Jumamosi, 09 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  20 Muharram 1444 Na: 1444 / 03
M.  Alhamisi, 18 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wale Wanao Halalisha (Mahusiano) na Umbile la Kiyahudi Watapata Fedheha Katika Maisha Haya ya Duniani na Adhabu Kali Akhera
(Imetafsiriwa)

Tangazo la uamuzi wa kubadilishana uteuzi wa mabalozi lilichukuliwa kama moja ya hatua za mchakato wa kuhalalisha mahusiano unaoendelea kati ya Uturuki na umbile nyakuzi la Kiyahudi tangu mwaka jana. Wakati Waziri Cavusoglu aliposema: "Kama Uturuki, tumeamua kumteua balozi huko Tel Aviv. Uteuzi wa mabalozi pia utakuwa muhimu katika suala la kufikisha ujumbe wetu kuhusu Palestina na Al-Quds moja kwa moja kwa 'Israel'." Aliona umuhimu wa kusisitiza kwamba kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi hakumaanishi kuachana na kadhia ya Palestina!

Unapoangalia mahusiano tangu siku ya kuanzishwa kwake baina ya umbile la Kiyahudi na Uturuki, kila mtu anaona kwamba kumekuwa na matukio ambayo hayawezi kuelezewa hata kwa maneno ya kimsingi zaidi ndani ya kamusi. Matukio ya muongo mmoja uliopita pekee yanatosha kuelezea aibu na fedheha hii. Mifano yake ni pamoja na makubaliano yaliyofikiwa baada ya uzinduzi wa Rais Erdoğan wa "dakika moja", kushushwa kwa kiti cha balozi wa Uturuki, tabia ya aibu ya Uturuki dhidi ya ujambazi wa walowezi wa Kiyahudi, Waislamu kufungiwa Msikiti wa Al-Aqsa, kutangazwa kwa Al-Quds kama mji mkuu unaodaiwa wa umbile la Kiyahudi na taarifa za uongo za kulaani. Kama badali ya kuachana na kesi ya Mavi Marmara, masharti yaliwekwa ya kuomba msamaha kwa Uturuki, malipo ya fidia kwa familia, na kuondoa mzingiro uliowekwa kwenye Ukanda wa Gaza. Hata hivyo, aliyekuwa rais wa Amerika wa wakati huo Obama alisemekana kumfanya Waziri Mkuu Netanyahu aombe radhi kwa matamshi, na suala hilo likafichwa. Ilisemekana kwamba fidia ingelipwa, lakini ni vijipeni kidogo vilivyotolewa na umbile hilo nyakuzi, kama zawadi kwa badali ya damu ya mashahidi wetu, vilivyotumwa kwa familia kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali, sio kupitia serikali. Kwa hivyo, damu ya mashahidi wa Marmara iliuzwa kwa vijipeni kidogo vilivyotumwa na umbile nyakuzi kana kwamba zilikuwa ni pesa za msaada.

Bila ya kutaja kuondolewa kwa mzingiro wa Gaza; huku Ukanda wa Gaza ukiharibiwa kwa mabomu, maafisa wa Uturuki walikuwa wanazungumza juu ya manufaa ya kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi! Vilevile, mahusiano ambayo yalisitishwa katika ngazi ya balozi kwa ajili ya kukabiliana na mauaji ya Waislamu katika matukio yaliyozuka baada ya Marekani kuitangaza Al-Quds kuwa mji mkuu wa umbile la Kiyahudi na kuhamishia ubalozi wake huko mwaka 2018, sasa yameregea katika hali yake ya kawaida, na uamuzi unachukuliwa kumteua balozi wa Uturuki jijini Tel Aviv. Mahusiano yanawezaje kuhalalishwa tena, licha ya kuwa umbile nyakuzi bado halijapiga hata hatua moja nyuma?! Badala yake linaongeza ujambazi na kiburi! Uturuki ambayo inakabiliwa na kufilisika kisiasa, uharibifu wa kiuchumi, udhaifu wa kidiplomasia na ukosefu wa maadili, kwa mara nyingine tena imehukumiwa udhalilifu na fedheha, kwa sababu inataraji kupata msaada kutoka kwa umbile la Kiyahudi, kwani imeharibu hadhi na sifa yake machoni mwa Waislamu!

Hata kama umbile la Kiyahudi lisingegusa nywele za mtu hata mmoja huko Palestina, na lisingegusa matukufu ya Kiislamu, na kuifanya kuwa ardhi yenye ustawi zaidi ulimwenguni, kuhalalisha mahusiano nalo kamwe kusingekubalika. Pia linapaswa kupigwa vita hadi liondolewe mbali kwenye ramani na majeshi ya Waislamu. Jambo la kimaumbile ni kukomesha mahusiano yote na umbile hili ambalo Magharibi ililiunda na bado lingalipo kama kisu kilichokwama kwenye nyoyo za Waislamu, na kuyakusanya majeshi kuliondoa haraka iwezekanavyo. Leo, maafikiano yanayotolewa kwa umbile la Kiyahudi kwa jina la kuhalalisha  mahusiano huenda yakatoa uhalali kwa watawala wa Uturuki, lakini hatua hizi hazitatoa uhalali kwa umbile hili nyakuzi, ima kwa Mwenyezi Mungu (swt) au kwa waja Wake. Maamuzi na hatua zinazochukuliwa na watawala kamwe hazitabadilisha ukweli huu, na wanachokifanya ni udhalilifu na kushindwa kwao hapa duniani, na adhabu kali ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu zake Akhera!

(قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا * الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعاً)

“Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao? * Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri.” [Al-Kahf: 103-104].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu