Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 14 Jumada I 1443 | Na: 1443 / 07 |
M. Jumamosi, 18 Disemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mnazo Nguvu! Uislamu ndio Mwelekeo Pekee wa Kutatua Migogoro Yote
(Imetafsiriwa)
Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Uturuki ilikuwa ikipitia mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Lira ya Uturuki inazidi kushuka siku baada ya siku. Ingawa Jumatano hutangaza kuwasili kwa Alhamisi, lakini sera za kimakosa zilizotekelezwa kwa miaka mingi zinapungia mwaliko wa kuribisha migogoro. Ingawa kiwango cha ubadilishaji pia kimeongezeka, maafisa wanatazama tu yanayojiri, hata mshahara wa chini uliotangazwa na Rais Erdoğan kama habari njema kwa mwaka wa 2022 unabakia chini ya kiwango cha mfumuko wa bei unaopanda. Huku idadi iliyotangazwa na Erdogan ya kima cha chini cha mshahara ilikuwa lira za Kituruki 4253.4, ambayo ilikuwa sawa na $274 wakati huo, leo ni sawa na $258. Hali hii pekee inatosha kuonesha madhila makubwa ambayo nchi hii inakumbwa nayo. Haswa kwa kupanda kwa bei kunakotarajiwa katika mwaka mpya, mshahara wa chini hautawawezesha ndugu zetu wanaofanya kazi kukidhi hata mahitaji ya kimsingi.
Matamshi ya watu wengi na ahadi, pamoja na hofu ya kisiasa katika kukabiliana na mgogoro, yanasababisha nakisi ya bajeti kuongezeka hata zaidi. Jaribio linafanywa ili kufidia nakisi ya bajeti kwa kuwekeza mtaji wa kigeni au kukopa kwa kiwango cha juu cha riba, au kwa kuchapisha pesa bila ya fidia. Uturuki imekuwa na nakisi ya bajeti tangu 1970, na inaongezeka maradufu baada ya muda. Serikali ya AKP inazidisha nakisi ya bajeti kupitia matumizi ya kiholela. Kwa ujenzi wa barabara kuu, madaraja, mikondo, mahandaki, na matumizi ya fedha kwenye viwanja vya ndege na hospitali za mijini, nakisi ya bajeti imekuwa vigumu kufidia. Bila shaka, barabara, madaraja na hospitali ambazo wananchi wanahitaji zinapaswa kujengwa, lakini ndani ya mfumo wa uwezo uliopo. Pia, uchapishaji wa pesa bila fidia na miradi inayotekelezwa kwa kutumia madeni yenye riba kubwa huileta serikali katika hatua nyingine ya maafa. Mbali na uwekezaji usio wa lazima, ufisadi, hongo, na zabuni zinazotolewa kwa bei ya kiholela na ya duni, yote yanafanya mgogoro wa kiuchumi kuwa tokeo lisiloepukika. Kwa hiyo, ufisadi na ubadhirifu ndio visababishi, na nakisi ya bajeti na mgogoro wa uchumi ndio matokeo.
Katika siku hizi ambazo mfumko wa bei unazidi asilimia 70 kulingana na takwimu zisizo rasmi, lira ya Uturuki inapoteza thamani yake siku baada ya siku, watu wanakuwa na wasiwasi kwa sababu ya gharama kubwa ya maisha, Hizb ut Tahrir inatoa suluhisho sahihi na imara kwa msingi wa kuhisi uwajibikaji. Tofauti na vyama vyengine vya kisiasa, linatokana na fikra ya Kiislamu na sio Urasilimali, ambao ndio chanzo kikuu cha tatizo.
Kwa njia hii, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Uturuki, tutaeleza kwa kina jinsi ya kupunguza mfumko wa bei, jinsi ya kuzuia kupanda kusiko kwa kawaida kwa viwango vya kubadilisha fedha, jinsi ya kufufua biashara pasi na wawekezaji wa kigeni, jinsi ya kuondoa vikwazo katika kilimo ambacho kinakaribia kutoweka, jinsi ya kuondoa ukosefu wa ajira, na jinsi riba na soko la hisa zinavyonyonya wafanyakazi wetu, jinsi ya kuanzisha uchumi usio na kodi, na yale ambayo rasilimali msingi za uchumi zitajumuisha . Hivi karibuni tuwagawia umma kazi yetu yenye kichwa, "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Migogoro ya Kiuchumi katika Vifungu 10".
Katika utafiti huu tulioutayarisha kwa msingi wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu, tunapotoa ufumbuzi wa migogoro ya kiuchumi na kimaadili, hatukwenda katika mfumo mwingine isipokuwa Uislamu. Kwa sababu Uislamu ndio mfumo pekee wenye uwezo wa kutoa masuluhisho ya kweli ya matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kimaadili. Uislamu sio Dini inayowafungia watu misikitini tu! Uislamu sio Dini iliyofungwa kati ya mtu na Mola wake! Uislamu sio Dini ambayo lazima ikumbukwe kwenye hafla za kidini! Bali Uislamu ni mfumo unaoelekeza nyanja zote za maisha. Uliwanyanyua Waislamu zamani na kuwanyanyua kutawala dunia. Uislamu leo bado una nguvu ile ile! Kwani mfumo wa uchumi wa Kiislamu ndio njia pekee ya wokovu si kwa Waislamu tu bali pia kwa wanadamu wote walionaswa katika makucha ya urasilimali, ambao uliwafanya kupoteza hisia zao za huruma. Nyinyi si wanyonge! Kwa sababu Uislamu ndio mwelekeo pekee wa kutatua migogoro yote.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |