Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  24 Safar 1444 Na: 1444 H / 02
M.  Jumanne, 20 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Leicester haihusu Ubaniani na Uislamu, lakini inahusu Hindutva na Malengo yake ya Ufashisti kote Ulimwenguni

(Imetafsiriwa)

Machafuko ya hivi majuzi jijini Leicester kwa mara nyingine tena yameangaza mwanga kuhusu itikadi kifashisti ya mrengo wa kulia ya Hindutva. Ghasia za Leicester haziwezi kulaumiwa kwa mvutano kati ya jamii au mechi ya kriketi, kama ambavyo mabadiliko ya tabianchi hayawezi kulaumiwa kwa kutovaa makoti yalitengezwa kwa sufi. Kuna usuli wa masuala haya ambao hauwezi kupuuzwa.

Jamii ya Mabaniani na Waislamu jijini Leicester wameishi pamoja tangu miaka ya 1960 bila ya matatizo. Mahekalu ya jamii za Mabaniani na Wajain yamelaani vurugu zilizochochewa na Hindutva.

Sababu halisi ya mvutano sio ya kindani bali ni ya kinje; mfumo wa ubaguzi wa rangi, Hindutva, ambayo awali iliungwa mkono na RSS; shirika la wanamgambo wa Kibaniani wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu na dini nyingine za walio wachache. RSS na wafadhili wao katika serikali ya India wanachochea vurugu dhidi ya dini za walio wachache nchini India, wakichochea ghasia, mauaji na vitendo vya kigaidi. Waislamu wengi wameshambuliwa na kuuawa na makundi ya RSS kote nchini India, huku misikiti, wanawake waliovalia hijab na biashara za Kiislamu zikilengwa. Itikadi msingi ya RSS, ni India Kubwa, ambayo inahudumiwa vyema zaidi kupitia kuuondoa Uislamu na Waislamu kutoka India na kupanua mafanikio ya kimaeneo nje ya mipaka ya sasa ya India. Malengo ya Hindutva yamefupishwa katika kauli mbiu yao wenyewe "kuna maeneo mawili tu kwa Waislamu kwenda: ima Pakistan au qabrestan (makaburini)". RSS ilianzishwa na watu walioshajiishwa na ufashisti wa Mussolini na mradi wa Kizayuni nchini Palestina. Wakiwa bado hawajaridhika na ukandamizaji wao katika mitaa ya India, sasa wanatafuta kusafirisha ufashisti huu chini ya pazia la chuki ya Kibaniani kwenye mitaa ya Uingereza, inayoendesha shughuli chini ya jina HSS.

Pili ni muhimu kutambua kwamba kama vile Uzayuni hauhusiani sana na Uyahudi (viongozi wengi wa awali walikuwa wapagani), Hindutva ina uhusiano mdogo sana na mafundisho ya Ubaniani. Kwa kweli Mabaniani wengi waliojitolea kwa ubaniani wanapinga vikali malengo ya Hindutva.

Sauti za Hindutva zinakusudia jinsi nchi kama Pakistan, Saudi Arabia au Iran zinavyowatendea walio wachache ni pazia kwani hakuna anayeona mifumo yao kuwa ya Kiislamu. Pakistan ametekwa nyara na wanasiasa walio na hamu zaidi ya kupora nchi huku Saudi Arabia na Iran zikiwa na tawala ambazo zina nia zaidi ya kuzua mizozo ya kidini katika Mashariki ya Kati. Zote zinafanya hivyo kwa ajili ya kuwatumikia wakoloni wa Magharibi na kwa hakika si kwa ajili ya Uislamu.

Leicester leo, kwa mara nyingine tena inafichua ukosefu wa uongozi wa Kiislamu wenye maadili duniani. Ubalozi wa India na viongozi wa eneo hilo wanatetea maslahi yao ya kibaguzi, wakati serikali ya Modi inatumia ushawishi wake katika utawala wa Uingereza ili kupurukusha kutokana na uungaji mkono wake muovu kwa malengo ya Hindutva. Hata hivyo kukosekana kwa uongozi wa dhati wa Umma wa Kiislamu duniani, ambao uko tayari kutetea Waislamu na Uislamu, ni kwa mara nyengine tena uchungu ulio dhahiri kuuona.

Mtu ni lazima aulize ni nani aliye nyuma ya uchochezi wa Hindutva jijini Leicester? Una alama makhsusi ya tukio lililopangwa, kwa hivyo tunahitaji kuuliza ni nani anayefaidika nao? Je, umefanywa kuuchokoza umma wa Kiislamu ili kupata muitiko? Je, umepangwa na serikali ya Hindutva ya India kwa ajenda ambayo haijatangazwa?

Zaidi ya hayo, yanaruhusiwaje kutokea? Kwa nini majambazi wanaobeba silaha wameachwa peke yao na nyuso zao zimefichwa? Kwa nini polisi hawajasema kama ni kweli silaha zilikamatwa, kama mashuhuda walivyodai?

Waislamu wanapaswa kufahamu mipango mipana ya Hindutva, ili tusiingie kwenye mitego yao na kutumikia malengo yao bila kukusudia. Uislamu unatufundisha kujilinda sisi, wanyonge na wanaodhulumiwa, lakini unaharamisha kuwashambulia raia wa kawaida kwa kulipiza kisasi. Dalili za Kiislamu kuhusu wajibu wa Muislamu kulinda damu, mali na haki za raia wasiokuwa Waislamu hufichua uwongo ambao ni simulizi ya Hindutva inayodai Uislamu kuwa ndio tatizo. Historia imejaa visa vya Waislamu kuwalinda Mayahudi, Wakristo na hata Mabaniani. Mayahudi wameokolewa mara nyingi kutokana na ukatili wa Kikristo na kuwepo kwa mamia ya mamilioni ya Mabaniani nchini India kunaonyesha uwongo wa madai kwamba Waislamu wanataka kuangamiza dini nyingine zote kwa nguvu.

Serikali za kidemokrasia za kisekula zilimwondoa Mungu katika siasa kwa furaha, lakini matatizo yao yanaendelea kulipuka. Mnamo 2022, wafuasi wakaidi wa kisekula hawana jibu kwa matatizo yoyote makubwa tunayoyakabili leo. Ubaguzi wa rangi umesalia kuwa mwingi na ukuaji wa ‘Alt’ na mrengo wa kulia nchini India pamoja na Ulaya na Amerika unaonyesha kufilisika kwa siasa za leo. Badala ya masuluhisho angavu tuna uharibifu muovu, badala ya ukweli ulio wazi tuna mpindo wa kitaasisi, badala ya kuleta jamii pamoja tunaona hali ya kuingilia kati ya vibaraka wa serikali wanaounga mkono kundi la rangi moja ya ngozi dhidi ya jengine.

Njia pekee ya kuondoa usekula wenye kugawanya au mitazamo iliyojaa chuki ya kilimwengu kama vile Hindutva na Uzayuni mahali pao ni kwa uongozi wa kweli wa Kiislamu kuanzishwa. Ni Khilafah ya Kiislamu pekee kwa njia ya Utume ndiyo iliyo na maadili, masuluhisho na rekodi ya kihistoria ya kuzileta jamii mbalimbali pamoja, zikiishi kwa ustawi na amani pamoja. Hadi uongozi huu utakapoanzishwa kiulimwengu, Waislamu nchini Uingereza, ambao tayari wanachukuliwa kuwa raia wa daraja la pili chini ya sheria mpya za uraia, wataendelea kutupwa kwa mbwa mwitu.

[ٱلْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلْإِسْلَـٰمَ دِينًۭا]

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [(5):3]

Yahya Nisbet
Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu