Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  21 Rabi' I 1444 Na: 05 / 1444 H
M.  Jumatatu, 17 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mapigano Mapya ya Kimakundi kati ya Vipengee vya Mfumo na Makundi Yanayohusishwa ni Jinai dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham na Kupuuza Hatima yake
(Imetafsiriwa)

Maeneo ya Ngao ya Furat na Operesheni Tawi la Mzaituni, kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Aleppo, yameshuhudia mapigano makali kwa siku kadhaa kati ya vipengee vya mfumo wa makundi yanayohusishwa na utawala wa Uturuki, kutokana na kuhusika kwa wapiganaji wa Kitengo cha Hamza katika mauaji ya mwanaharakati wa vyombo vya habari Muhammad Abu Ghannoum na mkewe, ambaye alitumiwa kama kisingizio cha kutatua hesabu na kupanua ushawishi na udhibiti.

Enyi Waislamu katika Ardhi Tukufu ya Ash-Sham: Suala la mapigano kati ya vipengee vya mfumo wa makundi yenye uhusiano ni suala lililofanywa upya ambalo limeambatana na miaka ya mapinduzi ya Sham kwa muda mrefu, na kila mara kundi miongoni mwa makundi huvunjwa na kufukuzwa uwanjani kwa visingizio mbalimbali. Wanaouawa ni watoto wa watu wa Ash-Sham ambao wanauawa kwa ajili ya kufanikisha maslahi na njama za waliofanya njama kwa Mapinduzi ya Ash-Sham, ili kutimiza matakwa ya viongozi wao kwa ajili ya ushawishi, udhibiti na uchangishaji fedha.

Hapana shaka kuwa mapigano haya yaliyoharamishwa yana madhara makubwa kwa mapinduzi na watu wake, pale wanapowaona watu wa handaki moja wakiuana wao kwa wao, wakiharibu silaha zao kwa mikono ya wao kwa wao, na kupoteza silaha zao na zana zao, na badali yake, dhalimu wa Ash-Sham anafurahia amani na usalama kwa ufunguzi wa vivuko kwa ajili ya maandalizi ya maridhiano naye.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Makao ya Uislamu: Wote wamefahamu ukweli kwamba viongozi wa mfumo wa makundi wanahusishwa na ujasusi wa nchi zile zinazoitwa zenye kuunga mkono, zinazoongozwa na ujasusi wa utawala wa Uturuki, utawala huu ambao waziri wake wa mambo ya nje alitoa wito hadharani kwa wale wanaoitwa upinzani kupatana na dhalimu wa Ash-Sham, muuaji wa wanawake, watoto na wazee na mbakaji wa heshima. Utawala huu ambao unaenda kwa kasi kwenye kuhalalisha tena mahusiano na utawala wa halifu wa Assad, na kuregesha uhalali wake, ili kuuzalisha tena. Utawala huu ambao umedhihirisha sura yake halisi inayotaka kuyabatilisha Mapinduzi ya Ash-Sham na kupoteza mihanga yake na kumwaga damu za mashahidi wake, utawala huu ambao unadhibiti maamuzi ya mfumo wa makundi katika vipengele vyake vyote, na unawaruhusu kupigana wao kwa wao  katika mapigano ya haramu ya kimakundi. Na kwa kweli, munaweza kuona baraka za serikali ya Uturuki kwa mapigano haya, ambapo munakumbuka uwezo wake wa kuyazuia makundi kuchukua hatua yoyote dhidi ya serikali iliyodhoofika ya kihalifu.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Makazi ya Uislamu: Kunyamaza kwenu kuhusu mapigano haramu ya makundi ambayo kwayo watoto wenu wanauawa, na yale yanayotayarishwa kwa ajili ya mapinduzi ya maridhiano na dhalimu wa Ash-Sham, na yale yaliyotangulia ya kufungua vivuko pamoja naye, ni kujiua kisiasa na kujisalimisha kwa hatima isiyoepukika ambapo mutarudi kwenye mshiko wa serikali na kisasi chake. Hakutakuwa na manufaa baada ya majuto. Ni lazima muregeshe uamuzi wenu mulioporwa na mamlaka yenu muliyonyang'anywa, kama hatua ya kwanza kwenye njia ya kurekebisha mkondo wa mapinduzi.

[...وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَنْ يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ]

“…Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.” [Muhammad: 47-35]

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu