Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  13 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: HTS 1445 / 45
M.  Jumanne, 21 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Dola za Sykes-Picot Zimetuletea Udhalilifu Ulioje?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumatatu, serikali ya Sudan ilituhumu Vuguvugu la Ukombozi wa Raia wa Sudan (SPLM-N) - mrengo wa Abdelaziz al-Hilu, kwa kusababisha kuporomoka kwa mazungumzo ya kuwezesha misaada ya kibinadamu kwa wale walioathirika katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile. Tuhma hizo zilitolewa na Waziri wa Ulinzi na mkuu wa ujumbe wa serikali, Luteni Jenerali Yassin Ibrahim, kufuatia wajumbe hao kuregea kutoka mji wa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, uliokuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo. Waziri wa Ulinzi alisema "vuguvugu hilo liliwasilisha pendekezo ambalo linakinzana na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu heshima ya ubwana wa nchi, ambapo ilionyesha uwezekano wa kila upande kusaini makubaliano ya upande mmoja na Umoja wa Mataifa na cheti cha upatanishi.” (Habari za Atheer).

Sheria halali ya kukabiliana na uasi ni wale waliobeba silaha dhidi ya dola, wakidai malalamiko, au sababu, na wakachukua upande mahali fulani, na lazima wakabiliwe na kuondolewa, na kabla ya kupigana nao, dola inazungumza nao, na kuona yale waliyonayo, na kuwataka warudi kwenye utiifu, na kuacha kubeba silaha. Iwapo wataitikia na kurudi, itawaacha, na ikiwa watakataa kurudi na kung’ang’ania kutoka, itapigana nao kwa njia ya kinidhamu, mpaka waregee kwenye utiifu, na kuweka chini silaha zao. Yote haya lazima yafanywe bila uingiliaji wa nje.

Kwa hiyo, kushughulikia suala la uasi dhidi ya serikali, pasi na utawala halali, ni dhambi, uasi, na huleta maovu yote, na fedheha, kwani vijidola vya Sykes-Picot vimekuwa na mazoea ya kuingia katika mazungumzo, na kutoa maafikiano baada ya maafikiano. Waasi vibaraka, ambao wana silaha na kufadhiliwa na mikono ya kigeni huamiliana na serikali kwa kiburi kikubwa, na kupeleka manufaa mingi kwa mabwana zao. Ni usaliti ulioje kuitenga Sudan Kusini mbali nasi! Katika muktadha huu, linakuja ombi la muasi al-Hilu kwa serikali, kwamba kila upande utie saini makubaliano na Umoja wa Mataifa, yenye kuiita harakati yake ya uasi kuwa ni dola sawa na dola ya Sudan!!

Asingesubutu hivi lau tungeshuka kwenye hukmu ya Sharia.

Lakini hukmu ya Sharia ni sehemu ya mfumo jumuishi wa hukmu, ambazo zote lazima zitabikishwe kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo ndipo tutaregesha maisha yetu katika Uislamu, na tutazivua nguo za udhalilifu, na tutaregea kuwa mabwana wa dunia kama tulivyokuwa tulipokuwa na Khilafah.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu