Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 14 Muharram 1444 | Na: 1444 / 02 |
M. Ijumaa, 12 Agosti 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uhalalishaji Mahusiano na Utawala wa Assad ni Kushirikiana Nao katika Uhalifu Wake
(Imetafsiriwa)
Katika jibu lake kwa swali: Iwapo Rais Erdogan angekutana na Bashar al-Assad, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu alijibu: “Hakuna mawasiliano hayo kwa sasa...Kwa muda mrefu, Putin na maafisa wa Urusi walitaka mkutano kati ya Assad na rais wetu. Kuhusu Rais wa Jamhuri yetu, alisema kwamba mkutano wa (vyombo vya) Ujasusi ungefaa”. Katika Mkutano wa Nchi Zisizofungamana na upande wowote uliofanyika Belgrade, Cavusoglu alisema kuwa njia pekee ya ukombozi ya Syria ni maridhiano ya kisiasa, ambayo magaidi wanapaswa kumalizwa bila kujali wao ni kina nani, amani inapaswa kuwekwa kati ya upinzani wenye msimamo wa wastani na utawala, na kwamba Uturuki iliwasilisha kwa mwenzake wa Syria kwamba wanaweza kuunga mkono serikali katika hali hii. Katika taarifa ya pamoja ya Mkutano wa Nchi Tatu kati ya Uturuki, Urusi na Iran uliofanyika jijini Tehran mnamo Julai 19, na katika taarifa ya kufungia mkutano huo ya Erdogan na Putin mjini Sochi mnamo Agosti 5, na katika taarifa nyengine nyingi alizozitoa huko nyuma, tayari imesisitizwa: Ulinzi wa heshima ya kieneo ya Syria, kupambana na mashirika yote ya kigaidi, na suluhisho la kisiasa. Mazungumzo hayo ambayo yalifanywa katika ngazi ya kijasusi siku za nyuma na kwa sasa katika ngazi ya mambo ya nje, yamepangwa kuendelezwa na kuwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Erdogan na Assad katika siku za usoni. Haya yote yanamaanisha kuzikwa kwa mapinduzi ya Syria yaliyodumu zaidi ya muongo mmoja na kuupa uhalali na ubwana utawala wa Assad, ambao umewahamisha makazi yao, kuwaua na kuwakandamiza kikatili mamilioni ya watu wake. Zaidi ya hayo, dori ambazo nchi hizi tatu zimechukua katika mchakato huu mzima na mafanikio waliyopata tayari ni dalili tosha ya hilo. Waziri wa mambo ya nje Çavuşoğlu alifichua dhamira hiyo ovu katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana ambapo alisema: "Ili kuzuia mgawanyiko wa Syria, lazima kuwe na utawala madhubuti nchini Syria. Utashi unaoweza kudhibiti kila pembe ya eneo lake unaweza kupatikana tu kupitia umoja."
Inajulikana kuwa nchi za eneo hilo, haswa Astana Trio, zilicheza dori ya wazi katika kubakia hai kwa serikali ya Syria, ambayo Amerika iliistawisha, kuiimarisha na kuifufua ilipokuwa ukingoni mwa kutoweka. Ama dori ya Uturuki katika meza ya mbwa mwitu wenye njaa, ni kujipenyeza na kuyateka makundi ya upinzani kwa kuwakumbatia wakimbizi na kupata huruma kwa kutumia mazungumzo ya Ansari (walionusuru) na Muhajiroon (waliohama), na kuwapurukusha dhidi ya kuupiga vita utawala chini ya jina la vituo vya uchunguzi. Chini ya kisingizio cha kupigana na PKK, ilijishindia makundi ya upinzani upande wake na kuyakabidhi maeneo kama Aleppo, ambayo waliyaacha bila ulinzi, kwa serikali, na hata kufumbia macho kutawala kwao juu ya watu waliochoka huko Idlib, ambayo hatimaye ilipelekea kuhakikisha kwamba wameketi kwenye meza ya serikali katika vyumba vya hoteli na kumbi za mikutano kwa gharama ya maisha, damu na roho za maelfu. Hili si lolote bali ni kudhamini uhai wa utawala wa kihalifu.
Lakusikitisha, serikali ya Uturuki, ambayo inakabiliwa na udhaifu usio na kifani na kutokuwa na uwezo katika kutafuta maslahi ya kisiasa na matarajio ya kiuchumi, haswa katika kipindi cha hivi karibuni, inazungumza juu ya maridhiano ya watu wa Syria na kuhalalisha mahusiano na serikali, adui wa watu wake iliyo waangamiza kabisa, na adui wa watoto waliouawa kwa mateso huko Daraa, na watoto waliouawa; kwa kuchinjwa na kukatwa vipande vipande na shabiha (majambazi) huko Homs, na raia kuzikwa kwenye mashimo ya mauti huko Damascus, na wanawake ambao heshima yao ilivunjwa, na wale waliopoteza maisha yao chini ya mateso magerezani, na watoto waliokufa kwa mabomu ya kemikali, na miji kuharibiwa, na wakimbizi waliofukuzwa kutoka katika nchi yao. Hakika, huu ni mchezo hatari na njama ya kudhalilisha ambayo inashuhudiwa kwa mifano mingi katika historia, na wale waliohusika nayo hawaja na hawatafanikiwa kamwe. Ni wajibu kwa wale wenye akili, ufahamu na imani kutenda kwa utambuzi wa matokeo mabaya ya dunia hii na hatima ya Akhera, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Al-Aleem Al-Khabiir (Mjuzi wa yote) anasema:
[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللّٰهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]
“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim: 42].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: |