Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  17 Safar 1442 Na: 1442 H / 03
M.  Jumapili, 04 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tishio la Urasilimali kwa Wanadamu
Mfumo wa Kisekula Umefichuka; Uislamu Ndio Badali ya Kweli

Tunaishi katika zama ambazo uongo, habari potofu na tuhma zisizo na msingi ni jambo kawaida kabisa, na marais, mawaziri wakuu na vyombo vikuu vya habari hunadi batili hii kila siku bila ya aibu.

Tangu mwanzoni mwa karne hii viongozi wa kirasilimali na maafisa wa benki wamefichuliwa kwa ujasusi wa uongo na mipango ya khiyana ya kifedha, na kusababisha vita haramu na mgogoro wa kifedha wa kiulimwengu. Hivi majuzi London imeibuka kama mji mkuu wa utapeli wa pesa ulimwenguni, huku kila mahali kwengine ikibidi kupate shida ya ubwana wa mfumo ambao unapendelea kipote cha matajiri wachache kuliko kila mtu mwingine yeyote.

Jibu la kukabiliana na janga la virusi vya Korona limekuwa darasa la juu katika uhadaifu na udanganyifu. Watu wa kawaida wanaanza kugundua kile ambacho mateso  yanatokana nacho kwa kuwa na viongozi wasiowajibika wenye ajenda za kujitumikia wenyewe, ambao hutumia janga hili la maambukizi kuficha miongo kadhaa ya mapuuza na kuendelea kwa matumizi mabaya ya mamlaka.

Warasilimali hawaamini kufuata sheria; badala yake sheria ni kwa watu wengine wasio na bahati kuzifuata. Johnson anatishia kuvunja mikataba iliyotiwa saini ya kimataifa, na Trump anatishia kwamba hakutakuwa na mpito wa amani wa mamlaka ikiwa atashindwa uchaguzi wa Novemba. Mfumo wa kati ya "walio nacho" na "wasio nacho" unauchukua ulimwengu mzima katika safari ya mateso hadi ukingoni mwa maangamivu, ukiligonganisha kundi moja dhidi ya jengine, ili "walio nacho" waweze kuwa na hata zaidi.

Haishangazi kwamba kuna ongezeko la mgawanyiko miongoni mwa watu na uhasama wa wazi kwa wageni na wahamiaji. Urasilimali ni dhahiri unafeli kila mahali, na viongozi wake maarufu wanajaribu sana kununua wakati, wakitafuta wa kumlaumu kwa lawama zao kongwe, hata hivyo haiwezekani. Kwa kweli, Macron nchini Ufaransa anatangaza kwamba anahisi kutishiwa na Uislamu, na kuutuhumu Uislamu kuwa ndio tatizo.

Ushirika wa serikali na vyombo vya habari umewapotosha watu, kiasi kwamba zaidi ya nusu ya wanachama wa chama cha Conservative cha Uingereza wanaamini uongo kwamba Uingereza ina "maeneo isiyoweza kwenda" ambako Shariah inatawala na wasio Waislamu hawawezi kuingia. Kinaya ni, idadi kubwa ilidai kwamba walihisi kutishiwa na Uislamu kwani "dini hii huzaa kutovumiliana."

Ubwana wa kirasilimali unamalizika. Mwenyezi Mungu Mtukufu amefichua kushindwa kwao ambako kuko dhahiri kwa kila mwenye macho. Ghafla kuna mazungumzo mengi juu ya mfumo mbadala; kiasi kwamba serikali ya Uingereza inajaribu kupiga marufuku fasihi inayoukosoa Urasilimali katika madarasa ya shule.

Sasa ndio fursa kwa Waislamu kuuwasilisha Uislamu ulimwenguni ili kuonyesha mfumo wake adilifu kwa watu wote, masuluhisho yaake ya kina ya kiuchumi, na amani na usalama ambayo ni mfumo tu ulioteremshwa na Muumba pekee, unaoridhisha moyo na akili, unaweza kuleta.

Tunakualika mujisajili na mujiunge na Hizb ut Tahrir / Uingereza kwa kongamano lake la kimataifa la mtandaoni: Kurudi kwa Mfumo wa Kiulimwengu wa Kiislamu.

Wazungumzaji watahutubu mada zifuatazo:

Kutoka kwa Janga la Maambukizi hadi BLM: WanadamuWanatafuta Badali kwa Hamu

Uchumi Mpya, Usiohudumia Asilimia Moja Pekee

Nidhamu ya Khilafah, Utunzaji wa Watu

Kuasisi Uongozi wa Uislamu Duniani na Wajibu wetu

Jumamosi, 31 Octoba 2:00pm GMT

Jisajili katika

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu