Ijumaa, 19 Rabi' al-thani 1442 | 2020/12/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  30 Safar 1442 Na: 1442/07
M.  Jumamosi, 17 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Nchini Tunisia Inafanya Khiyana na Kuwanyongesha Wale Wanaoikataa
(Imetafsiriwa)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إنَّ مِمَّا أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلَامِ النُّبُوَّةِ الْأُولَى: إذَا لَمْ تَسْتَحِ فَاصْنَعْ مَا شِئْت»

“Hakika, miongoni mwa yale walioyajua watu kutoka katika maneno ya utume wa mwanzo ni: ikiwa huoni haya basi fanya upendavyo.” (Al-Bukhari)

Eneo la usalama katika mkoa wa Kharouba / Nabeul lilimwita mwanachama wa Hizb ut-Tahrir Najmuddin Shuaibin Jumanne Oktoba 13, 2020 M, kufuatia hotuba aliyotoa wakati wa kisimamo kilichoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Tunisia mbele ya Msikiti wa Al-Ghufran huko Hammamet mnamo Ijumaa Oktoba 9, 2020 M, ili kupinga yale makubaliano yanayoitwa Ramani Mipango ya Kijeshi ya Amerika nchini Tunisia, iliyohitimishwa na Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Ibrahim AlBertaji, na kupitishwa na Rais Qais Saeed.

Bila aibu wala haya hata kidogo, vikosi vya usalama vilimhangaisha mwanachama Najmuddin Shuaibin kwa kumhoji juu ya ni kina nani walioandaa kisimamo hicho cha kupinga na ni kina nani walioshiriki ndani yake na ni kina nani walioleta mabango. Badala ya kumuuliza Waziri Mkuu, waziri wake wa ulinzi, na Rais Qais Saeed juu ya khiyana kubwa walioifanya dhidi ya haki ya Waislamu wa Tunisia kusalimisha mipaka yetu, usalama wetu,  jeshi letu na kambi zetu za kijeshi kwa majeshi ya Kikrusedi ambayo yanaficha chuki yenye sumu kali dhidi ya Uislamu na Waislamu, ambao wamemwaga damu za ndugu zetu nchini Iraq na Afghanistan, na bado wanafanya njama dhidi ya ndugu zetu wa Libya na Algeria, badala yake wanawahoji mashababu wenye ikhlasi wa Ummah huu ambao walipaza sauti zao kwa nguvu walipokataa makubaliano haya ya khiyana, na kutoa wito kwa wenye ikhlasi katika usalama na jeshi kuyakataa na kutoyatii. Kwani hakika yake, Wallahi, ni moja katika fitna kuu!!!

Sisi katika Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Tunisia tunathibitisha kwamba mbinu hizo duni ambazo zinatukumbusha polisi wa kisiasa wa Rais aliyeng'olewa Ben Ali hazitatuzuia kuendelea na mapambano yetu ya kisiasa dhidi ya watawala wasaliti na mabwana zao katika majeshi ya kikoloni. Na tunatoa wito kwa watu wetu nchini Tunisia, haswa watu wenye nguvu na ulinzi, kuchukua kutoka mikononi mwa watawala hawa ambao wameisaliti ardhi na heshima, kuwaudhi vipenzi (auliyaa) wa Mwenyezi Mungu, wakaacha njia ya Mwenyezi Mungu, na wakashinikiza uovu, na wala hakuna kinachofaa kwao ila kuondoshwa na kung'olewa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu