Jumatano, 18 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 27
M.  Jumapili, 07 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ndani ya Muundo wa Kampeni ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Kuvuruga Mpango wa Kutenganisha Darfur
Wanachama wa Hizb ut Tahrir katika Mji wa Al-Obeid Wahutubia Wito Mzito kwa Waislamu katika Msikiti Mkuu wa Al-Obeid na Kubeba Mabango katika Amali Nyengine katika Kituo cha Usafiri
(Imetafsiriwa)

Katika amali mbili tofauti, Mashababu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Obeid, mnamo Jumamosi tarehe 06/09/2025, na ndani ya muundo wa kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ya kuvuruga mpango wa kuichana Sudan kwa kutenganisha Darfur, na kwa kuzingatia kwamba umoja wa Umma ni suala nyeti ambalo kwalo kipimo ni uha na kifo, mashababu hao wa Hizb ut Tahrir mjini Al-Obeid, katika amali ya kwanza, walihutubia wito wa mzito kwa Waislamu katika nyadhifa zao mbalimbali: wanasiasa, wanahabari, wanazuoni, maafisa na wanajeshi, wakiwataka kutekeleza wajibu wao wa Kisharia kwa kuzuia kujitenga kwa Darfur. Hii ilikuwa katika Msikiti Mkuu wa Al-Obeid, na wito huo ulisomwa na Ustadh al-Nadir Muhammad Hussein, mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan. Waliohudhuria waliingiliana na wito huo kwa namna ambayo ilithibitisha mapenzi ya Ummah huu kwa Uislamu na wabebaji da‘wah wake.

Ama kuhusu amali ya pili, mashababu wa Hizb walifanya kisimamo mbele ya skrini kwenye kituo cha mabasi katikati ya soko, na kubeba mabango ya kuwataka watu wafanye kazi ili kuvuruga mpango wa Marekani unaolenga kuichana Sudan kwa kuitenga Darfur. Wapita njia walifanya maingiliano kwa maoni chanya na kwa kupiga picha, jambo ambalo lilimkera mmoja wa askari polisi, ambaye alitaka kutawanyika kwa kisimamo hicho, baada ya kuwa tayari kimetimiza lengo lake.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu