Jumatano, 02 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  11 Jumada I 1445 Na: 1445 H / 07
M.  Jumamosi, 25 Novemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Misri: Harakisheni Muzikomboe Nafsi zenu na Palestina kutokana na Ukandamizi wa Kikoloni

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Uingereza kwa mara nyengine tena iliandamana mbele ya Ubalozi wa Misri jijini London mnamo Jumamosi, Novemba 25.

Mazungumzaji waliita suluki ya Magharibi kwa sheria za kimataifa kuwa ya kinafiki; kutarajia Waislamu kuziheshimu, huku wao wakiipuuza kila wanapoona maslahi. Muislamu hapaswi kuhisi kufungwa na sheria hizi na mipaka ya kiholela ya Kimagharibi. Bali tunapaswa kushikamana na Sharia ya Mwenyezi Mungu, ambayo haitambui mipaka bandia iliyoachwa na wakoloni. Mipaka hii ndiyo inayolizuia jeshi la Misri kutokana na kuitetea Gaza na kuikomboa Palestina, kana kwamba Waislamu wa Palestina ni watu tofauti na sio jukumu lao. Ilhali mipaka hii ni mistari tu kwenye mchanga isiyo na thamani kwa mtu yeyote, isipokuwa wale wanaotaka kudumisha mgawanyiko wetu.

Ummah wa Kiislamu lazima uwakatae watawala vikaragosi wanaotumikia maslahi ya Magharibi, huku wakitazama tu mauaji ya halaiki yakiendelea chini ya pua zao. Lazima tumteue kiongozi mwenye ikhlasi atakayeyahamisha majeshi ili kuwaokoa wahanga waliosalia wa Palestina kutokana na uvamizi katili wa Wazayuni.

Alhamdulillah, Ummah wa Kiislamu kote ulimwenguni ameonyesha mapenzi yao kwa Uislamu, kwani tulishiriki uchungu wa ndugu na dada zetu, kina mama na watoto wanaokabiliwa na kuchinjio na kulipuliwa kwa wiki sita sasa. Tumetambua kwamba wameteseka na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka 75, na tukakumbuka kuwa huo ni wajibu wetu wa Kiislamu wa kuwaokoa wale ambao hawawezi kujiokoa.

Tulikumbuka kwamba Al-Aqsa na viunga vyake vilivyobarikiwa haiwezi kutelekezwa na kwamba lazima tujitolee kumaliza ukaliaji huu wa kimabavu na ukandamizaji, bila kujali watawala wasaliti wanaosimama kama kizingiti njiani, na kufanya kazi mchana na usiku kusimamisha Khilafah Rashida ya pili na Al-Qudsi kama mji wake mkuu.

Hatimaye, tumezikumbusha nafsi zetu na watu wote waadilifu wa ulimwengu kwamba mipango yote ya amani ya kivipande na mapendekezo ambayo hayajaiva yamewasilishwa na wakoloni sugu ili kuchelewesha mwisho usioepukika wa utawala wao mbaya.

Sasa ni wakati wa kuongeza juhudi za kufichua simulizi iliyofeli ya mauaji ya halaiki ya Wazayuni na wafuasi wao. Sasa ni wakati wa kuwasilisha Sharia adilifu ya Kiislamu, inayotabikishwa na Khilafah kwa njia ya Utume. Hili ndilo suluhisho pekee linalokubalika kwa tatizo la Palestina na ndio njia pekee kuelekea kwenye amani ya kweli ya kudumu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu