Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  8 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 04 / 1445 H
M.  Alhamisi, 16 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Faili ya "Kutekwa nyara na Kutoweka" ni Sanduku Jeusi Linalofichua Kiwango cha Uhalifu wa Uongozi wa Shirika la HTS
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 14/5/2024, kikao kilichofanywa na kundi la familia na jamaa za watu waliotekwa nyara katika magereza ya usalama ya Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) kilitawanywa kwa njia ya kijambazi na ladha ya Assad. Kikao hicho kilikuja baada ya uahirishaji mambo mengi na shirika la HTS kuhusiana na hasa suala hili.

Faili "utekwaji nyara" inachukuliwa kuwa mojawapo ya faili hatari zaidi ambazo uongozi wa HTS unaweka siri. Inafanya kazi kwa njia mbalimbali kukomesha jaribio lolote la kufichua faili hii au kutoa mwanga juu yake.

Faili ya "utekwaji nyara na kutoweka" inafanana na faili ya "watu waliopotea" inayoshikiliwa na utawala wa kihalifu wakati wa matukio katika gereza la Hama na Palmyra. Wengi wao walimalizwa kwa njia za kihalifu za kuogofya, na kuzikwa katika makaburi ya halaiki yasiyojulikana. Leo, Al-Julani na vyombo vyake vya ukandamizaji hadharani viko katika nafasi hiyo hiyo. Kuna madai mengi ya kufichua hatima ya watu waliotekwa nyara, na msukumo wa kujua hatima yao ni mkubwa, hasa baada ya kupata taarifa za kumalizwa kwa idadi kubwa ya watu waliotekwa nyara; chini ya msamiati “tulimkata!”

Kulingana na jambo hili, uongozi wa HTS haukuwa na chaguo ila kusonga na ukatili wote na kutawanya kikao hicho mjini Idlib. Ilichora, kupanga, na kutumia zana. Iliandika hali hiyo na haikujali ukubwa wa udhaifu wake, wepesi, na kiwango cha kusema uwongo ndani yake. Kisha, iliendelea kutawanya kikao hicho kwa nguvu nyingi za kijambazi, bila kujali matokeo. Kwake, kubeba matokeo ya kutawanywa kwa kukaa ndani ni rahisi zaidi kuliko kubeba matokeo ya kufichua ukweli juu ya mamia ya watu waliouawa (kukatwa) katika magereza yao na kuzikwa kwenye makaburi ya halaiki yasiyojulikana!

Mbinu ya kutawanya walioketi ilifichua ukubwa wa uhalifu wao. Hakuna kilichokatazwa kwao. Kila uhalifu unaruhusiwa ili kuhifadhi nafasi zao. Kwa hivyo, wanafuata njia ya utawala wa kihalifu, hadi wakamilishe dori yao ya kuwaondoa wana waadilifu wa mapinduzi ya Ash-Sham na kuwarudisha wale waliobaki chini ya udhibiti wa utawala wa kihalifu.

Ukweli kuhusu uhalifu wa uongozi wa Hay'at Tahrir al-Sham na vyombo vya ukandamizaji wa umma umejitokeza. Hivi ndugu zetu Mujahidina watakaa kimya kuhusu dhulma ya uongozi huu hadi lini na kukataa hata kauli mbiu uliokuwa ukitoa?! Je, wakati haujafika kwao kuacha msimamo wao hasi wa kutoegemea upande wowote na kuanza kuegemea kwa watu wao na mapinduzi yao?

Dhulma ya Al-Julani, majambazi wake, na vyombo vya umma vya ukandamizaji itaongeza tu kwa watu wa mapinduzi na harakati yake iliyobarikiwa azma ya kuendelea hadi wayaokoe mapinduzi yao, wapate tena udhibiti wa maamuzi yao, na kuendelea na njia yao hadi kupinduliwa kwa madhalimu wote na kusimamisha utawala wa Kiislamu kwenye magofu yao, na hilo litakuja karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَنُرِيدُ أَنْ نَمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ]

“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.” [Al-Qasas: 5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu