Jumanne, 29 Sha'aban 1444 | 2023/03/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  23 Jumada I 1444 Na: 1444/11
M.  Jumamosi, 17 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukamatwa kwa ajili ya "Sarakasi za Uchaguzi"
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari chini ya kichwa: "Licha ya Udanganyifu wa duara za Magharibi na sarakasi ya uchaguzi wa wabunge...mapinduzi ya Umma yanaendelea kusimamisha Khilafah ya Kiislamu", ambapo ilithibitisha kwamba mfumo ambao watu waliasi dhidi yake mnamo tarehe 17 Disemba 2010 ulikuwa ni mfumo wa kisekula mfuasi wa Magharibi, ambapo ilielezea uchaguzi wa wabunge unaoendelea kama "sarakasi" na kwamba ni sura mpya katika sura za njama dhidi ya Watu wa Tunisia, na kuonya ndani yake juu ya hatari ya njia ambayo Rais Kais Saied anafuata, kuanzia kwa kushirikiana na Ufaransa na kuunga mkono utawala wa Magharibi juu ya nchi yetu, kulinda mfumo wa kisekula wa Magharibi, na kuutoa Uislamu kutoka kwa Utawala na sheria.

Tangu mwanzoni mwa wiki hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia walizindua kampeni ya kusambaza taarifa hiyo, ambapo Shab, Muhammad Amin al-Dabibi, alikamatwa mnamo Alhamisi, Disemba 15, na kikosi cha polisi cha mahakama katika nyumba ya Tamim, ambapo bado ni siri kuhusu mahali pa kukamatwa kwake, na alihamishiwa kushtakiwa kwa mashtaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri!

Mnamo Ijumaa, tarehe 16 Disemba, Shab Zuhair Abdullah, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alikamatwa katika mji wa Sidi Bouzid, chimbuko la mapinduzi, kwa tuhuma za "kusambaza taarifa na kutoa hotuba juu ya suala hilo"! Anaendelea kuzuiliwa bila kufahamishwa kukamatwa kwake.

Kuhusu kukamatwa huku, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya Tunisia tunasema yafuatayo:

1- Tunamkumbusha Rais wa Nchi kwamba hitaji kuu la mapinduzi lilikuwa ni kupinduliwa kwa utawala, na kwamba kukamatwa kwa wale wanaotoa kauli mbiu hii na kuwakumbusha wananchi juu ya hitaji la mabadiliko makubwa kwa misingi ya imani yao ya Kiislamu ni usaliti wa mapinduzi na kutoyatimiza.

2- Kukamatwa kwa Mashababu hao wakisambaza taarifa ya kisiasa ni kashfa ya dola ambayo inathibitisha kutokuwa na mshikamano wa waliohusika nayo na kufichua uongo wa madai yao ya kushikamana na udhibiti wa kikatiba na kisheria wanaouweka mikononi mwao.

Hata hivyo, inaonekana kuwa taarifa hiyo iliyotolewa na hizb iliwatia wasiwasi wakaazi wa balozi, hivyo kuagiza tabaka tawala (ambalo limegubikwa na mizozo yake) kuhamasisha baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata Mashababu hao ili kuivuruga hizb na kupunguza sauti yake au kuinyamazisha, jambo ambalo linathibitisha uongo wa madai ya mara kwa mara ya rais kwamba hakuna aliyekamatwa na hatakamatwa kwa sababu ya maoni yake!

3- Kukamatwa huku mara kwa mara kunathibitishwa na mamlaka ya baada ya Julai 25, kufuatia mwelekeo wa utawala uliopita wenyewe katika kukabiliana na Hizb ut Tahrir, na kutoweza kwake kupambana hoja kwa hoja na kukabiliana fikra kwa fikra. Badala yake, tunaona kwamba inazalisha tena mbinu ya dola ya kipolisi ya vitisho, uvamizi na mashambulizi ya nyumba, kana kwamba iko mbioni dhidi ya wakati kuregesha udikteta na kuvifanya vikosi vya usalama kuwa fimbo kubwa tu ya kuwalenga wasomi na wanamaoni wanaowaonyesha watu ukweli wa serikali hii fisadi, na kwamba mgogoro huo ni wa kina zaidi kuliko kuupunguza hadi kuwa mapambano tasa juu ya viti vya madaraka, lakini ni mgogoro wa utawala fisadi ambao ulikusudiwa kuendana na ukoloni na vibaraka wake, na kutengwa Uislamu kutoka kwa utawala, sheria, na mwenendo wa mahusiano ya watu.

Kwa kumalizia, tunathibitisha kwamba Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia walikabiliana na serikali za Bourguiba na Ben Ali, na hawarudishwa  nyuma na kukamatwa au magereza, na leo wamejitolea zaidi kuupindua utawala wa Magharibi, mfumo wake wa sheria, na zana zake za ndani, na kusimamisha utawala wa haki juu ya msingi wa Uislamu, na haitaathiri azma yao kwenye jela za madhalimu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(يُرِيدُونَ أَنْ يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلا أَنْ يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ)

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [At-Tawbah:32].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu