Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  5 Rabi' II 1442 Na: 1442/19
M.  Ijumaa, 20 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Familia ya Kiislamu Imeimarishwa na Haihitaji Makubaliano Yanayodai Kheri na Kuleta Maafa

(Imetafsiriwa)

Lile linaloitwa Baraza Ulaya la Kuzuia na Kupambana na Unyanyasaji dhidi ya Wanawake na Ukatili wa Kinyumbani lilihitimisha makubaliano yanayojulikana kama "Makubaliano ya Istanbul" na kufungua mlango wa kutiwa kwake saini mnamo 11 Mei 2011 jijini Istanbul, Uturuki, likikuuza kwamba makubaliano haya ni makubaliano dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake na yanakusudia kuzuia unyanyasaji na kulinda wahasiriwa na "Kukomesha kutoadhibiwa kwa wahusika wa uhalifu huu."

Kufuatia majibu ya hivi karibuni ya Kamati ya Mawaziri ya Baraza la Ulaya kwa ombi lililotolewa na Tunisia kuialika ili ijiunge na makubaliano hayo, hakika sisi katika kitengo cha wanawake wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia:

1- Tunatangaza kuzinduliwa kwa kampeni kwa anwani "Familia ya Kiislamu imeimarishwa na haihitaji makubaliano ambayo yanadai kheri na kunaleta maafa", dhidi ya kutia saini Tunisia kwa Makubaliano ya Istanbul.

2- Tunakumbusha kwamba makubaliano haya ni nyongeza ya makubaliano ya maafa ya hapo awali kama "CEDAW" na "Geneva".

3- Tunabainisha kuwa hatari ya makubaliano haya iko katika kujitolea kutia saini vifungu vyake vyote bila ya masharti, licha ya ukweli kwamba yanajumuisha vipengee vya hatari mno, ambavyyo ni kama ifuatavyo:

Katiba: kwa kuvijumuisha katika katiba.

Utungaji sheria: kwa kufutilia mbali sheria zote zilizotangulia ambazo zinahitilafiana navyo.

Kielimu: kujumuishwa kwa kanuni za Makubaliano (zenye kuwakilishwa na usawa kamili kati ya wanaume na wanawake, dori zisizo za kimapenzi ya kijinsia na kupambana na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ...) katika mtaala rasmi wa elimu.

4- Tunachukulia kuwa utiaji saini makubaliano haya kunazidisha mgogoro wa ukosefu wa uhuru wa uamuzi wa kisiasa katika nchi yetu, na kuhalalisha uingiliaji wa kigeni katika maswala ya ndani ya nchi, haswa kwamba kutia saini makubaliano haya kutawaidhinisha kufuatilia nchi yetu na kuihisabu kwa kuhalifu vipengee vyake vyovyote, katika ukiukaji wazi wa ubwana serikali hii na matakwa ya watu ambayo yatupiliwa mbali kulingana na makubaliano haya batili na yasiyo ya haki yenye kutumikia maslahi ya mkoloni.

5- Tunaonya juu ya hatari ya kutia saini makubaliano haya juu ya umoja na utulivu wa familia ya Kiislamu ambayo itakuwa ni mfano wa kuigwa kwa familia ya Kimagharibi iliyosambaratika na kutawanyika iliyosimama juu maana ya maslahi na uhuru kamili.

Kwa hivyo, sisi katika kitengo cha wanawake cha Hizb ut-Tahrir katika Wilayah ya Tunisia tunatangaza kwamba tutakabiliana na jaribio lolote linalolenga kuivunja na kuiangamiza familia ya Kiislamu. Tunatoa wito kwa Waislamu walio huru kusimama kama kizuizi kisichoingilika mbele ya kutofaulu kwa serikali, ambayo ina hamu ya kutia saini kila makubaliano ili kuiridhisha Magharibi licha ya kupingana kikamilifu na sheria ya Kiislamu.

Na tunakariri wito wetu kwa watu wenye akili, busara na ikhlasi miongoni mwa watu wenye nguvu na uthabiti kutetea heshima yetu na kuokoa familia ya Kiislamu kutokana na makucha ya usekula; Kwa kuipa Nusra Hizb ut-Tahrir kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ وَمَنْ يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ مَا زَكَى مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ أَبَداً وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يُزَكِّي مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿

"Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua." [An-Nur: 21]

Ustadha Hanan al-Khamiri

Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu