioathirika msaada unaohitajika. Alitoa wito kwa umuhimu wa kupaza sauti za wanawake kwa sauti ili kusitisha vita na kufikia amani. Amesisitiza kuwa, nishati iliyoonyeshwa na wanawake wa Sudan katika Mapinduzi matukufu ya Disemba imesalia kuwa msukumo kwake na kwa wale wote walio na hamu na masuala ya Sudan, na wanawake wanapaswa kuendelea kufanya hivyo kwa mkabala huo huo wa kuregesha njia ya kidemokrasia.

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, kuhusiana na mkutano huu wa kutiliwa shaka ambapo wanawake hawa waliodanganywa walishirikiana na mjumbe huyu, Perriello, na demokrasia yake ambayo imeleta mateso yote wanayopitia wanawake, tunafafanua yafuatayo:

Kile ambacho wanawake nchini Sudan wanafanyiwa ni kwa sababu tu ya demokrasia, ambayo, mara tu inapotua katika nchi, huanzisha ndani yake nyumba ya mazishi ya maombolezi na vilio. Katika demokrasia ya kwanza, ya pili, na ya tatu ... nk, hata kama itafikia serikali za kidemokrasia bilioni moja, wanawake wa Sudan ndio waathirika. Umaskini uliokithiri na njaa ni matunda ya demokrasia ya kwanza.

Ama ya pili, iliongezeka kwa kuwashwa kwa migogoro ya kikabila iliyochochewa na Marekani na Ulaya, na kisha matokeo ya mwisho yalikuwa ni vita hivi vya kipuuzi ambavyo viliwakishwa na Marekani, ili kulipa kisasi chake kwa Ulaya, ambayo vibaraka wake kutoka kwa Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko waliingia mamlakani ndani ya serikali uliyotapakaa damu za waliouawa katika utawanyaji kikao! Je, mjumbe wa Marekani anazungumzia suluhisho gani, litakaloleta tiba wakati Marekani ndiyo iliyoleta ugonjwa huo?!

Ama kukiri uzembe wa jumuiya ya kimataifa, ni neno la ukweli tu lenye nia ya kufikia uwongo. Uzembe huo ni wa makusudi. Wanawake wa Sudan hawana tofauti na wanawake wa Ash-Sham, Iraq na Afghanistan waliotangulia kabla yao. Sasa wanawake wa Gaza wamesimama wima licha ya kupoteza wanaume na watoto. Kwa Mwenyezi Mungu tunamshtakia, sio kwa wale wanaopanga mateso, kisha kuja kulia kwa machozi ya mamba ambayo yanawadanganya tu wanaharakati wa aina hiyo, ambao akili zao zimechafuliwa na janga la zama hizi; Demokrasia, bila ya kuelewa maana yake!

Badala ya kufichua hatari ya Marekani na mjumbe wake, shirika hili lilifanya maonyesho ambayo walionyesha hadithi za ubakaji na mateso. Hivi ndivyo Marekani na mjumbe wake wanahitaji, kwa sababu ni watu ambao wanaishi tu kutokana na mateso ya watu.

Ama kuhusu ahadi za uwongo za misaada na kumalizika kwa vita, si chochote ila ni chambo kwa walinzi wa kike wa kile kinachoitwa maadili ya kidemokrasia, ambayo yamefichuliwa.

Ni wakati wa ukweli sasa mbele ya macho ya ulimwengu wote. Marekani na maadili yake ya kidemokrasia ni adui wa binadamu. Hebu na tukatae maadili yote ya Ubepari wa Magharibi kama wanawake wa Kiislamu, na tushikamane imara na maadili ya rehema na amani, maadili safi na thabiti ya Uislamu ambayo yataleta furaha kwa watu wanaoteseka kwenye sayari ya Dunia, kwa kujitahidi kwa dhati kuregesha dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo kweli itatukomboa kutokana na sababu za vita na uharibifu zilizoachwa na urasilimali.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu