Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 2 Rabi' II 1447 | Na: 1447 / 03 |
M. Jumatano, 24 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maradhi ya Mkurupuko Yawaangamiza Watu kwa Kukosekana kwa Dola ya Ustawi
(Imetafsiriwa)
Maradhi matatu ya kimazingira—kipindupindu, homa ya dengue, na malaria—yanawaangamiza watu katika majimbo ya Khartoum, Al-Jazirah, na Darfur, katikati ya uzembe wa kutisha na aibu ya kukosekana kwa serikali inayojiita “Serikali ya Matumaini”! Kuna matumaini aina gani wakati watu wanaishi katika mazingira yasiyostahili hata kwa wanyama—mazingira yanayotawaliwa na waenezaji magonjwa, ikiwemo mbu wa malaria, mbu wa dengue, na nzi?
Magonjwa yameingia katika kila nyumba, bila kumsaza mtu yeyote, haswa jijini Khartoum, ambapo hakuna nyumba isiyo na wagonjwa wa dengue. Serikali ikiwakilishwa na Wizara ya Afya, haifanyi chochote isipokuwa kuhesabu wagonjwa na wafu, na kwa kufanya hivyo, wanadhani wanaendelea vizuri! Serikali inatumia fedha kwa mambo ambayo hayana faida kwa wananchi, na inafuja fedha za umma kwa kila kitu isipokuwa afya za wanyonge wa nchi! Je, gharama na gharama nyenginezo za wajumbe waliosafiri kwenda New York kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa hazikuwa na manufaa yoyote na bila kutarajia mema yoyote kwa nchi na watu wake? Je, hazikutosha kunyunyizia dawa Khartoum na maeneo mengine yaliyoathirika na kuwaondoa waenezaji magonjwa?! Lakini kwa nini wafanye hivyo huku wao ni wauwaji walioachiliwa kwenye shingo za watu, na waajiriwa wanaoongeza idadi na takwimu, na kuwaomba mabwana zao katika Shirika la Afya Ulimwenguni na wengineo?!
Watu walitupa haki zao pale walipowaruhusu wanasiasa kama hawa vibaraka wa dola za kikoloni za kibepari kunyakua mamlaka yao na kuwatawala kwa njia nyingine zisizokuwa mfumo wa Kiislamu, na kwa hivyo fikra ya kwamba dola ndiyo yenye jukumu la kuchukua mambo ya raia wake imetoweka.
Chini ya mfumo wa Kiislamu, Mtume (saw) alizingatia afya na kuhimiza matibabu kwa wote. Yeye (saw) alipewa zawadi ya daktari, ambaye alimpeana kwa umma. Hospitali (hema la matibabu) ilikuwa karibu na Msikiti wa Mtume (saw) na ilisimamiwa na swahaba mtukufu wa kike Rufaydah al-Aslamiyyah. Katika zama zake zote za ustawi, Makhalifa na Maamiri wa Khilafah walianzisha hospitali za kuwatibu wagonjwa na kutoa matibabu ya bure kwa raia wote, bila kujali jinsia zao, dini zao, au madhehebu yao, wawe matajiri au maskini.
Watu wa Sudan, na dunia nzima, leo wanahitaji sana uangalizi na jukumu hili, ambalo litafanywa na Khilafah Rashida, tumaini la kweli na mwokozi wa wanadamu.
Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |