Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  22 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: HTS 1441 / 58
M.  Jumatatu, 13 Julai 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Mpito Yafutilia Mbali Hukmu ya Kuritadi ili Kuthibitisha Kujiondoa Kwake katika Utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Ikhlasi Yake katika Kuwatii Wamagharibi Makafiri
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Haki wa Sudan Nasruddin Abdel-Bari amefichua maelezo mapya kuhusu sheria ya mabadiliko tofauti tofauti, ambayo itachapishwa katika gazeti rasmi la serikali siku ya Jumapili 12/7/2020, (na hadi wakati taarifa hii ilipokuwa inaandikwa haikuwa imechapishwa) ili utekelezwaji wake uwe mara moja, na kuthibitisha kufutilia mbali kwake kifungu cha kuritadi (Sudan Tribune, 11/7/2020), na akasema katika kukutana kwake pamoja na runinga ya Sudan jioni ya Jumamosi, 11/7/2020: "Ikiwa kuna mtu anataka kubadilisha dini yake basi wewe huna haki ya kumuua, jambo hili halikubaliki zama hizi za sasa!!" na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok akaahidi kuendelea kwa uhakiki na marekebisho ya kikanuni Ili kushughulikia upotoshaji katika nidhamu ya kisheria kote nchini Sudan!! 

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tungependa kuweka wazi uhakika wa yafuatayo:

1- Hukmu ya sheria ambayo inaolea na hakuna chenye kuolea juu yake; ni hukmu ya Mwenyezi Mungu aliyeumba ulimwengu, mwanadamu na uhai; nayo ni kuwa yeyote aliye baleghe, mwenye akili timamu anaporitadi kutoka katika Uislamu, hulinganiwa katika Uislamu mara tatu, na hutengwa, akirudi ni kheri akikataa huuwawa, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَنْ يَرْتَدَّ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ذَلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ]

“Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua.” [Al-Ma’idah: 54], na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) anasema:

«مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ»

“Yeyote anayebadilisha dini yake, Muuweni” [Imesimuliwa na Bukhari]. Al-Bayhaqi na Darqutni wamesimulia: “Kwamba Abu Bakr alimtaka mwanamke mmoja kwa jina Umm Qarfah kutubia (kurudi katika Uislamu), kwa sababu alikuwa amekufuru baada ya yeye kuwa Muislamu, hakutubia na hivyo basi akamuua.”

2- Hakika yule anaye amua haki ni ipi ni Mmiliki wa haki, Mwenyezi Mungu subhanahu wa ta’ala, sio zama za sasa wala za zamani, wala sio kafiri mkoloni, wala chengine chochote miongoni mwa upotofu na upotevu!

3- Ama maneno ya Waziri Mkuu kuhusu upotoshaji katika nidhamu ya kisheria; ni neno la haki lakini lililo lengwa batili; ndio hazilingani hukmu ya kisheria ya kuritadi na hati iliyoundwa ya katiba; iliyo tungwa na miungu wa kisiasa wa Kiamerika kupitia mpatanishi wa Muungano wa Afrika, Mohamed El-Hassan Labat, ambapo iliitunga juu ya msingi wa hadhara ya kikafiri ya Kimagharibi na sheria zao.

Enyi Waislamu: Hakika mumedungwa kisu cha mgongo; pindi mulipo nyamazia kimya juu ya kujengwa maisha yenu juu ya msingi wa katiba batili zilizo wekwa na mwanadamu, na pindi mulipo salimisha mambo yenu kwa vibaraka wa Wamagharibi makafiri wanaowaongoza kwa hadhara yao inayonuka uvundo. Hakika amali ya kusimamisha Khilafah Rashida; ni utukufu mkubwa, ambayo ni wajibu kwa Muislamu anayetaka radhi za Mola wa Walimwengu, na kutokea kwa mageuzi ya kweli, asiiwache; kwa sababu ni Dola ya Khilafah Rashida pekee yenye kuondoa upotoshaji wa kisheria katika maisha yenu, pindi inapoweka katiba ambayo msingi wake ni wahyi, katika upande wa utabikishaji na utendakazi, huunda sheria na kanuni zote juu ya msingi wa wahyi huu mtukufu; ambapo ardhi itang'aa kwa nuru yake.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb it Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu