Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  24 Sha'aban 1438 Na: 1438 / 04
M.  Jumapili, 21 Mei 2017

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Polisi Nchini Tanzania Wamepiga Marufuku Kongamano la Hizb ut Tahrir la Kuikaribisha Ramadhan

Polisi kwa kiburi wamepiga marufuku kongamano la Hizb ut Tahrir la kuikaribisha Ramadhan ambalo lilikuwa lifanyike mnamo Jumamosi 20 Mei 2017 katika Hoteli ya Mayfair, jijini Dar es Salaam. Polisi walitoa barua ya vitisho kwa hoteli hiyo iliyo andikwa tarehe 19 Mei 2017 ambapo ilikuwa imebakia saa chache tu kabla ya kuanza kwa kongamano hilo. Kisingizio nyuma ya kupigwa marufuku huku kilikuwa ni kwamba kongamano hilo lilidaiwa kuwa mkutano wa siri unaohusisha viashirio vya nia mbaya kwa jamii.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunashangaa, je, kweli mkutano wa siri unaweza kufanyika katika eneo la hotel ambalo linabeba zaidi ya waalikwa 450? Au je, mkutano wa siri kweli utaalika hadharani watu maarufu kadha wa kadha, ikiwemo masheikh, maimamu, wasomi, wanasiasa, waandishi wa habari, mawakili, wanaharakati, nk? Ikiwa hiyo ndio sababu, ni kwa nini barua ya kupiga marufuku kongamano hilo ilitolewa siku moja kabla ya kongamano hilo na kutuarifu sisi saa chache tu kabla ya hafla hiyo?

Kadhia hii pia inafichua udhalimu na ukandamizaji wa nidhamu ya kidemokrasia, kama inavyo dhihirishwa na serikali zake kote ulimwenguni, ambapo zinadai kuenzi ule unaoitwa uhuru wa kuabudu na kujieleza huku kiuhalisia ikiwa ni miito mitupu tu.

Kwa unyenyekevu mkubwa, tunatoa samahani kwa waalikwa wote kutokana na uzito wowote ambao huenda waliupata kutokana na kupigwa marufuku hafla hii muhimu iliyo lenga kugusia kadhia nyeti ikiwemo kufeli kwa nidhamu ya kirasilimali duniani. Vilevile, tunawakumbusha kwa unyenyekevu kuwa hali hii ni ishara waziwazi ya kushindwa, kutofaa na kutostahiki kwa urasilimali na nidhamu yake ya kisiasa ya demokrasia iliyo mnyima mwanadamu kila kitu ikiwemo fursa ya kufanya majadiliano juu ya kadhia nyeti. Wakati uwewadia kwa kila mwenye kutafakari kwa undani kutafiti mfumo mbadala ambao bila shaka ni Uislamu na nidhamu yake ya utawala ya Khilafah.   

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu