Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  10 Jumada I 1446 Na: 04 / 1446 H
M.  Jumanne, 12 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sura Mpya ya Walaji Njama katika Astana 22

Imetanguliwa na Mkutano huko Tarnaba na Majadiliano kuhusu Kufungua Barabara na Vivuko vya Kimataifa

(Imetafsiriwa)

Uchunguzi wa Syria ulifichua kuwa mkutano ulifanyika kati ya maafisa wa ujasusi wa Urusi na Uturuki katika kijiji cha Tarnaba, magharibi mwa mji wa Saraqib. Uchunguzi huo iliongeza kuwa mkutano huo ulizingatia hali ya Idlib, kupunguza hali ya taharuki, na kufanya kazi ya kufungua njia za kimataifa na za kibiashara. Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano ya awali kati ya pande hizo mbili, pamoja na mikutano ya Uturuki na makundi ya upinzani, kama ilivyoripotiwa na Uchunguzi huo.

Raundi ya 22 ya mikutano ya Astana juu ya faili ya Syria ilianza katika mji mkuu wa Kazakh, Astana, mnamo Jumatatu, Novemba 11, kwa ushiriki wa wajumbe kutoka Uturuki, Urusi na Iran, pamoja na wawakilishi wa serikali ya kihalifu na “upinzani” wa nyumbani na wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, na waangalizi kutoka Jordan, Lebanon na Iraq, chini ya kisingizio cha kutafuta suluhisho la “mgogoro” wa Syria, hatua za kujenga imani kati ya wahusika, ujenzi mpya na kuregea kwa watu wa Syria nchini mwao.

Makongamano, mikutano na njama; lengo lao kuu ni kuyamaliza mapinduzi na kuyaregesha kwenye kifua cha utawala, mipango iliyobeba jina la kupoteza  mihanga mikubwa iliyofanywa na mapinduzi hayo, lengo lao ni kuregesha uhalali kwa dhalimu wa Damascus; hatua mpya zinachukuliwa na waliokula njama na zana zao kutekeleza “suluhisho la kisiasa la Amerika” lenye sumu linalowakilishwa na Azimio 2254.

Enyi Waislamu katika ash-Sham, Makaazi ya Dar ul-Islam: Kunyamaza kwenu leo ​​kuhusu mchakato ulioelezwa wa uuzaji unaofanywa kwa kutafakariwa kabla na kimakusudi na walaji njama ni kujiua kisiasa ambako kunaweza kuchangia kukomesha mapinduzi yenu. Tangu uamuzi wa mapinduzi kuibiwa na kuporwa, mapinduzi yamekuwa yakihama kutoka njama moja kwenda nyingine hatari zaidi kuliko ile ya awali, na pengine njama hii ndiyo hatari zaidi, hasa kwa vile kuendelea nayo itasababisha kurudi kifuani kwa utawala mhalifu. Munaona jinsi mambo yanavyozidi kuwa mabaya hadi mabaya zaidi, kutoka kwa dhiki hadi dhiki, kwa hivyo kuweni waangalifu sana musije mukaingia kwenye meno ya dhalimu mhalifu. Kwa hivyo, chukueni hatua na muregeshe uamuzi wenu wa kufanya mapinduzi kabla hamjachelewa.

Enyi Wana Mapinduzi: Tusikilizeni, sisi ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir Al-Nadheer Al-Aryan (mwonyaji wa wazi), ndugu zenu ambao mumeyaona maneno yao kuwa ya kweli na ambao kuona kwao ni kukubwa. Sisi hatuhitaji fadhila katika jambo hili juu yenu, kwani huu ni wajibu wetu na tutakutana nao kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Tunakuombeni nyinyi, watu wetu, mufanyeni haraka kuregesha uamuzi wenu kutoka kwa waliouiba, kwani nchi na zana zao ni mikono yenye nia mbaya inayotaka kukuangamizeni.

Enyi Waislamu katika ash-Sham, Makaazi ya Dar ul-Islam: Mumeona kwa macho yenu jinsi nchi zote zinavyo kula njama za kuyamaliza mapinduzi yenu na kupoteza mihanga yenu. Wajibu leo ni kuzikataa nchi hizi na miradi yao hatari na kuupitisha mradi ambao una wokovu na utukufu wetu, mradi unaotokana na Aqidah yetu ya Kiislamu, ambao kupitia kwao tunadhamini radhi za Mola wetu Mtukufu na ushindi Wake kwa ajili yetu, Mwenyezi Mungu akipenda.

Njia pekee ya kuyaokoa mapinduzi ni kuregesha uamuzi ulionyakuliwa na kutembea pamoja na mwongozo na utambuzi nyuma ya uongozi wenye ikhlasi, utambuzi na unaobeba mradi wa Uislamu, ili tuweze kuibuka kutoka katika mkanganyiko na hasara tuliyomo.

Enyi Wana Mapinduzi, Enyi Mliojitolea na Kutoa: Tambueni mapinduzi yenu kabla ya kuuzwa, na mregeshe uamuzi wenu, kwani wokovu ni wokovu, na tahadhari ni tahadhari, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[اسْتَعِينُوا بِاللهِ وَاصْبِرُوا إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ]

“Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu.” [Al-A'raf  7:128].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu