Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  10 Rabi' II 1444 Na: 07 / 1444 H
M.  Ijumaa, 04 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Daraa kwa Mara Nyengine Tena iko katikati ya Chuma cha Utawala wa Kihalifu na Nyundo ya Makundi ya Maridhiano
(Imetafsiriwa)

Mji wa Jasim ulizingirwa mwezi Agosti mwaka wa 2022. Kisingizio cha hilo kilikuwa uwepo wa chembechembe za ISIS katika mji huo. Mji huo baadaye ulivamiwa mnamo Oktoba; wengi waliuawa wakati wa uvamizi huo. Kabla ya hapo, mji wa Tafas ulishuhudia mandhari hiyo hiyo, na utawala wa kihalifu ulijaribu kuuvamia na kuzua mifarakano miongoni mwa wakaazi wake. Leo hii jiji la Daraa linaregea tena mbele kwa kutumia kisingizio kile kile, chenye mandhari ile ile potofu, na kwa namna ile ile iliyotumiwa katika miji ya Tafas na Jasim.

Madhumuni ya moja kwa moja ya vitendo hivi na ujanja huu ni jaribio la utawala wa kihalifu la kuzusha hitilafu kati ya watoto wa Hawran na kuwagonganisha wao kwa wao ili uweze kuregesha udhibiti wa miji na vijiji ya Hawran tena. Utaweza tu kufanya hivyo kupitia kuwamaliza watu wenye ikhlasi ambao hawakusalimu amri kwenye makubaliano ya maridhiano, na wanaokataa nguvu za utawala wa kihalifu na mawakala wake wa kijasusi kuingia katika miji na vijiji ya Hawran. Kisingizio cha hili kipo; ni kupatiliza fursa ya uwepo wa baadhi ya wanachama wa zamani wa kundi la Islamic State (ISIS) kumuondoa kila mtu anayesimama kama kizingiti katika njia ya mipango yake. Lakini kutokana na ulemavu wake, inapanga njama na kutoa vishawishi vya kutumia baadhi ya makundi ya maridhiano (makundi ya usaidizi wa usalama wa kijeshi) ili kuwamaliza wale wanaokataa udhibiti wa utawala wa kihalifu na wanaokabiliana na njama zake.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham kwa jumla na kwa watu wetu wa Hawran haswa:

Utawala wa kihalifu, baada ya kushindwa katika majaribio yake yote baada ya makubaliano mabaya yaliyotiwa saini na viongozi wa mfumo wa makundi, sasa unajitahidi sana kukomesha harakati zozote za kimapinduzi ndani ya miji na vijiji vya Hawran, na kuweka udhibiti wake tena, wakati huu. si moja kwa moja mkononi mwake, bali kwa kuwapiga wana wenu ni dhidi ya kila mmoja wenu, na kujenga mabishano baina yenu kwa lengo la kuwafarakanisha, na kutengeneza mpasuko kati ya kitambaa chenu ambacho hapo awali kilikusaidia kustahimili na kusimama kwenye kampeni zake nyingi.

Utawala wa kihalifu, baada ya kufeli katika majaribio yake yote baada ya makubaliano mabaya yaliyotiwa saini na viongozi wa mfumo wa makundi, sasa unajitahidi sana kukomesha harakati zozote za kimapinduzi ndani ya miji na vijiji vya Hawran, na kulazimisha udhibiti wake tena, wakati huu si moja kwa moja mkononi mwake, bali kwa kuwagonganisha watoto wenu dhidi ya wao kwa wao, na kuunda mizozo baina yenu kwa lengo la kuwafarakanisha, na kutengeneza mpasuko kati ya muundo wenu ambao hapo awali ulikusaidieni kustahamili na kusimama kwenye kampeni zake nyingi.

Hapo awali umefanya vyema katika kazi nyingi za kijasusi, na umesajili wengi walioisaidia kufikia hatua unayotafuta. Kwa hivyo, jihadharini na kuingia katika mtego huo huo na muwe macho na tahadhari dhidi ya utawala huu wa kihalifu na wa kijanja.

Na jueni kwamba yeyote aliyeridhiana na Al-Assad na anayefanya kazi chini ya bendera yake hatajali usalama wenu au usalama wa watoto wenu na ardhi zenu, kama anavyodai kwa kirongo, basi je mbwa mwitu hukabidhiwa kondoo?

Sasa munaweza kuona kwamba leo yule “anayeitakasa” Hawran, kama anavyodai, ndiye aliyetia saini ya kuisalimisha, na yeye mwenyewe ndiye aliye kula njama na nchi zilizo kula njama ili kuyaavya mapinduzi ya Ash-Sham ndani ya shina lake.

Enyi Watu wa Hawran: Kuweni kama vile tulivyo kuwa tukishuhudia muko, kwani nyinyi ndio chimbuko la mapinduzi, ngao yake, ngome yake isiyopenyeka, na jabali ambalo njama zote zinavunjwa dhidi yake. Jihadharini na kuingia katika mtego wa huduma za kijasusi za utawala wa kihalifu, na kuburutwa katika mapigano ambayo yatazalisha chuki na kinyongo ambazo utawala wa kihalifu unafanya kazi kuzipanda kupitia silaha zake. Kwa hivyo, jihadharini na zana zake ambazo zimefichuliwa katika miaka iliyopita, na murudi kama mwili mmoja, na waelekezeni watoto wenu kusimama dhidi ya utawala wa kihalifu na makundi washirika wake, kuwa upande wa wenye ikhlasi kati ya miongoni mwa ndugu zenu na watu wako, na lengo letu na liwe ni kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na kuinusuru Dini yake.

[هَذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ]

“Hii (Qur'ani) ni hoja zinazo toka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu na rehema kwa watu wanao amini.”  [Al-A’raf: 206]

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu