Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  26 Shawwal 1441 Na: 1441/02
M.  Jumatano, 17 Juni 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

KAMPENI YA KUTETEA HAKI ZA WAFUNGWA NA DHIDI YA UTEKAJI NYARA

Kutokana na ukweli kwamba wanaharakati watatu wa Hizb ut Tahrir / Tanzania (Ust. Ramadhan Moshi Kakoso, Wazir Suleiman Mkaliaganda na Omar Salum Bumbo) wanazuiliwa bila ya hukumiwa au ridhaa kwa zaidi ya miaka miwili, dhurufu zizo hizo pia zinawakumba wafungwa wengine miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu wa kundi la Uamsho ambao pia wanazuiliwa kwa zaidi ya miaka saba sasa, pamoja na wafungwa wengineo (Waislamu na wasiokuwa Waislamu) wakinyanyaswa katika hali hiyo hiyo, Hizb ut Tahrir / Tanzania ingependa kutangaza uzinduzi wa kampeni maalumu kutetea haki zao.

Kampeni hii itaanza rasmi mnamo 19 Juni 2020 hadi 24 Julai 2020 ikiwa na vipengee vifuatavyo:

1. Malengo ya Kampeni:

a. Lengo jumla

Kulaani na kuzungumza dhidi ya yafuatayo:

• Wafungwa kuzuiliwa bila ya kuhukumiwa

• Wafungwa kunyimwa haki ya ridhaa

• Muda usiojulikana wa uwasilishaji ushahidi

• Kuwepo kwa utekaji nyara

• Sheria ya Ugaidi

b. Lengo maalumu

• Kupaza sauti zetu ili wanaharakati wetu wapewe utaratibu wa kisheria wa kisawa sawa na wa haki kuwezesha kesi zao kusikizwa, kupewa ridhaa au kuachwa huru.

2. Maeneo ya kampeni:

• Darsa za Kiislamu za umma katika sehemu tofauti tofauti.

• Uandishi wa makala, vipindi vya moja kwa moja, video nk. kupitia mitandao ya kijamii kama: Twitter, Facebook, WhatsApp, tovuti nk.

• Kuvisihi vyombo vya habari kama Runinga, Redio, Magazeti kutangaza kwa upana na kuangazia kampeni hii.

• Kutangaza kampeni hii na kuhamasisha wengine kushiriki kikamilifu, kama: mawakili, wasomi, wanaharakati wa haki za kibinadamu, wanachuoni wa Kiislamu, Maimamu wa Misikiti, wahubiri wa Kiislamu, wanahabari, wanasiasa, wanafikra na umma kwa jumla.

• Pia kuhamasisha mashirika ya kijamii hususan yale yanayo shughulika na haki za kibinadamu kutangaza na kushiriki katika kampeni hii.

3. Kauli mbiu ya kampeni

“Ni ukandamizaji chini ya sheria kuzuilia bila ya hukumu, kunyima ridhaa, muda usiojulikana wa uwasilishaji ushahidi na utekaji nyara”

Tunatarajia kwamba kila mmoja katika mujtamaa atashiriki kikamilifu katika kampeni hii tukufu, kwani ajenda yake unajumuisha kila mmoja katika upande wa kidini au wa kibinadamu.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Alama za kampeni

#StopOppressiveLawsAndAbduction (English)

#KomeshaUkandamizajiWaKisheriaNaUtekaji (Swahili)

 

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu