Afisi ya Habari
Uholanzi
| H. 17 Rabi' II 1447 | Na: 03 / 1447 |
| M. Alhamisi, 09 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Amali” kama Pazia la Ukaliaji wa Kimabavu
(Imetafsiriwa)
Yale yanayoitwa makubaliano kati ya dola vamizi “Israel” na Hamas, yaliyopangwa na Washington, yanawasilishwa katika vyombo vya habari vya Magharibi na kwa masikitiko pia katika sehemu za ulimwengu wa Kiislamu kama hatua kuelekea amani. Kiulisia, si kitu chengine ila ni marudio ya mtindo wa zamani: mradi wa kikoloni “Israel” unaimarishwa na kulindwa zaidi, huku jinai zake zikifinikwa na vazi la “amani.”
Maneno kama vile “kusitisha mapigano” na “msaada wa kibinadamu” yanasikika kama upatanishi, lakini kiuhalisa ni ala ya kejeli. Kwani mtu anawezaje kuzungumzia misaada, huku dola hizo hizo zinazopanga misafara ya misaada zikiwa zile zile zinazotoa mabomu na pazia la kidiplomasia ambalo Gaza imeangamizwa nalo? Je, kusitisha mapigano kunawezaje kuaminiwa, wakati “Israel” imekiuka makubaliano mara kwa mara kila inapofaa maslahi yake?
Historia iko wazi: miongo kadhaa ya kufukuzwa, adhabu za pamoja, na mauaji ya halaiki yaliyofanywa na “Israel,” yanayoungwa mkono na Amerika, Magharibi, na tawala dhalimu katika ardhi za Waislamu. Haki au fidia haijawahi kutolewa kwa watu wa Palestina, na makubaliano haya hayatakuwa tofauti. Mtindo huo huo ulionekana mapema Iraq, Syria, Afghanistan, Libya, Sudan, na nchi zengine nyingi za Kiislamu: nchi zinaangamizwa chini ya pazia la amani na utulivu, lakini kiuhalisia zinakabidhiwa kwa uvamizi, mgawanyiko, na machafuko.
Hivyo, mtu anabaki amenaswa katika mzunguko mbaya: makubaliano ya muda yanayonadiwa kama “amani,” lakini ambayo kuhalisia yanaimarisha uvamizi zaidi. “Israel” inapata muda, uhalali, na usalama, huku Wapalestina wakiachwa na vikwazo, udhalilifu, na ahadi zilizovunjwa.
“Amani” ya kweli kamwe haitapatikana maadamu dhulma kuu: uvamizi wa kikoloni wa Palestina, inaendelea kuwepo. Suluhisho pekee la kweli liko katika kurudi kwa Palestina kama sehemu ya Khilafah, huku Waislamu wakiungana chini ya Khalifa mmoja anayetetea maslahi ya Ummah na kukomesha mradi wa kikoloni mara moja. Maadamu mkandamizaji analipwa ujira na wanaokandamizwa wanahimizwa kuwa na subira, Palestina itaendelea kusalitiwa kwa jina la “amani” ambayo kiuhalisia si chochote zaidi ya uvamizi katika pazia jipya.
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uholanzi |
Address & Website Tel: 0031 (0) 611860521 www.hizb-ut-tahrir.nl |
Fax: 0031 (0) 611860521 E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl |



