Alhamisi, 30 Rajab 1446 | 2025/01/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  23 Rajab 1446 Na: 11 / 1446 H
M.  Alhamisi, 23 Januari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pesa Zilizotumika Kutuua, Tunawezaje Kujitolea Kuzilipa?!
(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano na gazeti la ‘Financial Times’, waziri wa mambo ya nje wa Syria alifichua ruwaza ya serikali mpya ya Syria baada ya Assad, akisisitiza kwamba nchi hiyo “haitaki kuishi kwa msaada,” na kwamba suluhisho liko katika kupunguza vikwazo vya Amerika na Ulaya. Aliongeza kuwa serikali haina mpango wa kusafirisha mapinduzi hayo ng’ambo au kuingilia masuala ya nchi nyingine. Hivyo, ikionyesha mabadiliko makubwa katika sera ya kigeni. Pia alionyesha katika mahojiano yayo hayo nia ya kubinafsisha bandari na viwanda vinavyomilikiwa na serikali na kuvutia uwekezaji wa kigeni, licha ya changamoto kubwa zinazoikabili Syria, ikiwemo madeni ya dolari bilioni 30 kwa washirika wa zamani wa Assad; Iran na Urusi.

Katika miaka yote ya mapinduzi, watu wa Ash-Sham wameonja aina zote za jinai za Iran; ukatili wake na umwagaji damu, jinai na mauaji yake, na fikra yake ya madhehebu yenye chuki ambayo iliitumia kama kiongozi katika kupiga vita mapinduzi ya Ash-Sham na wanawe waaminifu. Iliua wanamapinduzi wengi na kufanya mauaji mengi. Ilibeba mradi wake wa madhehebu wa Kifursi na kuteketeza ardhi na watu ili kuutekeleza. Ilijaribu sana kumaliza mapinduzi yetu na kuturudisha kwenye kifua cha utawala tena. Lakini juhudi zake zilishindikana na pesa na juhudi zake zilikuwa janga kwake. Baada yake ilikuja Urusi yenye chuki, ilikuja kwa nguvu zake zote, ilikuja na ndege zake hatari, na ilifanya mauaji baada ya mauaji. Haikuheshimu udugu wala ahadi yoyote na watu wa mapinduzi. Ilifanya ukatili na kupanga vitimbi, na njama zake zikarudishwa kwake yenyewe, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu. Mwishowe, ilishindwa na juhudi zake hazikufaulu.

Enyi Watu wa Ash-Sham: Haya ni baadhi ya matendo ya wahalifu wa Urusi na Iran. Hakuna pesa kulipwa kwa watu kama hao, na hakuna haki zinazotambuliwa. Bali wanadaiwa kulipa fidia kwa makosa waliyoyafanya dhidi ya watu wa Ash-Sham, na wanapaswa kutendewa uadui wa wazi. Waliua na kutuhamisha wengi wetu. Hawa wauaji wahalifu ndio wanapaswa kulipa na kutoa fidia kwa waliouawa na kuhama makaazi yao. Wauaji hawa wahalifu wenye chuki, hawana haki nasi. Kwa hiyo, ni lazima wawajibike, wadaiwe, na kuonja kutoka kwenye kikombe cha hila, uhadaifu na njama zao.

Watu hawa katika ulingo wa kisiasa wanawajibishwa, na fedha walizolipa ni shahidi dhidi yao na si haki waliyo nayo, kwa sababu kukiri kwetu kuwa wana madeni na fedha ni kukiri waziwazi uhalali wa jinai zao.

Watu hawa lazima wawajibishwe haraka iwezekanavyo, na hatua ya kwanza ya kuwawajibisha ni kufukuzwa kwao kutoka Ash-Sham na kufukuzwa kwa kambi zao kutoka Ash-Sham.

Walicholipa kilikuwa dhidi ya mapinduzi yetu na kwa ajili ya kutuua.

Kukabiliana na wahalifu hawa na nchi nyingine zinazokula njama kunafanywa kwa kuchukua misimamo ya kimfumo tuliyolazimishiwa na Aqidah (itikadi) yetu ya Kiislamu, sio kwa kuwabembeleza na kuwaridhisha! Kunafanywa kwa kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili kuunda jeshi lenye nguvu linaloilinda nchi, huku msingi wake ukiwa ni Mujahidina wenye ikhlasi, na kuwategemea wanamapinduzi wenye ikhlasi ili nguvu na uwezo wao uwe katika kuutumikia Ummah wao, kwani wao ni watu wa kujitolea na subira katika muhanga.

Ni wajibu wetu kujitahidi kuunganisha misimamo ya mapinduzi ya Ash-Sham na kujitahidi kumridhisha Mola wetu peke yake kwa kusimamisha dola yake, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume na kutabikisha Shariah Yake. Katika hilo pekee ndiko kwenye masuluhisho ya kweli yatakayotatua matatizo yetu yote, kwa sababu tutakuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Peke Yake, na Yeye (swt) atatunusuru dhidi ya vitimbi vya wapangaji.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Mfano Hatari Ambao Haupaswi Kupuuzwa

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu