Jumatatu, 17 Safar 1447 | 2025/08/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  10 Safar 1447 Na: HTS 1447 / 13
M.  Jumatatu, 04 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahusiano ya Kigeni ni Jukumu la Dola Pekee, kwa kuwa Dola Pekee ndiyo iliyo na Haki ya Kuchunga Mambo ya Ummah Kivitendo
(Imetafsiriwa)

Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa wajumbe kutoka Muungano wa Vyama na Mavuguvugu ya Sudan Mashariki, wakiongozwa na Sheiba Dirar na kuandamana na kundi la watu mashuhuri, walikutana na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mnamo Jumamosi, 2 Agosti 2025, afisini kwake huko Adi Halo, ambapo wajumbe hao walijadiliana naye hali ya sasa ya Sudan kwa jumla, kwa kuzingatia changamoto zinazoikabili Sudan Mashariki. Ujumbe huo pia ulisisitiza umuhimu wa uratibu na nchi jirani ili kusaidia utulivu wa nchi na kukabiliana na migogoro ya kisiasa na usalama.

Je, udhaifu na udhalilifu wa serikali ya Sudan umefikia kiwango hiki? Au inajaribu kuwalazimisha watu wakubali picha hizi potofu kwa nia mbaya? Miongoni mwa picha hizi ni mafunzo ya wanamgambo wenye itiifu wa kikanda au kikabila nchini Eritrea!

Machafuko haya, yanayofadhiliwa kisiasa na kijeshi na serikali ya Sudan – ikiwemo kuinua simulizi ya kibaguzi katika duara za kisiasa – yote yanatumikia mpango wa Amerika wa kuigawanya Sudan katika dola kadhaa: kwanza Darfur, kisha Sudan ya Mashariki!!

Serikali ya Sudan lazima itie fahamu zake na kukomesha uchokozi huu, ambao utamaliza kile kilichosalia katika umoja wa nchi hii, na kuiacha umeangamizwa na kufutwa kabisa. Huo ni usaliti mkubwa! Komesheni vitendo hivi vya kisiasa vinavyolenga umoja wa nchi hii! Komesheni msururu unaoendelea wa kuunda wanamgambo wa ndani au wale wanaohusishwa na nchi za nje kwa mafunzo!

Ama kuhusu suala la raia wa Dola ya Kiislamu – kinachotakiwa kwao na kinachostahiki kwao – na uhusiano wao na dola za kigeni, ni jambo linalosimamiwa na Shariah. Uislamu una msimamo wa wazi juu ya hili: Hairuhusiwi kwa raia kutekeleza mujukumu ya mtawala, si ndani wala nje, isipokuwa kwa uteuzi wa halali, kama vile kuteuliwa kwa Khalifa wa Waislamu, kwa sababu yeye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mambo ya ndani na nje. Mtume (saw) amesema: «...فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake…” Au wale ambao Khalifa anawateuwa, kama wasaidizi, magavana na wengineo.

Wakati dola ya Khilafah Rashida itakaposimamishwa hivi karibuni, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, hakuna mtu atakayeruhusiwa kukutana na wakuu wa nchi za kigeni au kuwa na uhusiano wowote na nchi ya kigeni. Imeelezwa katika Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah iliyowasilishwa na Hizb ut Tahrir kwa Ummah, Ibara ya 182: “Hairuhusiwi kwa mtu binafsi, chama, kambi au kikundi chochote kuwa na uhusiano wa aina yoyote na nchi yoyote ya kigeni kwa vyovyote vile. Mahusiano na nchi za kigeni ni jukumu la dola pekee, kwani ndiyo pekee inayoshikilia mamlaka ya kivitendo kuchunga mambo ya Umma. Umma na kambi za kisiasa zina haki ya kuihisabu dola kuhusiana na mahusiano haya ya kigeni.”

Enyi watu wa Sudan, je, kile tunachokuitieni sio bora kuliko uhalisia huu mbaya ambao mnaishi ndani yake? Je, haujafika wakati wa nyinyi kufanya kazi na Hizb ut Tahrir—kiongozi asiyewadanganya watu wake—kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume? Hiyo peke yake ndiyo itahifadhi umbo la serikali na kuipa hadhi. Haitaruhusu nchi yoyote ya kigeni kuingilia mambo yake au kufungua njia za mawasiliano na raia wake. Yote haya ni uhalifu mkubwa na hatari kwa uwepo wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu