Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 12 Jumada I 1443 | Na: 1443 / 06 |
M. Alhamisi, 16 Disemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Njama Nyengine Yafeli Dhidi ya Hizb ut Tahrir!
(Imetafsiriwa)
Mwenendo wa kihistoria wa kesi za Hizb ut Tahrir nchini Uturuki umejaa kashfa za kisheria. Hizb ut Tahrir iliorodheshwa katika Sheria ya Kupambana na Ugaidi kama shirika la kigaidi, licha ya kutotumia nguvu na silaha, na mara kwa mara ilisema haya katika machapisho yake na taarifa zake kwa vyombo vya habari, na licha ya kutohusika katika vurugu zozote tangu kuanzishwa kwake miaka 68 iliyopita, iliainishwa kama "shirika la kigaidi" kupitia sheria haramu. Wanachama wake wamehukumiwa adhabu kali!
Lakini mahakama na usalama, ambao hujifanya kama mbwa mwitu anayejaribu kumla mwana-kondoo, hupanga njama dhidi ya Hizb ut Tahrir kila mara, kupitia kauli za ulaghai na mbinu zisizo halali. Moja ya njama hizi zilijaribiwa wakati wa ukamataji mtawalia katika majimbo 23 ya Uturuki mnamo 24/7/2009. Mnamo siku ya Alhamisi, 23/7/2009, vikosi vya usalama vilimkamata Suleiman Ogurlu, ambaye alipokea hukumu yake ya mwisho katika kipindi hicho. Hata hivyo, Ogurlu, ambaye kwa mujibu wa sheria alipaswa kusomewa amri ya kunyongwa, na kisha kuwekwa gerezani, alizuiliwa kiholela katika Kurugenzi ya Tawi la Ankara la Kurugenzi ya Usalama ya Uturuki hadi Ijumaa asubuhi, 24/7/2009. Baada ya kukamatwa kwa Suleiman Ogurlu, polisi walipandikiza silaha na baadhi ya vifaa vya kijeshi katika makaazi yake rasmi. Na jina lake likaongezwa kwenye orodha ya ukamataji iliyofanyika mnamo Ijumaa, 24/7/2009, na idhini ya kupekuliwa nyumba yake ikatolewa. Wakati wa upekuzi wa nyumba hiyo, silaha na risasi nyepesi zilipatikana; picha na video zao zilichezwa kwenye vyombo vya habari chini ya kichwa "Silaha za Hizb ut Tahrir"!
Katika njama kama hiyo, maelfu ya watu walishtakiwa na mamia ya watu walihukumiwa. Suleiman Ogurlu alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na miezi 6 gerezani. Hata hivyo, baadaye uchunguzi na kesi dhidi ya shirika linalojulikana kama Fethullah Golan Organization (FATU) ulianza. Kama sehemu ya uchunguzi huo, Salam Tawhid, mkurugenzi wa tawi la upelelezi la Uturuki mjini Ankara, ambaye alikuwa zamu mnamo Julai 2009, ambaye alitia saini faili ya ripoti ya njama na kuipeleka mahakamani, alikamatwa na kuzuiliwa. Mwendesha mashtaka ya umma aliyesikiliza maelezo ndani ya wigo wa faili na kuandaa hati ya mashtaka, mwanachama wa Mahakama ya 11 ya Jinai ya Ankara iliyoamua kupekua nyumba hiyo, na hakimu ambaye alishiriki katika ukikizwaji kesi ndani ya wigo wa faili hiyo na anayejulikana kama "Jaji wa Mahakama Jumla" alifutwa kutoka wadhifa wake kwa sababu ya kujiunga na shirika la Fathullah Golan.
Chumba cha 16 cha Mahakama ya Upeo ya Rufani, kilicho tathmini pingamizi la faili ya rufaa, kuhusu matukio haya kuhusiana na vyombo vya utekelezaji sheria vilivyoibua hoja hiyo, Afisi ya Mashtaka ya Umma iliyokuwa imetayarisha hati ya mashtaka, na majaji waliokuwa wameendesha kesi hiyo kinyume cha sheria, zilibatilisha hukumu iliyotolewa na Mahakama ya 11 ya Jinai mjini Ankara mwaka 2017 zilisimamisha uchunguzi wa tuhuma za ulaji njama. Mahakama ya Tatu ya Jinai mjini Ankara, ambayo imekuwa ikichunguza faili hiyo kwa takriban miaka 4, iliwaachia huru Suleiman Ogurlu, Ercan Tekinbas, Hakki Irene na washtakiwa wengine katika mashtaka yote katika usikilizwaji wa jana. Hivyo, njama nyingine dhidi ya Hizb ut Tahrir imefeli!
Hizb ut Tahrir inajulikana ulimwengu mzima kwa fikra zake, njia na mitindo yake. Kila mmoja anayeijua Hizb ut Tahrir anajua kwamba inatafuta kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida na kwamba inatafuta kufikia lengo lake kupitia kazi ya kifikra na kisiasa. Wale wasiojua wanaweza kupata habari hii kupitia utafutaji rahisi. Ingawa kulikuwa na ukiukwaji 9 tofauti wa haki za binadamu katika uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba dhidi ya Hizb ut Tahrir, vikosi vya usalama bado vinatoa ripoti za usalama za kuchekesha kupitia akaunti ghushi kwenye Telegram. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu akipenda, hawatafikia malengo yao. Kwa sababu jua haliwezi kung'arishwa kwa matope.
(وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ)
“Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango” [Al-Anfal: 30]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |