Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  14 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 H / 10
M.  Jumatatu, 13 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watetezi wa Uhuru wa Kuzungumza Hawana Mguu wa Kusimamia

 (Imetafsiriwa)

Licha ya Waislamu wote kuwa wahanga wa matamshi ya chuki dhidi ya Mtume (saw) na maswahaba zake (Mwenyezi Mungu awawiye radhi wote), masekula sugu katika serikali ya Uingereza na vyombo vya habari wamegeuka na kuwatuhumu Waislamu, kwa mara nyingine tena kwa kutishia uhuru wa kuzungumza. Wazo lenyewe la uhuru wa kuzungumza limejaa mikanganyiko kiasi kwamba haishangazi kwamba mabingwa wake hawawezi kutoa hoja za msingi katika utetezi wake. Badala yake, wana uwezo wa kujumuisha tu hoja chache dhaifu za kihisia, kama vile jinsi Waislamu wanavyopaswa kuwashukuru wakoloni wao ambao ni wapole kwao kuliko vile tawala za Saudia au Afghanistan zingekuwa. Hoja nyingine ya ‘kifikra isiyoeleweka’ iliyotumika kutetea hasira zao ni kwamba kuzikubali hisia za Waislamu kuhusu matusi kwa msingi wa Dini yetu, kutapelekea takriban kauli zote kupigwa marufuku. Kwa hivyo mtu atachora mstari wapi?

Hata hivyo katika uhalisia mstari unachorwa; na masekula wanaochukua manufaa kama vipimo vyao. Migongano ambayo ni dhahiri kwa Waislamu wote, ilhali masekula wanaonekana kuwa vipofu kwayo, inayotokana na kutofautiana kwa maslahi ya kipote cha masekula na Waislamu wa kawaida. Kwa hakika, maslahi ya raia wa kawaida katika nchi za Magharibi ni vigumu kukabiliana na yale ya kipote cha mabwana zao, lakini kinaya ni kuwa jaribio lolote la kuonyesha mwanya huu hukabiliwa na vikwazo vikali kwenye usemi kama huo. Sheria inatumika na zaidi inaandikwa ili kubana na kupiga marufuku kila aina ya usemi unaokwenda kinyume na maslahi ya kipote cha mabepari wachache, ilhali uhuru wa kutukana na kudunisha Uislamu na Waislamu ni jambo la ajabu la kipekee, licha ya kuwa ni ovu na la chuki katika tabia na motisha.

Ni kana kwamba mtu yuko huru kuzungumza, isipokuwa ikiwa anayezungumza ni Muislamu, anayeangazia migongano katika nadharia na utekelezaji wa uhuru wa kujieleza katika nchi za Magharibi.

Uhuru wa kutukana sio sifa ya maendeleo ya hadhara iliyoendelea, bali ni matokeo duni ya mfumo usio na uwezo wa kudhibiti tofauti. Usekula hauna vipimo vya kuamua nini kinapaswa kusemwa na kitosemwa, kwa hivyo unategemea mchakato wa kidemokrasia kuruhusu mtazamo mmoja kutawala na kukandamiza mengine yote, kwa sababu tu una kundi kubwa la wafuasi (waliodanganywa au vyenginevyo) katika siku yoyote.

Waislamu hawapaswi kuunga mkono dhana ya wengi watawale inayofumbatwa ndani ya demokrasia, wala hatupaswi kutetea dhana iliyofeli ya uhuru wa kuzungumza. Waislamu ni waumini wa haki na hawapaswi kuona haya kuitangaza na kuilingania maadili yake yenye heshima. Uislamu hauhitaji kuthibitishwa na mfumo wa kisekula uliofilisika kifikra; thaqafa tukufu ya Kiislamu inajieleza yenyewe kama shahidi wa utawala wake juu ya fikra na mifumo mengine zote.

 [هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [As-Saff 61:9]

Yahya Nisbet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir

Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu