Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  11 Rajab 1445 Na: 1445/21
M.  Jumanne, 23 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Chombo cha Usalama huko Kerkennah Kinawafuatilia Wanaotafuta Kuwaokoa Watu Wetu huko Gaza Wakitoa Wito kwa Majeshi Kuwanusuru, Na Kuwachukulia kuwa ni Washukiwa wa Uhalifu Wanaostahili Kuchunguzwa na Kukamatwa!!
(Imetafsiriwa)

Huku Gaza ikiungua mikononi mwa umbile halifu la Kiyahudi, na wanawake na watoto wakikatwa vipande vipande kikatili, katika kimya kamili kutoka kwa tawala za Kiarabu zinazosaliti na shirikishi, katika wakati ambapo Palestina; Isra na Mi’raj, Ardhi Iliyobarikiwa, cha kwanza kati ya vibla viwili, inalilia majeshi ya Waislamu kwa ajili ya hatua ya haraka kukomesha uhalifu wa mauaji ya halaiki ambao haukomi.

Kufuatia hatua ya moja ya timu za ulinzi katika kisiwa cha Kerkennah, mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 19/1/2024, kumkamata Ndugu Fathi Arous kutoka nyumbani kwake, baada ya kutoa hotuba siku hiyo mbele ya Msikiti wa Al Jazeera katika eneo la Al-Ataya kuhusu ulazima wa kuinusuru Gaza na watu wake, wanachama wa Hizb ut Tahrir walioshiriki katika maandamano waliitwa, nao walikuwa: Naji Youssef, Abdel Latif Warda, Moez Al-Samit, Farah Farhat, na Mohammad Abdel Razzaq. Walionekana jana, Jumatatu, 22/1/2024, kabla ya uchunguzi huko Kerkennah, ambao uliamua kubakia nao na wakahamishiwa hadi Sfax.

Ni ajabu leo kwamba chombo hiki cha usalama cha Kerkennah kiliharakisha kuwakamata wanachama hawa na kuwafuatilia wengine, bila sababu yoyote ya wazi au kisingizio!

Inashangaza kwamba mamlaka iliyopo nchini Tunisia inayodai kusimama na watu wa Gaza, imenyamaza kimya kuhusu ukiukwaji huo wa mara kwa mara dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir, badala ya kuunga mkono hatua zao za kutafuta nusra kutoka kwa majeshi kwa kuwahamasisha kuhami heshima yetu, ambayo inakiukwa na umbile la adui ambalo lilitupiga kwa bomu huko Hammam al-Shatt mnamo 1985. Kisha likarudi mnamo 2016 kuzunguka katika mitaa yetu kutoka Tunisia hadi Sfax kumuua mhandisi wa ndege Muhammad Al-Zawari, Mwenyezi Mungu amrehemu. Kisha linatoka bila kudhurika kujisifu kwa ulimwengu juu ya uhalifu wake, na hili hapa leo, linaendelea na mauaji na uharibifu huko Palestina!!

Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, tunawahutubia watu wetu nchini Tunisia, hasa wale wenye nguvu, na kueleza:

Hatukuandika taarifa hii kwa ajili ya kulalamika au kutafuta huruma, kwa maana huu si wakati wa kulalamika, bali ni wakati wa kuwa makini, wakati wa kukomesha mambo haya yote, wakati ni kukomesha udhalilifu huu, kukukuta vumbi la unyonge na udhalilifu, na kuvunja minyororo kutoka kwa makufuli ya kambi za jeshi ili majeshi ya Kiislamu yaliyofungiwa, likiwemo jeshi la Tunisia, yaweze kutoka, na kutekeleza wajibu wao wa kuiokoa Palestina na watu wake.

Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wenu, wala hatakuangusheni, na kumbukeni kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu