Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Sweden

H.  14 Rabi' I 1445 Na: 1445 / 03
M.  Ijumaa, 29 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhalifu Unatokana na Mtindo wa Maisha wa Magharibi na Uoanishaji ni Jambo Kuu katika Kuenea kwake

(Imetafsiriwa)

Jioni ya Alhamisi, Septemba 28, Waziri Mkuu, Ulf Kristersson, alitoa hotuba kwa taifa kuhusu ghasia ambazo zimeharibu nchi, akisema kwamba "ni sera ya uhamiaji isiyo na uwajibikaji na uoanishaji uliofeli ambao umetufikisha hapa". Waziri wa Sheria, Gunnar Strömmer, pia alisema katika mahojiano na Dagens Industri iliyochapishwa Septemba 28 kwamba uhamiaji na uoanishaji duni ndio sababu kuu za wimbi la ghasia nchini Uswidi.

Waziri wa Nchi na Waziri wa Sheria wote wanadai kwamba uhalifu unatokana na uhamiaji, wakati ukweli wa uhakika ni kwamba uhalifu wa kupangwa na uundaji wa magenge haujatokea kati ya kizazi cha kwanza cha wahamiaji wa Kiislamu, ambacho kinabeba pamoja nacho mabaki ya maadili ya Kiislamu ingawa kizazi hiki cha kwanza kilifika katika nchi za kigeni kikiwa kimebeba hofu na wasiwasi pamoja na kutokea maeneo yenye vita kama vile Iraq, Syria, Lebanon na Somalia. Tunapoona kuenea kwa uhalifu wa kupangwa miongoni mwa wahamiaji wa kizazi cha pili ambao wamekulia katika mujtamaa wa Kimagharibi, katika taasisi za Kimagharibi, zilizojaa maadili ya Kimagharibi na kuvutiwa na viigizo vya Kimagharibi, ina maana kwamba tatizo hilo linahusishwa na thaqafa ya Kimagharibi.

ufyatiliaji risasi waziwazi barabarani, mapambano ya ushawishi katika mitaa, vurugu, mauaji na biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya ni jambo la asili na tabia ya miji mingi ya Magharibi na ni matokeo ya maadili ya uhuru wa kisekula; kama vile nadharia ya kuamua jambo kuwa baya au zuri kutokana na natija yake (utilitarianism) na dhana ya furaha. Maadili na desturi zinazotawala katika mazingira ya magenge hueleza thaqafa ya jamii za Kimagharibi, ambayo ni ile ya manufaa ya kimada isiyo na vima vya kiroho, kiakhlaki na kiutu. Maadili ya uhuru wa Kimagharibi hujenga fikra za vijana kwa msingi wa kuwa huru na kujitahidi kufikia mafanikio ya kimada. Ni wazi kwamba thaqafa ya Kimagharibi na maadili ya Kimagharibi yanayowakilishwa katika uhuru, manufaa ya kibinafsi na kujitambua kibinafsi yanafungamana na dhana ya Kimagharibi ya furaha ambayo imefungwa katika starehe za kimada. Mawazo ya wanachama hawa wa genge la wahalifu ni mawazo yale yale ya mabepari yanayoegemea juu ambao hushindana katika soko la biashara na ya wanasiasa wa Kimagharibi wanaofuata sera zenye msingi wa 'lengo huhalalisha njia'.

Sababu halisi ya uhalifu ni tabia ya utengaji ya thaqafa ya Kimagharibi inayosababisha ubaguzi wa rangi, ubaguzi na utelekezaji unaowaacha vijana hawa nje ya milango ya jamii bila ya kuwa na hisia za kuhusika jambo ambalo linawasukuma kujiingiza katika duara za uhalifu.

Mbali na siasa za ubaguzi zinazochangia uhalifu, kuna jambo jengine ambalo wanasiasa wanahusika nalo nalo ni sera ya uoanishaji ambayo imekuwa ikitaka kuwaowanisha Waislamu ndani ya maadili ya Kimagharibi na kuwaweka mbali na ufahamu safi wa Uislamu. ufahamu huu unaowapa kinga na kuwalinda Waislamu kutokana na maisha ya kabla ya Uislamu (jahilia) katikati ya uhalifu wa magenge wa kupangwa. Sera za utangamano zilizopitishwa na wanasiasa hao, ambazo wanaziona kuwa tiba na suluhisho la mzozo kati ya magenge, kwa hakika ni sababu kuu ya kuibuka uhalifu wa kupangwa miongoni mwa vijana wa Kiislamu. Utangamano umewatenganisha vijana na kitambulisho chao cha Kiislamu ili Uislamu usiathiri tena matendo yao na maisha yao yaelekezwe kulingana na maadili ya mtazamo wa usawa na makosa wa Magharibi.

Suluhisho pekee la uhalifu wa kupangwa wa magenge liko zaidi katika thaqafa na maadili ya Kiislamu na uchache katika maadili potovu ya Kimagharibi ya uhuru na manufaa haribifu. Hivyo basi, Waislamu lazima wajilinde kwa Uislamu kutokana na sera za lazima za uoanishaji na mitindo ya maisha yenye uharibifu ya Kimagharibi kwa kuimarisha kitambulisho chao cha Kiislamu. Uislamu hausuluhishi tu matatizo ya kijamii ya ulimwengu, bali mtindo wa maisha wa Kiislamu pia unatoa suluhisho la uhalifu wa kupangwa kwa kumpa mwanadamu maana na kuifunga suluki yake na hisabu Siku ya Kiyama.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uswidi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Sweden
Address & Website
Tel: 
https://hizb-ut-tahrir.se/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu