Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  20 Jumada II 1445 Na: 09 / 1446 H
M.  Jumapili, 22 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfano Hatari Ambao Haupaswi Kupuuzwa
(Imetafsiriwa)

Katika mfano hatari katika historia ya mapinduzi, Huduma Kuu ya Usalama mjini Aleppo iliteka nyara wanawake kumi mnamo siku ya Jumamosi, 21 Disemba 2024. Wanawake hao walikuwa wamejitokeza wakiandamana, wakitaka utawala wa Uislamu na kuachiliwa huru waume zao, vijana wao na watoto wao waliotekwa nyara zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita. Watu hawa wamefungwa jela na Jolani [al-Julani] mjini Idlib tangu Mei 7, 2023!

Tunawahutubia watu wote wa mapinduzi na wanaharakati miongoni mwao, wakiwemo wapiganaji, wanafunzi, wataalamu wa vyombo vya habari, wasomi, na mashirika: Je, mapinduzi haya, pamoja na kujitolea muhanga na mamilioni ya waliokufa mashahidi na watu waliohamishwa makaazi yao, yalizinduliwa kwa ajili ya hili? Je! ilikuwa ni kwa vitendo kama hivyo, kuiga yale ambayo utawala wa kihalifu wa Assad ulifanya kwa miongo kadhaa?

Ni kinaya kwamba huku wanawake wasiokuwa na hijab jijini Damascus wanaweza kuandamana kwa uhuru kwa ajili ya usekula na uhuru bila mtu yeyote kuwaingilia, wanawake wema wanaotaka kutekelezwa kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu na kuachiliwa huru kwa vijana wao ambao wametekwa nyara kwa muda wa mwaka mmoja na nusu wangali wametekwa nyara!

Enyi Watu wa Mapinduzi, mliojitolea muhanga na kuvumilia mengi: Je, mapinduzi haya hayakuanza ili kulinda heshima ambayo utawala dhalimu wa Assad ulikuwa umekiuka? Je, sasa tunaweza kukubali kuregeshwa kwa sera kama hizo, zinazolenga wanawake wema?

Mapinduzi ya Al-Sham yalichochewa na kauli moja ya mhalifu Atef Najeeb, ambapo aliwatukana wanawake waheshimiwa wa Daraa. Leo, tunashuhudia kutekwa nyara kwa wanawake wema katika hatua ya kwanza ya usalama baada ya kuanguka kwa utawala wa kihalifu. Jihadharini na kukaa kimya juu ya vitendo kama hivyo, kwani heshima ni mstari mwekundu, ambao maisha hutolewa kafara, na kila rasilimali ya thamani hutumiwa.

Enyi Watu wa Mapinduzi, je, mtakubali kwamba wanawake kumi waliotaka kuondolewa dhulma waliyotendewa, watekwe nyara huku wanawake walio bila ya hijab, ambao mwanzoni walitoa wito wa kuuwawa watoto na wanawake, wanaruhusiwa kuandamana kwa uhuru? Na wapi? Jijini Damascus, jiji la Bani Umayya, na katika uwanja ulioitwa kwa jina lao!

Mcheni Mwenyezi Mungu kwa heshima yenu, ambayo kwayo mliibuka katika mapinduzi. Jihadharini na kukaa kimya, kwa maana matokeo yake ni makubwa, na majuto yatakuja wakati mushachelewa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu