Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  28 Rabi' I 1444 Na: 05 / 1444
M.  Jumatatu, 24 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maandamano ya Pegida; Chombo Chengine tena Kinachotumiwa Kuhalalisha Chuki Dhidi ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Pegida (kundi la wazungu wazalendo dhidi ya kuenea kwa Uislamu Ulaya) lilitakiwa kuandamana mnamo Jumamosi, tarehe 22 Oktoba 2022, katika eneo la Stationsplein karibu na kituo cha Rotterdam Central ambapo walipanga kuteketeza Qur’an. Mnamo Jumapili, tarehe 23 Oktoba, waliandaa pia kuteketeza Qur’an. Manispaa ya Rotterdam, pamoja na The Hague, ziliwapa Pegida ruhusa ya kuandaa maandamano yao. Idadi kubwa ya vyama katika mabaraza ya jiji ambayo tayari yalitarajia kutopiga marufuku mkusanyiko kwa sababu, machoni pao, haki ya kuandamana ni "takatifu".

Mnamo Jumamosi na vile vile Jumapili kiongozi wa kundi la Pegida, Edwin Wagensveld, alikamatwa na polisi. Jumamosi, Pegida lilikuwepo pamoja na wafuasi wachache "wajasiri" wa Pegida. Baadhi ya watu 150 walifika kwenye maandamano ya kupinga. Siku zote mbili hatimaye polisi walichukua Qur’an zote zilizokuwepo ili kuzuia zisiunguzwe, sababu ni kwamba uchomaji moto hadharani hauruhusiwi. Licha ya nia ya wazi ya Wagensveld ya kuteketeza Qur’an, maandamano yaliruhusiwa kuendelea.

Kampeni za chuki za Pegida, zilizo na lengo la kuvunja mapenzi kwa Qur'an na kuhalalisha chuki dhidi ya Uislamu hazikutokea tu kwenye ombwe. Sera ya chuki dhidi ya Uislamu ya vyama vya kisiasa imekuwa wazi zaidi katika miongo iliyopita na sera hii imeibua na kulilisha zimwi lenye siasa kali la mrengo wa kulia. Leo, chombo hiki cha Magharibi chini ya pazia la uhuru wa kuzungumza na maandamano, kinaonyesha uadui wa wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa lengo la kumlazimisha Muislamu kujioanisha na kuvunja utiifu kwa Uislamu na nembo zake.

Pindi tutakapohalalisha kampeni kama hizi kwa sababu tunakubali haki ya kuandamana, Magharibi itakuwa imeshinda. Haikubaliki kabisa kuhalalisha vitu kama hivyo kwa msingi wa uwongo kwamba haviwezi kuathiri hadhi ya Qur’an na nembo zengine za Kiislamu. Swali lililopo hapa, ni wajibu wetu kusimama kwa ajili ya Uislamu na kupeleka ujumbe wa wazi kwa mujtamaa. Athari ya kukubalika kwa vitendo kama hivi vya matusi ni kwamba inakuwa rahisi kudhihirisha hata aina kali zaidi za matusi. Wanawataka Waislamu nchini Uholanzi kukubali matusi hayo kama wanavyojaribu kuwafanya Waislamu kukubali propaganda za LHBTI+.

Enyi Waislamu msivumilie matusi kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), Qur'an au nembo zozote za Uislamu. Wao ni vipenzi zaidi kwetu kuliko nafsi zetu, kamwe hatutakubali kwamba Ujumbe wa Wahyi udhihakiwe, uwe kitovu cha dhihaka. Je, hili linachangia vipi kwa mujtamaa unaojumuisha jamii tofauti taofati? Hivyo basi sisi, kama Waislamu na tuulinganie na kuulinda Uislamu wetu kwa fahari ili Mwenyezi Mungu atupe heshima na hadhi duniani na akhera.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu