Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  11 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 / 08
M.  Jumapili, 19 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ubepari Hauna Dhamira ya Kuzuia Mimba kwa Wanafunzi

(Imetafsiriwa)

Kufuatia taarifa za karibuni kwamba ndani ya mwezi mmoja takriban wanafunzi 194 wa shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Momba mkoani Songwe (Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania) wamepata ujauzito.

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/wanafunzi-194-momba-wapewa-mimba-ndani-ya-mwezi-mmoja--4624920

Kufuatia kadhia hiyo Hizb ut Tahrir / Tanzania inapenda kueleza yafuatayo:

1. Chini ya nidhamu ovu ya kidemokrasia, jamii ya Tanzania na duniani kote inakumbwa na mporomoko mkubwa wa maadili kutokana na fikra chafu za kisekula za 'uhuru binafsi' kiasi kwamba kila sehemu ya jamii imeathirika. Wazazi huelemewa na mzigo wa ulezi kwa kiasi fulani kutokana na uzembe, lakini sehemu kubwa kutokana na fikra chafu za mfumo wa kibepari ambazo zimeleta maafa na msambaratiko mkubwa wa kijamii.

2. Katika kukabiliana na suala la mimba za wanafunzi, mataifa ya kibepari yanayasukuma mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania katika mwelekeo wa kiupofu ulio kinyume na maumbile, zikilazimishwa nchi hizo maagizo ya ajabu na ya hatari ambayo huhifadhi mfumo wa kibepari, lakini kuipelekea jamii yao katika shimo la maangamizi ya kimaadili. Ubepari huhamasisha na kuchochea huria matamanio ya kingono na hushajiisha uhuru wa kushibisha matamanio hayo, ambapo kimaumbile wakati mwanadamu anapofikia baleghe hutaka kushibisha matamanio hayo. Hata hivyo, suala la ndoa kwa wanafunzi wa kike ni kosa la jinai ambalo huadhibiwa vikali, tena kwa wanaume pekee.

3. Msingi wa hoja inayotumika kwa zuio hilo hudai ‘hali ya kuwa chini ya umri’ kwa wanafunzi wa kike kuolewa. Jambo hilo halina mantiki na haliendani na uhalisia. Inakuwaje aliyechini ya umri kuweza kubeba  ujauzito?

4. Kinachodhihirika katika suala hili, ni kwamba ubepari haupingi hata kidogo wanafunzi wa kike kujihusisha na vitendo vya kingono kwani kwa mujibu wa imani ya mfumo wa kibepari ni sehemu ya ‘uhuru wa mtu binafsi’. Lakini kisichotakiwa na ubepari ni kuwa wanafunzi wasipate ujauzito, na ndiyo maana mfumo huo unatoa na kuhimiza masomo ya elimu ya ngono ili kuwapa wanafunzi mbinu za kuepuka na kuzuia ujauzito.

5. Mtazamo wa Kibepari juu ya suala hili ni aibu ya wazi, ujuha, unaogongana na asili ya mwanadamu. Bali haulindi maadili wala murua wa kibinadamu.

Zaidi ya hayo, inaonyesha wazi kwamba ubepari hauna uwezo hata kidogo wa kumsimamia mwanadamu mambo yake.

Uislamu unatambua uwepo wa hisia ya ndani ya kuendeleza kizazi katika maumbile ya mwanadamu, ambapo makusudio makuu ya hisia hiyo ni kudumisha uwepo wa wanadamu. Ndani ya hisia hiyo  hupatikana raha na starehe (ya ngono) ambazo mwanadamu huhitaji kushibisha nafsi yake. Hata hivyo, Uislamu uko tofauti na ubepari, kamwe hauachi huria huria katika kushibisha matamanio ya kijinsia isipokuwa katika ndoa, ambayo Uislamu unaihimiza mara tu mtu anapofikia baleghe.

Pia, Uislamu unazuia na kuadhibu kwa uadilifu matendo yote ya ngono nje ya ndoa kwa wanaume na wanawake katika kulinda jamii.

Chini ya serikali ya Kiislamu ya Khilafah, jamii itakuwa katika hali ya ubora na utulivu, kinyume na hali ya ubepari leo ambao umeudidimiza ubinadamu katika silika za kinyama kutokana na maadili machafu ya kingono.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu