Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  14 Safar 1446 Na: 1446 / 02
M.  Jumatatu, 19 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mashirika ya Haki za Kibinadamu na Waungaji mkono wao Yanasalia kimya katika Kesi Kama Zetu
(Imetafsiriwa)

Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Mashad linafichua kuwa zaidi ya wanawake 21 wakiwemo wasichana walio chini ya umri wa miaka 18 wamebakwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Sennar na wanachama wa Kikosi cha Msaada wa Haraka. Mashad linatoa wito kwa mashirika ya kimataifa na ya kikanda ya kutetea haki za binadamu kuchukua hatua za haraka kuwalinda wanawake wa Sudan na kupunguza hatari zinazowakabili raia. Shirika hilo pia linahimiza mashirika ya kibinadamu kuendelea na juhudi zao za kukidhi mahitaji ya kimsingi ya wale walioathiriwa na vita katika Jimbo la Sennar. (Al Jazeera - Sudan, Agosti 19, 2024)

La kusikitisha, baadhi ya wanachama wa Umma wa Kiislamu bado wanaweka matumaini yao kwa walaghai waliotufikisha katika hali hii, wakiomba msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika yake, ambayo si wengine bali ni Marekani na Ulaya ile ile ambazo zinashindania rasilimali za Sudan na ambazo matendo yao yamechochea vita hivi vya kikatili. Hii ima ni kutokana na ujinga au kukata tamaa, na kuwapelekea kughafilika na masuala ya Ummah. Badala ya kufuata malengo yao wenyewe, wamejihusisha na mashirika na taasisi za kimataifa zinazoshikamana na sheria zao zile zinazoitwa za kidemokrasia (za kinyama), ambazo zinatanguliza watu kulingana na utaifa na utambulisho wao, kama ilivyoonyeshwa na vita vya Ukraine. Pindi vita hivyo vilipozuka, mashirika yaliharakisha kutoa misaada ya kweli na yenye ufanisi kwa wanawake na watoto, kuwatetea kwa kutuma silaha kwa serikali ya Kyiv na kutoa msaada mkubwa wa kifedha, kwenda mbele zaidi ya kulaani tu.

Hata hivyo, linapokuja suala la wanawake wa Kiislamu, wale wanaojiita Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa daima wanajifunga tu na shutma zisizo na maana bila kuchukua hatua yoyote ya kivitendo. Iwapo watachukua hatua yoyote, ni kutumikia tu maslahi yao machafu ya kikoloni, kuendelea kuutiisha Umma wa Kiislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[إِنْ يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُمْ بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ]

“Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.” [Surat Al-Mumtahina:2].

Umoja wa Mataifa, nchi za kidemokrasia za Magharibi, vyombo vya habari vya kimataifa, na mashirika ya haki za binadamu yamechagua kwa aibu kupuuza mauaji na dhulma zinaozidi kufanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Badala yake, wamechagua kulinda na kufuatilia maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa kwa kuendelea kuzipa pande zote mbili msaada na silaha kupitia mawakala wao wa kikanda, na hivyo kufichua unafiki wa kaulimbiu zao tupu za kidemokrasia kuhusu haki za binadamu!

Kwa vikosi nyoofu vya majeshi: Tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيّاً وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيراً]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako” [Surat An-Nisa:75].

Kwa hivyo mnawezaje kuijua aya hii na bado mnawaacha dada zenu kwenye uhalifu wa RSF?

Udanganyifu wa mataifa ya Magharibi ya kibepari, Umoja wao wa Mataifa, na jumuiya yao ya kimataifa, pamoja na mikataba wanayoweka juu yetu kuhusu haki za wanawake na haki za binadamu, pamoja na maamuzi yao, mapendekezo, na ufumbuzi wa sumu ambao umejificha kama shauri la wale waliomwaga machozi ya mamba kwa ajili yetu, si chochote ila ni njama mbaya ambayo kwayo hatujavuna chochote ila udanganyifu, kwani yote ni uhadaifu. Wokovu wetu upo mikononi mwa wanajeshi wanyoofu, sio mikononi mwa maadui zetu wanaotuvizia, ima wanatangaza wazi uadui wao au kwa unafiki kuvaa vazi la ubinadamu. Kuunganisha sababu zetu na maadui zetu ni kujiua kisiasa, hatari kubwa kwa taifa letu, na mwaliko wa kukiuka ardhi za Waislamu.

Bado kuna fursa ya kuwageukia wapangaji njama wote na wapambe wao kupitia suluhisho la haraka na la kivitendo ili kuzuia kuvunjiwa heshima kwa wanawake hao na wengine katika ardhi zote za Waislamu, ambapo mvutano wa kibepari wa kutafuta rasilimali umezigeuza ardhi hizi kuwa uwanja wa unyanyasaji dhidi ya wanyonge. Suluhisho hili ni kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaregesha heshima na adhama ya Waislamu kwa kuzuia ukoloni ambao umezua mifarakano na vita baina ya wana wa Ummah. Hii ndiyo njia pekee ya kuwaokoa wanawake wanaodhulumiwa na kuwalinda dhidi ya uhalifu wa Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu