Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 7 Rabi' I 1445 | Na: 1445/10 |
M. Ijumaa, 22 Septemba 2023 |
Tangazo kwa Vyombo vya Habari
Kukamatwa kwa Ustadh Khaled al-Loumi, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, huko Sfax Ikiwa huu sio ukamatwaji wa kisiasa, basi ni nini?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatano, Septemba 20, 2023, Kitengo cha Utafiti na Ukaguzi huko SFAX kilimkamata mwanachama mmoja wa Hizb ut Tahrir, ndugu Khaled al-Loumi. Alipokea wito kutoka kwa kitengo kilichotajwa hapo juu na alikataliwa uwepo wa wakili wake wakati wa wito huo. Sababu iliyotolewa ni kwamba kazi yao na Ustadh Khaled ilikuwa tu utaratibu wa ushauri. Kuhojiwa kwake kuliendelea kutoka 10:00 asubuhi hadi 5:00 jioni. Wakili wake alipouliza juu ya hili, maafisa wa kitengo hiccho walijibu kwamba wataandaa ripoti mpya, wakimshtaki kwa "tuhma za ugaidi," na kwamba watamfunga kwa angalau masaa 48.
Kutokana na hili, afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia inatangaza yafuatayo:
1. Tungependa kumkumbusha kila mtu kwamba Ndugu Khaled Al-Loumi ni mtu anayejulikana vyema katika eneo lake, na mamlaka za usalama zinajua kuwa anahusishwa na Hizb ut Tahrir kama mmoja wa wanachama wake. Je! Ni nini kusudio la kumtuhumu kwa uwongo kwa "tuhuma za ugaidi"? Ikumbukwe kwamba mtu huyu ana umri wa zaidi ya miaka sitini, ana matatizo ya moyo, na amepitia upasuaji kadhaa. Ikiwa huu sio ukamatwaji wa kisiasa, basi ni nini?!
2. Kwa kuongezea, inadhihirika kuwa sera ya kuwaandama mashababu wa Hizb ut Tahrir na ukamataji wa kiholela unaowalenga unatumika kama huduma ya wazi kwa ajenda za kisiasa zenye lengo la kuzuia Hizb ut Tahrir na ulinganizi wake. Kutokana na hayo, Ndugu Khaled Al-Loumi amekamatwa, kudhulumiwa, na kushtakiwa kwa uwongo - yote kwa maoni yake, haswa kutokana na hali yake ya kiafya.
3. Mashtaka ya uzushi dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir na kukamatwa kwao mara kwa mara ni hatua za kisiasa zinazolenga kutishia umma kutokana na Hizb. Vitendo hivi vimekusudiwa kuitengana hizb, kuzuia watu wa Tunisia kupinga ukoloni na washirika wake, na kuzuia juhudi zao za kurejesha maisha kwa mujibu wa kanuni za Uislamu.
4. Tunalaani vikali ukamataji huu na kuuona usio wa haki na kinyume na Uislamu. Hizb ut Tahrir, popote ilipo, ikiwemo nchi yetu Tunisia, inafanya kazi kuinua neno la Mwenyezi Mungu na kunyanyua heshima ya Uislamu na Waislamu kwa kufufua maisha ya Kiislamu kupitia utabikishaji wa Sharia ya Kiislamu chini ya kivuli cha Al-Khilafah.
Hizb inabaki kuwa thabiti katika kujitolea kwake kutabanni njia ya Mtume Muhammad (saw) katika kulingania Uislamu, bila kupotoka hata kwa upana wa unywele. Inapinga vurugu, inalaani, na inazichukulia kuwa Haram. Tunasisitiza kwamba ukamataji kama huu sio kitu zaidi ya lango ambalo linaruhusu wana usalama kuzua mashtaka ya kisheria katika huduma ya vyombo kandamizi vya kisiasa vyenye nia mbaya.
Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia, tunadai kuachiliwa huru mara moja kwa Ndugu Khaled Al-Loumi na kukomeshwa kwa ukamatwaji wa kisiasa kwa Mashababu wa Hizb ili waweze kuendelea na kazi yao katika kuhudumia Uislamu na Waislamu kote ulimwenguni, ikiwemo Tunisia. Walikabiliwa na kukamatwa na kifungo chini ya serikali za Bourguiba na Ben Ali, na wala kukamatwa au magereza hakutawazuia. Leo, wanasalia kuwa na azma zaidi kuliko hapo awali kupindua utawala wa Magharibi, mfumo wake wa kisheria, vyombo vyake vya ndani, na kusimamisha sheria ongofu iliyojengwa juu ya Uislamu. Uchochezi wa waovu na magereza ya madhalimu hayatadhoofisha azma yao.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[يُرِيدُونَ أَنْ يُطْفِئُوا نُورَ اللهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللهُ إِلا أَنْ يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [At-Tawba: 32].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |