Afisi ya Habari
Uingereza
H. 18 Dhu al-Hijjah 1443 | Na: 1443 H / 12 |
M. Jumapili, 17 Julai 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutoka Al-Hind hadi Al-Quds - Simamisheni Khilafah - Komesheni Ukandamizaji
(Imetafsiriwa)
Makongamano yote mawili yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Uingereza wikendi hii yalifanywa kwa ufanisi katika ukumbi uliojaa na mapema. Ujumbe mkuu na wito wa kuchukua hatua ni kwa Waislamu kukataa usawazishaji wote wa mahusiano na mikataba inayofanywa pamoja na serikali ya Hindutva na Kizayuni ambazo zinakanyaga haki za kimsingi za Waislamu kila uchao. Waislamu hawana budi kukataza munkar (uovu) huu mkubwa wa zama zetu, ambapo uovu kama huu unaweza kufanywa chini ya pua za watawala wa nchi za Kiislamu, ambao hawathubutu hata kuinua kidole kuwazuia. Sawia na wajibu huu ni kazi ya kuamrisha mema ya kuyakumbusha majeshi ya Kiislamu kwamba kazi yao kwanza ni kuulinda Ummah kutokana na mashambulizi kama hayo na sio kuwa tu kama majeshi sanafu, au usalama wa kibinafsi kwa watawala wasaliti. Hatimaye, ma’ruf (wema) mkubwa zaidi ni kujijenga kinguvu na kueneza kadhia ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume.
Wazungumzaji walizungumza juu ya hatari ya utaifa. Mazhar Khan aliuita "saratani katika jamii za wanadamu", na akaeleza kuwa si chochote chini ya uhalifu wa kiburi cha Iblis, ambapo upande mmoja unasema wao ni bora au wanastahili zaidi kuliko mwengine. Uovu kama huu umewahamisha mamilioni ya watu na kusababisha mauaji ya maelfu, kutoka al-Hind hadi al-Quds. Hindutva na Uzayuni zote mbili ni itikadi za kisekula za kitaifa, zisizo na msingi katika dini. Waislamu lazima wakatae migawanyiko yoyote ya kikabila, kimbari au kitaifa [ [وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ صِبْغَةً وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ “na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.” [Al-Baqarah (2):138].
Rupon Shahid alijadili jinsi Uislamu ulivyokuja katika karne ya saba kwa watu waliogawanyika kabisa, lakini ukawaunganisha na kuwanyanyua hadi kuwa umma bora ulioletwa kwa wanadamu. Uislamu ulipotabikishwa kama Dola ya Kiislamu, hapo ndipo historia ilijaa mifano ya jinsi raia wasiokuwa Waislamu walivyolindwa na kupewa fursa za kustawi. Hii ni kinyume kabisa na itikadi ya Hindutva, Uzayuni na hata mfumo wa Kimagharibi unaokandamiza na kuwadhulumu watu wachache mara kwa mara. Mifumo kama hii inawafelisha watu wote wawe wachache au wengi, na hutumia mgawanyiko huo kuwavuruga watu huku kipote cha mabepari wachache wakipora nchi kwa ajili ya kujinufaisha ulafi wao wenyewe.
Dkt Nazreen Nawaz, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir alieleza jinsi eneo la Magharibi mwa India lilivyofunguliwa kwa uadilifu wa Uislamu kutokana na ukandamizaji wa Mfalme wa Kibaniani Raja Dahir ambaye aliwafunga baadhi ya wanawake Waislamu. katika karne ya nane. Muhammad bin Qasim alitumwa kutoka Damascus kuwaokoa. Heshima ya wanawake wa Kiislamu daima imekuwa mstari mwekundu kwa Waislamu hadi leo. Sasa mwanamke wa Kiislamu anaweza kudhalilishwa, kuvunjiwa heshima na kuuawa waziwazi, ilhali wale wanaojiita watawala wa Waislamu wanalifumbia macho jambo hilo. Dkt Nawaz alitoa mifano mingi ya kushangaza ya ukandamizaji wa kila siku wa wanawake kutoka al-Hind hadi al-Quds. Hata hivyo hili linawezekana tu kwa sababu ya kutojali kwa watawala wa sasa maneno ya Mwenyezi Mungu [إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ إِخۡوَةٌ [ “Hakika Waumini ni ndugu…” [ Al-Hujurat (49):10] na:
[وَإِنِ ٱسْتَنصَرُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ فَعَلَيْكُمُ ٱلنَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal (8):72].
"Utaifa ni ugonjwa unaoyavua ubinadamu mataifa na dola kiasi kwamba yanasimama kimya na kulemazwa katikati ya mauaji ya halaiki bila ya dhamira ya kisiasa ya kuchukua hatua isipokuwa ikiwa ni kwa maslahi yao ya kitaifa."
Taji Mustafa aliwakumbusha wahudhuriaji juu ya ulazima wa kusimamisha Khilafah kama mradi wa Ummah, kwa kuwa ndiyo kadhia yake nyeti. Zaidi ya hayo, ni lazima tuiondoe mistari ya utaifa tuliochorewa nyoyoni mwetu na wakoloni. Hatuna deni la utiifu wowote kwa mipaka hiyo yenye migawanyiko. Hatimaye, mistari ya ardhini, iliyochorwa na wakoloni wale wale wa Kimagharibi na kutekelezwa na tawala zinazoungwa mkono na Magharibi katika ardhi zetu ni lazima iondoke. Haina thamani ya yoyote ya kisheria na inatumika tu kutudhuru pekee.
Neno la mwisho ni kuzingatia urithi wetu.
Je, urithi wetu utakuwa ni kulia tu machozi kwa masaibu ya ummah wetu wakati machozi yetu hayatazuia maumivu ya kaka na dada zetu? Au ni kutoa tu sadaka ili kupunguza mateso ya ummah wetu, wakati pauni na dolari hazitamaliza mateso au risasi na mabomu kuwanyeshea ndugu zetu?
Au urithi wetu unapaswa kurudi katika njia ya Mtume wetu (saw) na Uislamu kupitia kusimamisha tena dola hiyo tukufu na uongozi wa Kiislamu ambao utakuwa ni mlinzi wa Waislamu wote bila kujali rangi zao, kabila, ardhi ya kuzaliwa au sehemu wanayoishi - dola ya Khilafah kwa njia ya Utume?
[مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعِزَّةَ فَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ جميعاً]
“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu.” [Fatir (35):10]
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk |