Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Sweden

H.  6 Shawwal 1443 Na: 1443 / 05
M.  Ijumaa, 06 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kufungwa kwa Shule Huru za Waislamu Kunalenga Kitambulisho cha Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, Dagens Nyheter, Göteborgsposten na Aftonbladet waliripoti kwamba Mamlaka ya Ukaguzi wa Shule ya Uswidi inabatilisha vibali vya shule mbili za kibinafsi za Waislamu kufuatia tahadhari kutoka kwa Huduma ya Usalama ya Uswidi kwamba wanafunzi wako katika hatari ya kupewa itikadi ya mfumo wa Kiislamu. Uamuzi huo unaathiri watoto takriban 300.

Hii si mara ya kwanza kwa Wakaguzi wa Shule wa Uswidi kubatilisha uidhinishaji wa shule huru za Waislamu na hivyo kuzifunga. Sio muda mrefu uliopita, iliamuliwa kwamba Shule ya Alazhar huko Vällingby ingefungwa, na kabla ya hapo kibali cha Römosseskolan huko Gothenburg kiliondolewa. Hii ilitokea licha ya ukosoaji kutoka kwa Afisi ya Ukaguzi ya Jiji kwa muamala wa wanasiasa dhidi ya Römosseskolan na uamuzi wa mahakama kwamba shule inaweza kuendelea kufanya kazi. Mahakama ya Kiidara ilisema kwamba "uamuzi wa Wakaguzi wa Shule unaingilia ndani sana na una madhara makubwa kwa mkuu wa shule na pia kwa watoto au wanafunzi". Kabla ya hapo, idadi kadhaa ya shule za kibinafsi za Waislamu zilikashifiwa na kisha kulazimishwa kufungwa. Licha ya ukosoaji huo, msako dhidi ya shule za Waislamu unaendelea na sasa shule mbili zaidi zinalazimika kufungwa na wanafunzi 300 wanalazimika kubadili shule.

Kufungwa kwa shule za kibinafsi za Waislamu si uamuzi wa kielimu unaotokana na matokeo mabaya au mapungufu katika ufundishaji, bali ni uamuzi wa kisiasa wenye nia ya chuki dhidi ya Uislamu. Shule nyingine kama vile Shule ya Christian Immanuel zimekosolewa kwa unyanyasaji wao wa masuala ya LGBT na watu wa LGBT kunyanyaswa shuleni, lakini hii haijasababisha msako dhidi ya shule hiyo na wala leseni haijaondolewa.

Upagawaji wa vyama vya kisiasa na wanasiasa na Uislamu, hofu ya kusonga mbele kwa Uislamu na kuchukizwa na mshikamano wa Waislamu katika Uislamu vinawapeleka kwenye kushindwa katika vita dhidi ya Uislamu ambapo kufungwa kwa shule za Waislamu ni mojawapo ya malengo mengi ya vyama hivi. Chama cha Social Democrats kilitaka kufunga shule za kibinafsi za Waislamu lakini sio za Kiyahudi. Waziri wa Elimu wa Uswidi, Anna Eksström, alisema kuhusiana na kufungwa kwa shule za Waislamu, "Tunataka kupata ukweli kwamba watoto na wanafunzi wanasomeshwa katika shule ambazo zinazidi kuwa tofauti." Kulingana na Eksström, "Tumeona kesi za ubaguzi wa kijinsia na maoni ambayo sio ya shule za Uswidi". Nia ya kufungwa kwa shule za Waislamu ni kuwavuruga akili watoto wa Kiislamu na kuwaingiza usekula kupitia kuwatupa katika shule za manispaa ambako wanaweza kuelimishwa kwa usawa kwa maadili yaliyo ya shule za Uswidi. Ndio maana Axel Darvik (L), kamishna wa Manispaa ya Baraza la Jiji la Gothenburg, alielezea uamuzi wa kufunga shule ya Römosse kama "wa kuwafurahisha watoto" na akasema kwamba watoto wa Römosse sasa watakuwa na "nafasi halisi ya kuoanishwa katika jamii ya Uswidi".

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisema kwamba uoanishaji ni ala ya kufuta kitambulisho cha Waislamu na kuwaoanisha kwa nguvu watoto katika maadili ya kisekula. Utangamano hauhusiani na lugha wala kazi. Muislamu anapaswa kuwa chanya na kuchangia kikamilifu katika jamii huku akihifadhi kitambulisho chake cha Kiislamu. Lakini uwiano leo unamaanisha kuacha maadili ya mtu na kuzama katika jamii na maadili yake. Ikiwa hujawiana, una msimamo mkali, tuhma isiyo na msingi ambayo kivitendo inamaanisha kutokumbatia maadili ya kisekula. Ndio maana Idara ya Usalama ya Uswidi ilionya kwamba watoto wako katika hatari ya kuwa na itikadi kali za Kiislamu. Maana yake hasa ni kwamba watoto wanalelewa kwa mujibu wa Uislamu. Kupagawa kwa serikali na kuyapiga vita maadili ya Kiislamu imewafanya kuwapa polisi uwezo wa kuzifunga shule nyingi hata bila ya ushahidi. Morgan Johansson, Waziri wa Haki, na Mikael Damberg, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, waliandika katika kipande cha maoni juu ya DN mnamo 2020 kwamba kazi kubwa ya polisi wa usalama imefunga shule 5 na wakatetea juhudi hizo kwa kusema "kufungwa kwa shule imeokoa mamia kutoka na kupewa misimamo mikali".

Kwa hiyo kufungwa kwa shule za kibinafsi za Waislamu kunapaswa kueleweka katika muktadha huu ambapo Uislamu daima uko chini ya mashambulizi na maadili ya Kiislamu kutatizwa. Hakuna tofauti kubwa kati ya kufungwa kwa shule, kuchomwa moto kwa Quran au kutekwa nyara kwa watoto wa Kiislamu na huduma za kijamii; ni ala tofauti tofauti tu ndani ya kisanduku cha ala za sera ya uoanishaji.

Kwa wanadamu wenzetu wasiokuwa Waislamu:

Chuki ya wanasiasa wenu kwa Uislamu imewasukuma kuyahujumu maadili na kanuni zenu katika vita dhidi ya Uislamu. Kila mtu anaweza kuwa na uhuru wa maoni isipokuwa Waislamu. Kila mtu anaweza kubaki na maadili yake isipokuwa Waislamu. Nyamko Sabuni alitaka wakimbizi kutoka Ukraine wawe na shule zao zenye mitaala yao huku Waislamu wakiwa hawaruhusiwi kuwa na shule zenye mtaala wa Uswidi. Sera ya chuki dhidi ya Uislamu hivi karibuni itakuwa ndio kuanguka kwa jamii endapo itaruhusiwa kuendelea kugusa kanuni za jamii. Waislamu wanaweza kufanya kila kitu sawa na kushinda mahakamani lakini wanasiasa huchomoa uafiriti wao kwenye shimo, Huduma ya Usalama ya Uswidi, kwa ushahidi wa siri na tuhuma kali ambapo tuhuma hii ndio ushahidi ambao hatuwezi kupambana nao. Mnamo 2019, Säpo ilikamata maimamu 5 bila kuwasilisha ushahidi wowote na kuwahukumu kufukuzwa nchini. Je, hivi ndivyo Uswidi inavyopaswa kuwa? Nchi ya kipolisi bila utawala wa sheria?

Waislamu Wapendwa:

Muna mfano mzuri kwa Mtume Muhammad (saw) wakati yeye pia alilazimika kuvumilia mateso na vitisho kwa sababu ya Uislamu. Fuateni mfano wake jilindeni nafsi zenu na watoto wenu kwa Uislamu, kupitia kuusoma Uislamu kimfumo, kuulingania na kuwasilisha masuluhisho ya Uislamu kwa ulimwengu. Ni hapo tu ndipo tunapoweza kujitengenezea kinga ya kuoanishwa. Aminini uwezo wa Uislamu kutatua matatizo ya mwanadamu na kuyafikisha kwa wanadamu.

Kwa vyama vya kisiasa na wanasiasa: Mnajua kwamba mfumo wenu uko katika mporomoko na tunafahamu kwamba mnajaribu kutia purukushani kutokana na kufeli kwenu na kuangamia kwenu kwa kuushambulia Uislamu. Lakini vita vyenu vya kibwege dhidi ya Uislamu vitaharakisha tu kuanguka kwenu. Kamwe hamtafanikiwa kuufuta Uislamu katika nyoyo za Waislamu, kwani ndani yake tumebeba maadili ya kweli ambayo hayauzwi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uswidi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Sweden
Address & Website
Tel: 
https://hizb-ut-tahrir.se/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu