Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  19 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 / 09
M.  Jumatano, 30 Juni 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania Yazuru Ubalozi wa Pakistan Kuitaka Kukomesha Utekaji wa Kimabavu wa Naveed Butt

Kufuatia kampeni ya kilimwengu inayoendelea ya kunyakuliwa Naveed Butt, msemaji wa Hizb ut Tahrir, Wilaya ya Pakistan ambaye alitekwa nyara na shirika la kijasusi la Pakistan zaidi ya miaka 9 iliyopita.

Jana tarehe 29 Juni 2021, Hizb ut Tahrir Tanzania ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan jijini Dar es Salaam ulioongozwa na Masoud Msellem, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Tanzania akiwa pamoja na Said Bitomwa, Mjumbe wa Afisi ya Habari, kwa dhamira ya kupeleka taarifa rasmi ya Hizb ut Tahrir yenye anuani: “Wito wa Kutaka Kumalizwa kwa Kupotezwa kwa Nguvu kwa Naveed Butt Nchini Pakistan” taarifa hiyo imeitaka Pakistan kumuachia huru mara moja mhandisi Naveed Butt aliyetekwa mnamo tarehe 11 Mei 2012 kimabavu na kihalifu na mchana kweupe mbele ya watoto wake. Tangu muda huo mpaka leo familia yake imebakia gizani wakiwa hawajui alipo Naveed.

Baada ya kusawazisha taratibu za kiusalama Ubalozini hapo, ujumbe ulikutana na Bwana Nafees Wahab, Afisa Utawala, ambapo ujumbe ulijitambulisha kwake na kumueleza lengo lao. Katika hali ya kuonesha mashirikiano Afisa huyo (wa ubalozi) akapokea nyaraka za ujumbe, kuzikagua na kuutaka ujumbe uketi kwa subra huku akiratibu mkutano baina yao na mkubwa wake (balozi)

Ujumbe ulikutana na Bwana Azam Bihan, Makamu wa Balozi, ulizungumza naye kuhusiana na kadhia ya kutekwa Naveed, na ukataka kukomeshwa mara moja kutekwa huko kwa mabavu. Majibu ya Bwana Bihan yalikuwa, akiwa kama mwakilishi wa serikali ya Pakistan amepokea risala ya ujumbe huo, na ataifikisha kwa serikali yake, endapo atapokea majibu yoyote juu ya kadhia hiyo kutoka serikalini, atawasiliana na ujumbe huo kwa kutumia anuani zao.

Muda umefika kwa mukhlisina ndani ya mamlaka za Pakistan na kwa wale wote wenye athari na ushawishi kubeba jukumu la kufedhehi tendo hili la aibu na kusimama thabiti na Uislamu na haki, wasimame kwa kupinga vikali dhulma na uvunjaji haki wa serikali ya watawala wa kihuni na vibaraka pamoja na mabwana zao wa Magharibi, ili achiwe huru Naveed Butt ili arudi kwa  familia yake baada ya miaka ya maumivu na kuwa kizuizini.

Masoud Msellem

Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu