Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  16 Ramadan 1445 Na: 1445 / 06
M.  Jumanne, 26 Machi 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah:156]

(Imetafsiriwa)

Kwa masikitiko makubwa Hizb ut Tahrir / Tanzania inaomboleza kwa ajili ya mmoja wa wanaharakati wake mahiri na mwanachama aliyejitolea:

Sultan Said
(Mwenyezi Mungu amrehemu)

Marehemu alifariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 25 Machi 2024 M / 15 Ramadhan 1445 H akiwa na umri wa miaka 50, akitumia maisha yake kama mbebaji Da'wah, akifanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida.

Marehemu alikuwa kinara wa amali na shauku katika kubeba Dawah ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Daima alikuwa mkakamavu na mvumilivu katika kukubali mtihani wa maradhi kama qadhaa ya Mwenyezi Mungu, pamoja na kuendelea kuwa na bidii na kujitolea katika Da'wah, kiasi kwamba alikuwa akihudhuria halqa za Hizb na kutoa mchango wa kifedha kwa Hizb hata katika siku zake za mwisho japo afya yake ilizidi kuzorota.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amsamehe na ammiminie rehema kubwa, na amuweke peponi pamoja na Mitume, wakweli, Mashahidi, na watu wema, na hao ndio marafiki wema. Pia tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awatie moyo familia yake kwa subira, uthabiti, na rambirambi njema. Amin.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu