Afisi ya Habari
Tanzania
H. 28 Jumada II 1446 | Na: 1446 / 07 |
M. Jumatatu, 30 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uchumi wa Kibepari Unasambaratisha Familia na Misingi yake
(Imetafsiriwa)
Warsha ya karibuni ya kinachoitwa ‘usawa wa kijinsia’ iliyofanyika ndani Ngorongoro, Kaskazini mwa Tanzania iliibua suala la uwepo baadhi ya wanandoa kutoka katika jamii za wafugaji ambao wametelekezwa na waume zao walioondoka vijijini kwenda mijini kutafuta kazi, na wakati mwengine waume hao hawarudi katika familia zao.
Hali hiyo si tu imewapelekea wanandoa hao (wanawake) walioachwa vijijini na upweke, taharuki, huzuni na kukata tamaa, bali pia inawalizimisha wanawake hao kubeba majukumu mazito ya kutunza familia majumbani mwao, wakiwa na msaada mdogo kutoka jamii zao. (The Guardian, 27 December 2024)
Kuhusiana na jambo hilo Hizb ut Tahrir Tanzania ina haya ya kusema:
Mbali na uwepo wa taathira za tamaduni za kikabila ambazo hatuwezi kuzipuuza kuwa na kijisehemu kidogo kuhusiana na jambo hilo. Bali sababu msingi ni sera za uchumi wa kibepari ambazo zimepelekea yafuatayo:
1. Kuwepo unyonyaji wa kiuchumi kwa kisingizio cha uwekezaji wa kigeni uliopelekea msingi wa kiuchumi katika vijiji kusambaratika na kubwagika, kwa kuwa nyenzo nyeti za kimaisha kama maeneo ya kulisha mifugo, vyanzo vya maji kama mito hubinafsishwa. Mgogoro wa Mbuga ya Ngorongoro ni mfano hai wa hilo: https://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/2017-01-28-14-59-33/news-comment/22692.htm
2. Maumbile ya mfumo wa kibepari kukosa udhati katika kuwatumikia raia, hivyo nguvu kubwa ya kihuduma hutumiwa kwa kipimo cha kimaslahi, kiasi cha mfumo huo kushughulika zaidi na maeneo ya mijini, kinyume na maeneo ya vijijini ambayo hutelekezwa na kukoseshwa huduma muhimu. Matokeo ya jambo hilo ni kuibuka wimbi kubwa la uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini. Kuwafanya watu wa vijijini kukimbilia mijini kutafuta hali bora.
Hali hizo huwalazimisha watu wa vijijini kutafuta namna nyengine ya kujikimu maisha yao.
Kadhia hii ni miongoni mwa matunda machungu ya mfumo wa kibepari. Hali inayopaswa kuwaamsha wanafikra wakiwemo wanaharakati wa kinachoitwa ‘usawa wa kijinsia’ ambao badala ya kubeba kauli mbiu za kiuwongo za ‘kuinua hali ya wanawake’ na ‘haki sawa’ ambazo huvuruga zaidi nidhamu ya kijamii, wangepaswa wawekeze juhudi zao kuondoa moja kwa moja mfumo wa kibepari kwa mbadala wa mfumo mwengine ambao ni Uislamu.
Mfumo huo wa Uislamu una uwezo wa kukabiliana na matatizo yote ya wanadamu kwa uadilifu na katika msingi wake.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |