Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  17 Sha'aban 1443 Na: 08 / 1443 H
M.  Jumapili, 20 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Dhalimu wa Ash-Sham kwa Watawala wa Imirati

Watumwa Wakutana Kuwatumikia Mabwana zao
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa,18/3/2022, dhalimu wa Ash-Sham, Bashar Assad, alifanya ziara yake ya kwanza nchini UAE tangu kuzuka kwa mapinduzi ya Syria miaka 11 iliyopita. Alikutana na viongozi wengi walioeleza nia yao ya kuimarisha uhusiano na Syria kwa mara nyingine tena.

Enyi Waislamu katika Ardhi Tukufu ya Ash-Sham:

Ziara hii inathibitisha kwa mara nyingine tena kwamba watawala Ruwaybidhat (wajinga) katika ardhi zetu wanasimama pamoja dhidi ya Ummah, hata kama ngozi na barakoa zao zinatofautiana. Wako katika utumishi wa mabwana zao katika dola za kikafiri, wako vitani dhidi ya Ummah wao, Dini na wanawe wenye ikhlasi.

Mauaji na uhalifu wote uliofanywa na Bashar, dhalimu wa Ash-Sham, dhidi ya watu wa Ash-Sham, haukuwazuia watawala wa Imarati kuendelea na uhusiano wao naye na kumpokea katika nchi yao katika utekelezaji wa mipango na amri za mabwana zao wa Kiingereza na Marekani dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham haswa na watoto wa Ummah kwa jumla.

Na sote tunajua kwamba wahalifu na wapanga njama wote dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham walifanya hivyo kwa idhini kutoka kwa mkuu wa uhalifu, Marekani, ambayo ilikuwa na bado ingali inamuunga mkono kibaraka wake, Bashar, na kuzuia kuporomoka kwake.

Ndiyo iliyowaruhusu wanamgambo wa Iran, chama cha Iran nchini Lebanon na wengineo kuingia ili kuziba pengo lililotokana na kujitoa kwa maafisa na wahusika kutoka katika jeshi la dhalimu wa Ash-Sham, na ndiyo iliyoruhusu kuingia kwa majeshi ya Urusi ili kumuunga mkono kutoka angani na kufanya mauaji ya kutisha dhidi ya watu wa Ash-Sham. Ndiyo iliyogawanya majukumu kwa zile nchi zilizoitwa zenye kutoa usaidizi ili kuwadhibiti viongozi wa mfumo wa makundi; kuyanyang'anya uamuzi yake, kuupora utashi wake na kulemaza harakati zake, na bado inajitahidi kupenyeza ukataji tamaa katika nyoyo za watu wa mapinduzi ya Ash-Sham, na kuuhifadhi utawala wa kibaraka wake, dhalimu wa Ash-Sham. kwa kuweka masuluhisho yake ya kisiasa yenye nia mbaya huko Geneva, ambayo la kwanza kabisa ni Azimio 2254 la Baraza la Usalama.

Ziara hii inakuja kama hatua katika njia ya kuuzaa upya utawala wa kihalifu na kuvunja kutengwa kwake. UAE haikuwa peke yake katika kucheza dori katika mchezo wa kuvunja kutengwa na usawazishaji mahusiano na dhalimu wa Ash-Sham. Badala yake, kundi la nchi zilifuata njia hii, ikiwemo Tunisia, Oman, Misri, Iraqi, serikali ya Al Saud, na nyenginezo. Licha ya hapo awali kudai kuunga mkono mapinduzi ya Ash-Sham, Abu Dhabi ilifungua tena ubalozi wake jijini Damascus mnamo Disemba 2018, na tangu wakati huo imetoa wito wa kuregeshwa kwa Syria katika Jumuiya ya nchi za Kiarabu.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Nyumba ya Uislamu:

Mnaona kwa macho yenu njama za nchi dhidi ya mapinduzi yenu, juhudi zao zisizo na kikomo za kuyabatilisha na kupoteza muhanga wake. Ni wakati muafaka sasa wa kukomesha ghiliba za nchi hizi na ushiriki wao katika kumwaga damu yetu na kuongeza ugumu wetu. Tushikeni kamba yenye nguvu ya Mwenyezi Mungu Peke Yake na tumtegemee Yeye, hatuna yeyote ila Mwenyezi Mungu. Wajibu wetu sasa ni kuharakisha ili kuyanusuru mapinduzi yasiporomoke, na kufanya kazi kwa bidii na ikhlasi pamoja na wafanyaji kazi wenye ikhlasi ili kuipindua serikali hii ya kihalifu na kuusimamisha utawala wa Uislamu mahali pake. Na ikiwa hatutaharakisha kufanya hivyo, tutakuwa miongoni mwa wale wanaoisalimisha hatma yao kwa maadui zao na kuwapa faida ya shaka, na tutakuwa, baada ya kuwa tumejitoa muhanga mkubwa katika mapinduzi makubwa zaidi, mithili ya yule anayeukunjua uzi wake uliosokotana baada ya kuwa imara. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنْكَاثاً) “Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu.” [An-Nahl: 92].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu