Jumapili, 10 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  18 Jumada I 1444 Na: 1444 / 05
M.  Jumatatu, 12 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kiini cha Mgogoro wa Nishati kiko Wapi?
(Imetafsiriwa)

Kama ilivyotarajiwa, kwa kuanza kwa msimu wa baridi katika nchi yetu, kuharibika kwa mfumo wa nguvu kumejitokeza tena. Lakini mgogoro wa nishati wa mwaka huu ni mkubwa kuliko hapo awali kwa sababu kuna habari kwamba idadi ya watu waliokufa kutokana na gesi ya carbon monoxide iliongezeka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Uvumilivu wa watu umejaa pomoni na kuonyesha kulaani vikali dhidi ya kukatika kwa umeme, kupunguza shinikizo la gesi au kuacha kabisa, kukata gesi na umeme kwa taasisi, na matatizo mengine katika uwanja huu. Kana kwamba hii haijawahi kutokea hapo awali, serikali ilianza kuchukua hatua za nasibu. Waziri wa Nishati, katika mahojiano na mwandishi wa habari, alipojibu maswali yake kuhusu suala hili, alitoa maoni yasiyo sahihi na ya upotoshaji, akikiri kwa sehemu kuwa serikali ndiyo inahusika na kiini cha tatizo. Kwa mfano, waziri alisema kuwa serikali inatia saini mikataba na kufanya mazungumzo kulingana na uwezekano wake wa kiuchumi. Mtazamo huo wa kimantiki unaonyesha kuwa serikali inalitazama tatizo la raia wake kwa upande wa maslahi ya kiuchumi na si kama tatizo la kibinadamu hata kidogo. Mwelekeo huu ni matokeo ya mfumo wa kidemokrasia unaotekelezwa na serikali. Waziri huyo pia bila kujali alisema kuwa mgogoro wa sasa ulionekana tu katika majira ya baridi! Kana kwamba hakuna shida kama hiyo wakati mwingine! Ni ajabu kwamba ikiwa mfumo wa nishati nchini haujapangiliwa kwa kuzingatia hali za majira ya baridi zaidi, basi ni hali gani iliyozingatiwa?! Je, majira ya joto huzingatiwa?! Kuna haja gani ya mfumo huo wa kizamani usioweza kuwapatia watu nishati wakati wanaihitaji zaidi?!

Katika mahojiano na BBC, waziri huyo alisema kuwa Uzbekneftegaz JSC inashirikiana na makampuni kadhaa ya kimataifa kutoka nchi za kibepari, kama vile kampuni ya kifedha, Rothschild & Co, kampuni ya Marekani, Boston Consulting Group, na kampuni ya kimataifa ya ushauri ya McKinsey & Kampuni. Ni serikali tu isiyo na utu na yenye khiyana ndiyo inayoweza kushirikiana na mashirika hayo ya uuaji, katili na yenye kupenda mizoga. Waziri huyo alieleza ni kwa nini “mapendekezo” ya makampuni hayo yanabaki kuwa siri kwa kuwa na kifungu (sharti) cha namna hiyo kwenye mkataba. Hii inatilia shaka hata zaidi.

Aidha, katika mkutano na waandishi wa habari, naibu waziri huyo hakuenda zaidi ya maneno, "hii ni siri ya serikali" alipokuwa akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu makampuni yanayomiliki maeneo ya gesi nchini Uzbekistan! Kwa kutia shaka zaidi, waziri huyo hakutaja kuwa Urusi inadhibiti gesi ya Uzbekistan, ambayo ni mhimili mkuu wa mfumo wa nishati nchini Uzbekistan, na kwamba tatizo la nishati nchini humo linasababishwa na uhaba wa gesi. Kinyume chake, aliwapotosha wananchi kwa makusudi na kusema kuwa serikali hufunga mikataba katika sekta ya nishati kwa misingi ya maslahi ya taifa pekee na ushawishi wa nje haukubaliki kabisa. Kwa kweli, serikali inatetea mkataba kwamba LUKOIL itamiliki 90% ya gesi ya Uzbekistan hadi 2046. Kwa kushajiishwa na mikataba hii, makampuni mengine ya Kirusi pia yanashindana kwa ajili ya gesi na nyanja zengine.

Udhibiti wa gesi ya Uzbekistan unaruhusu Urusi kushawishi sera ya ndani na nje ya Uzbekistan. Ambapo Urusi inatumia hitaji la watu wetu ambao wanaishi katika umaskini bila umeme na gesi katika siku za baridi za msimu wa kipupwe ili kuivuruza Uzbekistan katika miradi yake ya kisiasa na kiuchumi. Kwa mfano, Putin alivumbua mradi mwingine wenye tashwishi unaojumuisha Urusi, Kazakhstan na Uzbekistan (muungano wa gesi) na inazitaka kushiriki katika hilo. Na huku wakati ukiwa umefika wa kutoa jibu linalofaa kwa dola hii ya kihalifu ambayo imekuwa ikipora utajiri wa Asia ya Kati kwa karne moja, watawala wetu wamethibitisha kwa hakika kwamba wanajishughulisha tu na kuhifadhi mali na viti vyao vya enzi kwa kuamiliana nayo kwa wema. Hivyo basi, kipote tawala cha wanasiasa hakiwezi kutatua matatizo ya watu.

Kwa kumalizia, tunasisitiza kwamba Waziri wa Nishati alisema kuwa usambazaji imara wa nishati nchini Uzbekistan utapatikana tu pindi wa usasa wa mitandao na uchumi wa watumiaji wa nishati utakapohakikishwa na pindi uwekezaji mkubwa utakapofanywa katika sekta hii. Kutokana na hili ni wazi kwamba hata tatizo liwe la kina kiasi gani, serikali haina suluhu. Suluhu gani inaweza kuwepo ilhali serikali ya Uzbekistan inaupa kisogo Uislamu na hukmu zake zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu na kukabidhi mali ya umma kwa makampuni ya kigeni?! Waislamu wa Uzbekistan lazima watambue dhulma hii, na lazima wawajue maadui zao, na lazima watafute suluhisho la matatizo yao kutoka kwa Uislamu pekee, na lazima washirikiane na Hizb ut Tahrir ili kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Hapo tu ndipo watakapopata furaha duniani na Akhera, Mwenyezi Mungu akipenda.

[لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [As-Saffat: 61]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu